Serikali: Stiegler's Gorge ipo katika ilani ya CCM

PAZIA 3

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
1,070
1,842
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati na umeme, Dr. Medard Kalemani wakati akijibu hoja za Nape Nnauye na kusema, ilani ya CCM imetaja miradi itakayoendelezwa ni pamoja na maji, gesi, upepo na makaa ya mawe, ilani haijataja mradi mmoja mmoja.
 
eti nasikia ilani ya sisiem ilitengenezwa na wapenzi wa ulipo tupo ndiyo maana imetupwa waliokalia mkeka wanatekaleza yao.
 
Hayo yamesemwa na waziri wa nishati na umeme wakati akijibu hoja za Nape Nnauye na kusema,ilani ya ccm imetaja miladi itakayoendelezwa ni pamoja na maji,gesi,upepo na makaa ya mawe,ilani haijataja mladi mmojammoja
Miradi na sio miladi
 
Mambo mengi tu hayakutajwa ndani ya ilani,ikiwemo ujenzi wa kiwanja cha mpira dodoma,ujenzi wa ikulu dodoma,ukuta mererani nk,hivyo sioni hoja ya kupingana na serikali
 
Isikurupuke kumjibu Nape kwa majibu ya jumla ije na maandiko kama alivyofanya yeye.... Serikali ya ccm inatikiswa na watu wepesi mno

Nape bwana..hao upinzani wenyewe wazee wa hoja kwa sasa wamekosa hoja wamebakiwa na demokrasia demokrasia, itakuwa yeye nape..amesahau gesi ya mtwara jk alishamaliza kila kitu hadi bomba likajengwa iende kinyerezi..ye anajifunika shuka kumekucha..

Magufuli alipoenda mtwara alitaka dangote aunganishiwe gesi kwa bei ya mtwara ambapo kiwanda kilipo na gesi ni km 10, badala ya kuuziwa kutokea dar..maana yake ni kuwa gesi ilishavutwa kwenda dar..

Wamakonde hawataki tena kusikia jinamizi la gesi maana waliongea ila wakaambulia vifo na ulemavu wa kudumu..

Nape wakati huo alikuwa Katibu wa itikadi na uenezi wa ccm..anajua kila kitu..
Akitaka gesi ibaki mtwara aongoze mapambano ya kupasua lile bomba linalokuja dar..aache kukumbusha watu machungu
 
Mambo mengi tu hayakutajwa ndani ya ilani,ikiwemo ujenzi wa kiwanja cha mpira dodoma,ujenzi wa ikulu dodoma,ukuta mererani nk,hivyo sioni hoja ya kupingana na serikali
Wanapingana na maendeleo hao wataka madaraka..vipi wanapotakaga rais asafiri? kwenye ilani ya ccm alisema atakuwa anasafiri kwenda Nje?
 
Back
Top Bottom