Serikali, TBS na wadau wa umeme wakae watengeneze viwango vya Kizalendo

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,902
52,003
Nchi za wenzetu mfano Marekani na Afrika ya kusini wadau wa umeme nikimaanisha wazalishaji umeme na wazalishaji na watengenezaji vifaa vya umeme wa ndani wamejiwekea viwango vya taifa vya bidhaa zao ili kudhibiti vifaa toka nje ya nchi ili vya viwanda vyao viuzwe.

Mfano marekani umeme wanaotumia ni ule wa volt 110.Wazalishaji wote wa ndani huzalisha vifaa vyote vya umeme vya volt 110 wakati nchi zetu na ulaya ni volt 220

Afrika ya kusini socket zao ni tofauti.Na hata sehemu za kuchomeka balbu ziko tofauti lengo ni kuhakikisha viwanda vyao vinazalisha na kupata soko.

Sisi hatuwezi kuwa na umeme wa VOLTI 100 na viwanda vya ndani vikaanza kuzalisha vifaa vya volti100 Kuanzia nyaya,nk?

Au tukaweka viwango vipya vya size za balbu zetu ziwe nyembamba mno kuliko zinazotoka nje na tuongee na viwanda vyetu kama ambavyo afrika kusini na marekani wamefanya?
 
Back
Top Bottom