Serikali sikivu sikia hili pia.

Serikali sikivu sikia hili pia.

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,250
Reaction score
17,548
Leo kwenye hospitali moja iliyoko jimbo la Kawe nimeshuhudia ugomvi wa kati ya mtosha mshuru wa maegesho ya magari na ndugu wa marehemu aliyefariki kwenye hospitali hiyo wakati akipatiwa matibabu kwa takribani masaa 4 hivi.

Ndugu na majirani walimleta mgonjwa wao aliyeanguka ghafla, baada ya kumshusha mgonjwa wakikosa packing ndani ya hospitali, hivyo kuombwa waende wakapaki gari yao pembezoni mwa ukuta nje ya hospitali ambako ushuru wa maegesho unahusika. Wakiwa wako ndani ya hospitali wakisubiri matibabu ya ndugu yao kwa masaa 4 mshika ushuru aliendelea kufanya yake huko nje.

Bahati mbaya mgonjwa alikufa (rip) ndugu walipotaka kuondoka pale kwenda kufanya mpipango inayohusiana na marehemu wakakumbana na deni la maegesho la sh. 2000 wanalotakiwa kulilipa, na hapo ndipo chanzo cha ugonvi kati ya binti mkata ushuru dhidi ya ndugu za marehemu wakiungwa mkono na baadhi ya wagonjwa na watu wengine walioko karibu na tukio lile.

Jamani, ni kweli kwama serikali inahitaji hela kwa maendeleo, lakini kuwatoza kodi wagonjwa wanaosubiri na wanaopatiwa matibabu hospitalini sio jambo la kiungwana na kuwasononesha zaidi wagonjwa.

Kwani haiwezekani serikali kuacha kutoza kodi ya maegesho sehemu za hospitali?
 
Sio kila eneo serikali imeruhusu tozo za parking,sometime hivi vicampuni vinaenda kukusanya ushuri maeneo yasiyo rasmi ili kutunisha mfuko wao,
 
Sio kila eneo serikali imeruhusu tozo za parking,sometime hivi vicampuni vinaenda kukusanya ushuri maeneo yasiyo rasmi ili kutunisha mfuko wao,
kutoza kodi wanaoomboleza ni uhuni kama uhuni mwingine tu. Hii ni kodi ya aibu kwa wananchi wagonjwa walioko kwenye foleni ndefu za kusubiria matibabu. Kodi hii inawastahili wale walioko kwenye sehemu za starehere wanaopiga ugimbi
 
Back
Top Bottom