Mtaji wa Serikali ni wananchi wakiwa na afya, elimu na makazi bora; uhuru, amani, upendo furaha na starehe

Shoctopus

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
3,434
1,985
Wanabodi Assalamu alaikum!

Nauliza bila wananchi kuwezeshwa ili wawe na 'disposable income' nani atanunua bidhaa za viwanda tunavyojenga?

Leo nimekuja na swali au mada kama ilivyo katika utangulizi na kichwa cha habari hapo juu na kwa maelezo zaidi kidogo kama ifuatavyo:

Kwanza nakubaliana na lengo na sera ya Mh. Rais JPM ya VIWANDA kama njia ya kuinua uchumi wa INCHI yetu ya TZ ili kufikia kiwango kinachoitwa "Uchumi wa Kati".

Pamoja sera ya uchumi kitaifa, lengo pia ni kuzalisha ajira nyingi na bora, pamoja na kuongeza kipato cha kila familia ili kuboresha maisha ya wananchi wote na kuondoa umasikini leo hii, kama sio jana!

Kuhusu hali ngumu ya maisha (ufukara) inayolalamikiwa na wananchi wengi wa kipato cha chini; watawala wamesikika wakisema hiyo ni gharama wanayopaswa kulipa ili tufike kwenye nchi ya viwanda na uchumi wa kati. Lakini hii ni kwa wananchi sio watawala ambao maisha yao kila mwenye macho anaona.

Gharama hiyo ni pamoja na kusitishwa nyongeza za mishahara kwa wafanyakazi wa Serikali na baadhi ya wastaafu kucheleweshewa au kutolipwa kabisa pension zao.

Wakulima na wavuvi kuandamwa na gharama za pembejeo na masoko duni ya bidhaa zao. Hapohapo kuwaongezea maumivu wakulima na wafanyakazi kwa makusanyo ya kodi mbalimbali, pamoja na vitu kama VAT, import duty nk. Ili Serikali igharamie starehe za watawala na kutoa 'huduma muhimu' kwa raia na miradi ya maendeleo ya INCHI, na VIWANDA. (Kwa maana kwamba hivyo tu, ndiyo mtaji wa MAENDELEO)

Sera hii ya kupunguza kipato cha wananchi wa hali ya chini na kuwaongezea gharama za maisha, matokeo yake ni kushusha (standard of living) kufukarishana wananchi wasiweze kununua hizo bidhaa za viwanda halafu Serikali nayo mwisho itakosa kodi ya kugharamia masurufu ya watawala, huduma za jamii na ujenzi na uendelezaji wa miundombinu na viwanda zaidi.

Kwa ujumla umasikini unaongezeka nchini, hivyo wananchi wasio na purchasing power hawawezi kufanikisha sera ya viwanda (industrialization) na hawawezi kuboresha maisha ya familia zao kiafya, kielimu, nk. Na Hali hii ikiachwa iendelee umasikini utajikita nchini vizazi na vizazi.

Itafika mahali tutashindwa kuhudumia na kuendeleza miundombinu mingi tunayoijenga sasa au tutaona miundombinu isiyo na viwango kama barabara na madaraja yanayobomoka wakati wa mafuriko.

Lakini ukweli zaidi ni kwamba purchasing power ya mwananchi lazima ifuatane na kipato cha ziada (disposable income) kwa maana ya fedha ya ziada ya kutumia kwa mahitaji kama sigara, pombe, muziki, sanaa, vipodozi, safari za burudani, furniture na makazi ya kisasa nk.

Vitu hivi ndiyo huongeza furaha kwa mwananchi na ndivyo mwananchi hawezi kulalamikia saana kodi zake. Kwamfano hivi sasa bei ya lita moja ya petroli ni T.Sh. 2,000/-. Lakini Bei ya Safari beer ni 2,000/- kwa nusu lita! Whiskey, Konyagi, na pombe nyingine halali kwa Bei ya chupa moja unapata suruali moja mpya ya dukani! (bidhaa ya kiwanda)
Kuna watu wanakunywa chupa kama hiyo moja kila siku, huku akivaa suruali ya mtumba ya elfu kumi! Si amefurahi? Serikali nayo si imekusanya kodi yake?

