Serikali piga marufuku tabia hii

Kiumbe duni

Senior Member
Dec 3, 2011
100
8
Kumekuwa na tabia ambayo imejitokeza na inayozidi kushika kasi pale ambapo yanapotokea maafa kuna baadhi ya medi na kampuni binafsi kujifanya ni waungwana sana na kuhamasisha wananchi kuchangia kupitia vyombo vyao. Serikali inajua jinsi Watanzania tusivyokuwa waaminifu, halafu inaruhusu (media,kampuni za simu za mkononi) binafsi kuendesha michango hii. Serikali hii inajua jinsi haya makampuni ya simu yanavyochakachua masalio yetu na kuendesha bahati nasibu za kizushi halafu inakaa kimya tuendelee kuibiwa. Serikali anzisheni utaratibu maalum yanapotokea maafa wananchi hata walio mbali waweze kuchangia moja kwa moja kupitia kwenu hivi vyombo binafsi viwe vinahamsisha tu, sio kuchukua michango. Wanachangisha kwa maslahi binafsi hawana wema hawa, Kama wameweza kuwaibia uso kwa uso wasanii wa muziki wa kizazi kipya sembuse sisi tunaochangi kwa kutumia simu za mkononi!. Wadau nawasilisha...
 
unaweza kuchangia pesa yote wanayochangisha??

badala ya kuzuia, ni bora kuongeza transparency na accountability
 
Hapa kuna Maslahi pia kwa anayejifanya kusaidia. Siamini kabisa ati sasa Makampuni kama ya Simu sasa yana huruma sana kuliko Mama Tereza wa Culcuta. Wizi mtupu.
 
ndo mana mimi sichangiagi kupitia mitandao mana naweza kuta namchangia mtu hela ya kukombolea gari yake bandarini, bora nitoe mchango wangu moja kwa moja kwa mhanga/wahanga km cdm walivyofanya.
 
Kuishaur serikal km hi ni kupoteza time yako! Huwez kumziba ng'ombe pua wakat mdomo uko wazi af ukajidai kua ng'ombe huyo atakufa! Ng'oo hafi....
 
Mi nachangiaga kwa imani tu kwamba mchango utafika kwa walengwa. Natoaga 500/-,tena kupitia Voda. Mabomu nilitoa na mafuriko pia. Cha muhimu through TCRA kuwe na accountability na transparency.
 
Back
Top Bottom