Naibu Waziri wa Bishara Exaud Kigahe awatuhumu watumishi wa TBS kwa kupokea rushwa. Ataka wafanyabiashara wa kigeni wasakwe!

Mindyou

JF-Expert Member
Sep 2, 2024
2,093
5,566
Wakuu,

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe, amesema baadhi ya watumishi wa Wakala wa Vipimo (WMA) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wamekuwa wanapokea rushwa na kuruhusu bidhaa duni na kuendelea kuuzwa mitaani, hivyo kuhatarisha afya za watumiaji.

Akiwa ametembelea Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) na Wakala wa Vipimo (WMA) mkoa wa Singida, Naibu Waziri Exaud alisema:

"Maelekezo ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Selemani Jafo, ni kwamba ingieni mitaani kusaka bidhaa. Kama zinazalishwa mwende kwa wenye viwanda muwasaidie wazingatie sheria za nchi. Wale ambao hawatazingatia maelekezo ya serikali hatua zichukuliwe,"


"Unakuta raia wa kigeni anakodi nyumba lakini huko nyuma anazalisha bidhaa au anakodi godauni na kuingiza bidhaa kutoka nje ambazo hazina ubora halafu anatafuta vijana wamachinga wanaziuza kwa bei nafuu. Yaani wanakuwa hawana maduka rasmi wala leseni na hawalipi kodi ya serikali,"
alisema.

Naibu Waziri alisema lengo la serikali ni kuhakikisha viwanda vya ndani vinalindwa ili vizalishe bidhaa bora zenye ushindani kwenye soko ndani na la nje na kuzitaka TBS na WMA kutoa elimu kwa wazalishaji kuhusu ubora wa bidhaa wanazozalisha.


"Bidhaa ambazo zinazalishwa na baadhi ya viwanda ambavyo wakati mwingine havijulikani vimeingiliwa na hawa wageni lakini na wengine ni Watanzania na wanazalisha maeneo ambayo hayatambuliki na hazina nembo inayoonesha zimezalishwa wapi, "

"Tuwasaidie wajasiriamali badala ya kumdhibiti kwa kumfungia kiwanda. Tumsaidie kwanza kumwelimisha. Kumfungia si sifa maana mtu anakuwa amewekeza fedha zake,"
alisema.

Source: Nipashe
 
Hapo naona kama analalamika tu badala ya kuweka uchunguzi huo nani kabainika na kachukuliwa hatua gani?

Hili ndio tatizo la viongozi wetu, kuogopana au kutokujua
Unakamata mizigo, viwanda halafu ndio unakuja na ushahidi mzuri.

Watu wanababuka ngozi na hatujui nani aliingiza hayo mafuta
Leo hao masikini hata dawa sijui kama walipewa
 
Back
Top Bottom