SERIKALI TAMBUENI POMBE INAONGEZA AMANI NCHINI

NJALI

JF-Expert Member
Jan 9, 2014
1,534
1,090
Huenda baadhi wakakejeli, wengine wakapinga ila kwa uchunguzi nilio ufanya pombe inapunguza stress, hata kama hujala ukilewa unajisikia poa tu.

KUPIGA marufuku viroba, ili hali gongo ni haramu, pia bia ni ghali, maana yake watu hawata kunywa pombe, hasa wenye vipato duni kama Mimi.

kitakacho fanyika ni kuwaza maisha muda wote, hali ambayo itaongeza stress, uharifu, ili MTU apate pesa ya kunywa bia.

Serikali iliangalie sana hili la viroba, kuna watu bila kulewa kiroba hafanyi kazi kabisa, ni kama anakuwa teja.

Mimi nashauri vifungwe kwenye chupa kama soda za take a way na bei iwe buku, kuzuia kutaathiri pia uchumi. Mimi nakunywa, sijifichi na kauli ya waziri mkuu imeniathiri Mimi pia, hembu vigogo wa serikali tuineeni huruma japo tufarijike maisha magumu, bora ulewe uamke kesho na mapya, kuliko kukaa unawaza utakula nini.
 
Back
Top Bottom