Serikali sasa kuelekeza lawama za matatizo yake kwa RCs na DCs | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali sasa kuelekeza lawama za matatizo yake kwa RCs na DCs

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Nov 25, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 25, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,457
  Likes Received: 81,692
  Trophy Points: 280
  Imetolewa mara ya mwisho: 25.11.2008 0007 EAT
  • Kuna tatizo serikalini-Pinda

  *Acharukia ma-RC, ma-DC, wakurugenzi
  *Asema migomo, maandamano ni kawaida

  Na Mwandishi Wetu
  Majira

  BAADHI ya watendaji wakuu wa Serikali mikoani hadi wilayani ni dhaifu na ndicho chanzo cha matatizo yanayoikabili Serikali hivi sasa, imeelezwa.

  Hayo yalisemwa jana na Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, alipokuwa alizungumza na wahariri wa vyombo vya habari ofisini kwake Dar es Salaam.

  Alisema usimamizi mbovu wa viongozi hao ndio umesababisha wananchi wasitatuliwe matatizo yao kwa wakati na hivyo kuleta migomo isiyokuwa na maana.

  "Baadhi ya wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri zetu, wapo kusubiri mishahara tu, hawatusaidii kabisa," alisema Waziri Mkuu na kuwataka waondoke ofisini na kwenda kusaidia wananchi vijijini.

  Bw. Pinda alisema kutokana na udhaifu huo, ndiyo maana kumekuwa na urasimu mkubwa katika kutatua matatizo ya wananchi, wakiwamo walimu na kusababisha wagome wakati ambao hawakutakiwa kufanya hivyo.

  Akifafanua kuhusu mgomo wa walimu, alisema utaratibu uliopo katika kushughulikia walimu wapya ni mrefu na hasa pale wakurugenzi wa halmashauri wanapopokea fomu za walimu hao na kukaa nazo mpaka ziwe nyingi ndipo wazishughulikie.

  "Hili kwa kweli limechangia katika matatizo haya, tunachokitaka ni Mkurugenzi akipokea fomu moja aipeleke kunakohusika, badala ya kukaa nazo mpaka eti ziwe nyingi.

  "Urasimu ndilo tatizo, tunajaribu kulikabili kwa kutumia wakurugenzi hao hao ili lisijirudie...pia tutafuata ushauri wa Rais wa kuingia katika kutumia teknolojia ya kisasa ya mawasiliano, badala ya kuendelea kubeba majalada haya ya kizamani, ili tuharakishe kuhudumia wananchi," alisema.

  Kuhusu malalamiko kuwa fedha zinazolipwa hazilingani na walimu walizokuwa wakidai, alisema ndiyo maana ya kufanyika uhakiki, na kwamba kila mwalimu aliyelipwa baadaye atapewa maelezo ya jinsi malipo hayo yalivyofikiwa, ili kuondoa malalamiko.

  Akizungumzia mgomo wa wanafunzi wa elimu ya juu nchini, Waziri Mkuu alisema kamwe Serikali haitakopesha wanafunzi wote kwa asilimia 100 kama wanavyotaka, kwa sababu kuna baadhi ya wazazi wenye uwezo wa kulipia watoto wao hata kama ni kwa kuchangia kiasi fulani.

  Alisistiza kuwa dawa ya mgogoro wowote ni watu kukaa chini na kuzungumza badala ya kutumia ubishi na nguvu na kusisitiza Kamati ya Pamoja ya Uongozi wa Vyuo Vikuu nchini (TAHLISO) na Serikali kuendelea kukutana na kujadili matatizo yaliyopo.

  Alivitaka pia vyombo vya Serikali kuwa makini katika kushughulikia matatizo ya umma, ili jamii isifikie kwenye migomo.

  Kuhusu mgogoro wa wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Waziri Mkuu Pinda, alisema pamoja na hatua kuchukuliwa kwa mazungumzo, bado kuna fukuto la malalamiko na hivyo Serikali sasa imeamua kumshughulikia mstaafu mmoja mmoja badala ya kundi.

  "Tumeamua kushughulikia mmoja mmoja ili tuchambue na kuwatendea haki, kwani kama kundi tunashindwa kujua yupi anadai kipi na ashughulikiwe vipi," alisema.

  Kuhusu kilimo, Waziri Mkuu alisema bado wasimamizi wa sekta hii hawajakidhi mahitaji kutokana na kutoelewa ni nini wajibu wao kwa wakulima na ndiyo sababu wanakaa ofisini bila kuwafikia wakulima na hawatumiki ipasavyo.

  Alisema ili kuleta tija katika kilimo, Serikali inafikiria kuanzisha mashindano ya uzalishaji kuanzia ngazi ya mkoa hadi mtu mmoja mmoja, ambapo Siku ya Wakulima ya Nane Nane mwakani, ndiyo itakayoonesha utekelezaji wake.

  Akizungumzia elimu, alisema bado kuna changamoto mbalimbali katika upungufu wa walimu hususan wa masomo ya Sayansi na kupongeza juhuydi za uanzishaji wa shule za awali katika shule nyingi za msingi nchini na ujenzi wa sekondari za kata.

  Kuhusu sakata la EPA hususan malalamiko ya baadhi ya watu ya kutaka wamiliki wa kampuni ya Kagoda Agricultural Limited wafikishwe mahakamani, Waziri Mkuu alitaka Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) aaminiwe.

  "Kama wengine wamefikishwa mahakamani na DPP huyu huyu, kuhusu Kagoda ataamua tu, kwani kutokana na mashinikizo haya yaliyopo, kila jambo litaanikwa tu ," alisema Waziri Mkuu.

  Akizungumzia kuliimarisha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), alisema ni kipaumbele chake na Serikali inahangaika kwa nguvu zake zote kuhakikisha kuwa ATCL inarudia kutoa huduma vizuri zaidi.

  Alisema inakabiliwa na matatizo mengi yakiwamo ya upungufu wa ndege, marubani na madeni mbalimbali ya mafuta na kadhalika.

  Kuhusu madai kuwa Serikali imelemewa, Bw. Pinda alisema hilo halipo na migogoro inayoendelea ni ya kawaida na ni changamoto ya Serikali kupambana nazo.

  "Haya yalikuwapo hata katika miaka mitano ya kwanza ya Rais Ali Hassan Mwinyi, mnakumbuka mihadhara mbalimbali na nini...miaka mitano ya awali ya Rais Benjamin Mkapa, pia kulikuwa na matatizo na hii ya Mzee Kikwete nayo ni hivyo, lakini katika miaka mitano ya pili mambo yatakuwa shwari," alisema.

  Akijibu swali kuhusu hatima ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Dkt. Edward Hosea na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. Johnson Mwanyika, kuhusu sakata la Richmond, Waziri Mkuu alisema itajulikana tu.

  Alisisitiza kuwa viongozi hawa nao wana haki ya kusikilizwa, hivyo lazima wasikilizwe ndipo hatua zichukuliwe. "Kuna mambo makubwa ya kufanyiwa kazi ma kutolea uamuzi si kama tunavyoliona."

  Akizungumzia kampuni ya reli ya TRL, alisema madai kuwa 'anaibeba' si sahihi na kwamba anaisaidia kwa kuwa ni chombo muhimu na nafuu cha usafiri wa wananchi wa kawaida hasa wa mikoani, lakini Serikali ina hisa nyingi, hivyo haiwezi kuikwepa.

  Akijibu madai kuwa Serikali ina matumizi makubwa ya magari ya kifahari, alikubali na kueleza kuwa anachoangalia yeye si gharama ya magari, ila ni kama magari hayo yanazalisha tija, kinyume chake hayana maana.

  Kuhusu kufungiwa kwa gazeti la MwanaHalisi huku Habari Leo likiachwa, Waziri Mkuu alisema Serikali ilichukua hatua baada ya kujiridhisha kuwa kilichofanyika na maelezo ya Mhariri wake hayakuwa yanatosheleza.

  Aliongeza kuwa Habari Leo, Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, analifanyia kazi na hatua zitajulikana kama alivyoahidi bungeni katika Mkutano uliopita Dodoma.

  MwanaHalisi ilifungiwa baada ya kuwataja kwa majina wenyeviti wa CCM wa mikoa minane nchini kwamba wamepanga kumng'oa Rais Kikwete katika kinyang'anyiro cha urais mwaka 2010 huku wakimhusisha mtoto wa Rais, Bw. Ridhwan Kikwete.

  Habari Leo katika habari inayolalamikiwa, iliandika kuwa baadhi ya wabunge (bila kuwataja) walipanga njama za kupinga msimamo wa Rais Kikwete kuhusu mapambano dhidi ya wezi wa fedha za EPA.

  Waziri Mkuu Pinda hata hivyo, alisisitiza wanahabari kuzingatia maadili ya taaluma yao ili kuepuka matatizo na migogoro kama hiyo hata kufungiwa.
   
 2. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #2
  Nov 25, 2008
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Hivi hawa wataacha lini kutoa sababu ambazo hazina macho wala mwelekeo?
  1. PInda ndiye alikuwa waziri wa Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa wakati hawa jamaa wanateuliwa, yeye ndiye aliwagroom.
  2. Wizara ya Tawala za Mikoa na serikali za mitaa ipo chini ya ofisi ya waziri mkuu ambaye ni yeye Pinda,
  3. kwa kuwa wapo chini yake anaweza kumwambia mkuu wa kaya awawajibishe any time
  4. Kushindwa kuwajibika kwa wakuu wa mikoa na wailaya ambao wako chini ya ofisi yake ni kuhindwa kuwajibika kwa waziri wa TAMISEMI na kushindwa kwa waziri mkuu kuwawajibisha inatosha kwa waziri mkuu mwenyewe kuwajibika, sasa nani atawafanya hawa jamaa wafanye kazi yao, waziri mkuu amekiri shindwa!

  Naona haya majibu hayajakaa sawa yamekuwa na mizengwe iliyopita kwa kupinda. Jamani kukubali kushindwa sio jambo baya ni jambo la uungwana tu, kama akina Tony blair walifika mahali waksema tuondoke kabla muda hujaisha, akina Festus Mogae (Botswana) Pamoja na kupendwa na wananchi wake na nchi yake kufanya vizuri sana kiuchumi lakini alijiuzuri hata Rais maarufu wa wakti huo wa Botswana Sir Ketumile Masire alistaafu. Mwanglieni Mbeki, kuisaidia Nchi amekubali yaishe kwani mumeona kuna maneno maneno huko??? hhaa shwari.
  Pinda hili Jibu lako sijui...... labda wapo wanaokuelewa, kweli unaenda kusema haya kwenye Vyombo vya habari????? siamini???? macho yangu???
   
Loading...