Serikali rekebisha haya mapema TRA

Serikali rekebisha haya mapema TRA

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,277
Reaction score
13,920
Serikali isipoangalia inaleta matatizo makubwa kwenye uchumi hasa ajira. Biashara ndogo ndogo hazikui vizuri

(1) Kodi wanazotakiwa kulipa

(2) Hawajui kutoa au kuweka rekodi za biashara.

Kinachotokea ni kwamba TRA sasa wakija kwenye biashara hasa ndogo wanakuja na namba zao za kulipa kodi kutokana na makadirio pekee na makadirio yao yanakuwaga hata mara tatu zaidi ya ukweli na hata ukibisha ili biashara yako isifugwe unatakiwa kulipa 33% kwanza!.

Biashara ndogo sio tu hazijui kodi vizuri wanazotakiwa kulipa lakini vilevile hawajui jinsi ya kutoa matumizi kwenye biashara zao mfano wanaonyesha mauzo bila kutoa gharama kama vile usafiri, mishahara, umeme, maji, manunuzi n.k

hii inasababisha walipe kodi kubwa kuliko uwezo na ukweli wa biashara. Biashara hivi zinaanza kwenda kwa harasa na baada ya muda zinakufa kwani ukweli ni kwamba kuna gharama nyingi sana za biashara lakini hakuna utaratibu wa kuweka takwimu. Serikali kwa kupitia TRA wanatakiwa;

(1) watoe elimu ya kodi

(2) Wasitoze kodi kwa makadirio.

Biashara hizi zikifa na kazi zinapotea haya ni mawazo tu
 
Ilinishangaza sana pale mwenye genge la mboga mboga na matunda alipokokotolewa kodi alipe sawa na mwenye mini supermarket ya jirani.
 
Nenda ofis yoyote TRA omba kitabu wanakupa, huwezi kulisoma likubwa kweli. Muda huna wa kulisoma.
 
Serikali isiko angalia inaleta matatizo makubwa kwenye uchumi hasa ajira. Biashara ndogo ndogo hazijui vizuri (1) Kodi wanazotakiwa kulipa (2) Hawajui kutoa au kuweka rekodi za biashara. Kinachotokea ni kwamba TRA sasa wakija kwenye biashara hasa ndogo wanakuja na namba zao za kulipa kodi kutokana na makadirio pekee na makadirio yao yanakuwaga hata mara tatu zaidi ya ukweli na hata ukibisha ili biashara yako isifugwe unatakiwa kulipa 33% kwanza!. Biashara ndogo sio tu hazijui kodi vizuri wanazotakiwa kulipa lakini vilevile hawajui jinsi ya kutoa matumizi kwenye biashara zao mfano wanaonyesha mauzo bila kutoa gharama kama vile usafiri, mishahara, umeme, maji, manunuzi n.k hii inasababisha walipe kodi kubwa kuliko uwezo na ukweli wa biashara. Biashara hivi zinaanza kwenda kwa harasa na baada ya muda zinakufa kwani ukweli ni kwamba kuna gharama nyingi sana za biashara lakini hakuna utaratibu wa kuweka takwimu. Serikali kwa kupitia TRA wanatakiwa (1) watoe elimu ya kodi (2) Wasitoze kodi kwa makadirio. Biashara hizi zikifa na kazi zinapotea haya ni mawazo tu
Biashara ndogo kutokuwa na uelewaa huo sio excuse lakini badala ya kulalama mi naona kama ni opportunity ya kibiashara mtu kama atajikita kutoa huduma za utunzaji wa mahesabu kwa biashara ndogo..Kutokujua sio excuse..Tuchukulie kama ni changamoto
 
TRA not user friendly. Hata wao hawajui wanachokitala. Full kumkandamiza mwananchi
 
Wapo wahasibu na wakaguzi wa hesabu watumieni hao watawasaidia badala ya kuwalaumu TRA
 
wenyewe wanakadiria tu hovyo wanatoa makadirio hawajali mteja hata mtaji wake ukiisha
 
Biashara ndogo kutokuwa na uelewaa huo sio excuse lakini badala ya kulalama mi naona kama ni opportunity ya kibiashara mtu kama atajikita kutoa huduma za utunzaji wa mahesabu kwa biashara ndogo..Kutokujua sio excuse..Tuchukulie kama ni changamoto
Tatizo wachangiaji wengine au kwa makusudi au si wafanya biashara Tra si rafiki wa mfanya biasha, someni mada mtaelewa wengine eti, Tumieni wahasibu mtaji wa laki nne unamlipa nini mhasibu.?
 
Tatizo wachangiaji wengine au kwa makusudi au si wafanya biashara Tra si rafiki wa mfanya biasha, someni mada mtaelewa wengine eti, Tumieni wahasibu mtaji wa laki nne unamlipa nini mhasibu.?
Ni pendekezo tu. Kama unaona halifai basi endelea kulalama subiri Yesu arudi. Sidhani kama unajua unachoongea. Hiyo biashara ya mtaji wa laki nne ambayo TRA wanaikomalia kodi ni biashara gani. Hebu toa mfano. Maana tunapenda kupotosha. Na pia wewe unamiliki biashara gani maana usiongelee wengine.
 