Wapi pia wanaotoa sadaka makanisani za laki mpaka milioni! Zote hizo ni 'disposable incomes' (halali) zinazochangia uchumi wa VIWANDA.

Ukiongeza bei ya bia/pombe kwa wananchi wenye afya nzuri, makazi bora, elimu na mishahara mazuri, wengi hawatajali, hawatalalamika. Lakini ukiongeza bei ya petroli au sukari amani inatoweka!

Maana yake ni kwamba mtaji mkubwa wa Serikali ni wananchi wenye afya na elimu bora, makazi bora, amani, upendo, UHURU, FURAHA na STAREHE!

Bila kuwawezesha wananchi wengi wale vizuri na kumudu mambo hayo muhimu ya maisha na kuwapa wengi 'purchasing power'; bidhaa nyingi za viwanda tunavyojenga zitanunuliwa na nani? Na bila soko la ndani bidhaa za viwanda vyetu si tutawapelekea wazungu au majirani zetu ambao wananchi wao wamewezeshwa?

Na hapa tunazungumzia viwanda vikubwa na vidogo vidogo huko vijijini tunakopeleka umeme. Bila malighafi, technologia, na masoko ya bidhaa zitakazozalishwa huko gharama za rural electrification zitarudishwaje?

Mtu asiyejua atapataje mlo wake wa leo na kesho, asiyejua atalipaje kodi ya pango, asiyejua maisha yake baada ya kustaafu atawezaje kuhudumia familia yake kwa afya bora, elimu bora, makazi bora nk. unategemea afurahie kulipa kodi (kunywa bia au kuunga mkono juhudi) badala ya kukwepa kodi ili kulisha familia yake?

Kama hayo siyo kweli hao wahujumu uchumi wanaoambiwa wakiri makosa halafu warudishe fedha (waliyofanya nini sijui) ni mafukara? Watu wa aina hiyo (matajiri wenye fedha isiyoeleweka chanzo chake) hapa TZ, nchi 'TAJIRI' au Bongoland, wapo wangapi?

Nionavyo mimi bila kuboresha MTAJI ambao ni maisha ya mwananchi kwa kumwongezea kipato cha ZIADA, mafanikio ya sera ya viwanda labda yatakuwa kwa wajanja wachache; haitafikia matarajio kwa walio wengi.

Najua kuna wenzangu baadhi mtasema heri wengi wapate kidogo kidogo kuliko wachache waneemeke. (Socialism vs Capitalism) Huo ni mjadala wa kale. Sasa hivi ni capitalism mbele kwa mbele na 'trickle down economy'.

Samahani, mimi sio mtaalamu wa Uchumi wala siasa. Mnategemea wasomaji hapa watakuwa huru kujibu watakavyo. Ndio misingi ya freedom of speech.

NAWASILISHA
 
Kuhusu hali ngumu ya maisha (ufukara) inayolalamikiwa na wananchi wengi wa kipato cha chini
Kwa ujumla umasikini unaongezeka nchini, hivyo wananchi wasio na purchasing power hawawezi kuboresha maisha ya familia zao kiafya, kielimu, nk. Na Hali hii ikiachwa iendelee umasikini utajikita nchini vizazi na vizazi.
Naunga mkono hoja, ila Watanzania huu umasikini uliotopea tumeuzoea, elimu sasa ni bure, maradhi ni mitihani ya Mwenyezi Mwenyezi Mungu, rushwa na ufisadi is an order of the day, tuko kama Kozi mwana mandanda, kulala njaa kupenda, mwezi October, sisi wenyewe katika Umoja wetu, kazi ni moja tuu, unachukua, unaweka, waa...!.
P
 
october ipo kama geresho tuuu. Kaka watakao endelea kutawala paka 2025 walisha chaguliwa mapema. Tuzidishe juhudi katika kufanya kazi kwan ndo mtaji wetu
Naunga mkono hoja, ila Watanzania huu umasikini uliotopea tumeuzoea, elimu sasa ni bure, maradhi ni mitihani ya Mwenyezi Mwenyezi Mungu, rushwa na ufisadi is an order of the day, tuko kama Kozi mwana mandanda, kulala njaa kupenda, mwezi October, sisi wenyewe katika Umoja wetu, kazi ni moja tuu, unachukua, unaweka, waa...!.
P

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom