Serikali, Rada na gazeti la Majira, Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali, Rada na gazeti la Majira, Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbunge, Jul 20, 2011.

 1. M

  Mbunge Senior Member

  #1
  Jul 20, 2011
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HVI kashfa hii ya rada na fedha zinazodaiwa kutoka Uingereza baada ya kusemekana maofisa wa serikali yetu walipewa chochote ili dili hilo lifanyike si iliwahi kuandikwa na gazeti la Majira linalomilikiwa na Business Times LImited, Tanzania kwenye miaka ya 1994. Nakumbuka kuwa wachapishaji na mhariri wa gazeti hilo walishtakiwa kwa kosa la uchochezi. Ni nani alikuwa mchochezi hapo. Na Watanzania na ubinafsi wetu hatuoni kwamba wanahabari hawa wa Business Times Limited walionewa na wanastahili kuombwa radhi na kupata kifuta machozi kwa mateso waliyopata wakati wa kesi yao ambayo leo inaonekana walikuwa wakiandika ukweli na ukweli mtupu!!!Je, serikali ya Uingereza nayo haioni kwamba pamoja na kuzirudisha fedha hizo kwa serikali, waandishi hawa wa habari wa Business Times Limited walifanya kazi nzuri na ili kuwapa mori na motisha waandishi wa leo lazima watu hawa watafutwe na kuzawadiwa pia na serikali ya Uingereza ili tusiruhusu serikali zetu kushirikiana kufanya madhambi at any time, any place in this world?
   
Loading...