Ni pendekezo tu. Kama unaona halifai basi endelea kulalama suburu Yesu arudi
Mkuu si kulalama nadhani angalia mazingira ya wafanya biashara wadogo wanahitaji elim ya biashara Tra wanaonea wafanya biashara wadogo wanatozwa kodi zinazo wafilisi. Soma mada mkuu utaielewa
 
Mkuu si kulalama nadhani angalia mazingira ya wafanya biashara wadogo wanahitaji elim ya biashara Tra wanaonea wafanya biashara wadogo wanatozwa kodi zinazo wafilisi. Soma mada mkuu utaielewa
Nimekuuliza swali unamiliki biashara? Maana ulidai kwamba mimi nimeandika pumba.. Nikasema kwamba ni vizuri sasa biashara zetu ziwe na mahesabu ili kupunguza uonevu wa TRA. Wewe ukaja umekurupuka unaongelea biashara ya mtaji wa laki nne. Pendekezo langu ni kwamba kuwe na biashara za bookkeeping zinazo target SMEs wasio weza kuafford service za ma accountant wakubwa..
 
Tatizo la TRA wanakadiria kodi kulingana na mauzo hawaangalii gharama ambazo mfanyabiashara anatumia mfano: kodi ya chumba cha biashara, leseni ya biashara, fire, n.k. Mimi nina biashara ya Stationery wamenikadiria tsh 385,000 kwa mwaka, nikajaribu kuongea na mwasibu ili aweze kuniandalia maesabu, akaniambia nimlipe tsh 50,000 kwa mwezi, ambazo ni sawa na tsh tsh 600,000 kwa mwaka. Hizo gharama za kuwa na mwasibu ni kubwa wafanyabiashara wadogo hawawezi. TRA wangekuwa wanatoza kodi kwenye faida ingekuwa jambo jema.
 
Nimekuuliza swali unamiliki biashara? Maana ulidai kwamba mimi nimeandika pumba.. Nikasema kwamba ni vizuri sasa biashara zetu ziwe na mahesabu ili kupunguza uonevu wa TRA. Wewe ukaja umekurupuka unaongelea biashara ya mtaji wa laki nne. Pendekezo langu ni kwamba kuwe na biashara za bookkeeping zinazo target SMEs wasio weza kuafford service za ma accountant wakubwa..
Samahani u busy ulisababisha nisikujibu Mimi ni Contractor wa civil work & building na pia nafanya Office stationery na Supply wa office equipment, tools na timber yard. Ninachokisema nakijua hivi sasa nipo Tra Mapato kwa issue kama hizi za ukandamizaji kodi isiyolingana na kiwango halisi cha biashara. Wanakadilia bila kuangalia changamoto zipi zinamptia mjasiliamari, Na hali ni ngum zaidi kwa wajasiliamali wadogo. Mjasiliamari mdogo hana uwezo wa kumlipa mhasibu kukokotoa taarifa zake mwezi na mwaka
 
Poa mimi niko hapa Kibaha Tra naomba kuhamisha faili toka Shinyanga kuja kibaha na ambiwa niende Shinyanga kupeleka barua ya kuhamisha faili yaani ina maana Tra bado wanatumia manuel nikaomba kukadiliwa hapo sasa ni komoeni naomba zichapishwe form zenye vipengele kama vilivyotajwa juu,usafiri,kodi nk badala ya mhasibu mtaji mdogo utampa nini
 
Samahani u busy ulisababisha nisikujibu Mimi ni Contractor wa civil work & building na pia nafanya Office stationery na Supply wa office equipment, tools na timber yard. Ninachokisema nakijua hivi sasa nipo Tra Mapato kwa issue kama hizi za ukandamizaji kodi isiyolingana na kiwango halisi cha biashara. Wanakadilia bila kuangalia changamoto zipi zinamptia mjasiliamari, Na hali ni ngum zaidi kwa wajasiliamali wadogo. Mjasiliamari mdogo hana uwezo wa kumlipa mhasibu kukokotoa taarifa zake mwezi na mwaka
Kaka unakwepa hoja ya msingi. Soma uelewe nilichoandika. Narudia nimesema umefika wakati muafaka kuwe na services zinazotarget SMEs kwenye mambo ya book keeping kwa maana gharama zake zitakiuwa ndogo. Nimependekeza tu kama kuna mtu mwenye nia ya kuinvest kwenye hili. Wewe umengangana na kwamba biashara ndogo biashara ndogo. Sasa mimi nasema kuwe na accounting services zinazotarget biashara ndogo kwa gharama nafuu. Mwisho wa siku biashara bila records ni kupoteza muda. Bila ya hivyo TRA wataendelea kuwakadiria watu kodi kubwa. Sasa mtu atajuaje kuhusu ishu ya gharama zako kama huna mahesabu yeyote ya kuaminisha? Tutafute suluhu ya tatizo...Mimi nimependekeza hivyo. Wewe pendekeza ipi itakuwa ni hatua stahiki ya kupunguza tatizo. Maana mpaka sasa unalalamikia TRA bila kupendekeza hatua stahiki za kufanya aidha na wafanyabishara au TRA. Sema nini TRA wanapswa kufanya ili kujua kiwango stahiki unachopaswa kulipa kama huna mahesabu yeyote ya biashara?
 
Back
Top Bottom