Wahandisi hutengenezwa wahandisi hawazaliwi hivyo kama kuna mtu anadhani uhandisi ni kipaji na kuna watu wanazaliwa wakiwa wahandisi huyo anajidanganya.
Jukumu la kutengeneza wahandisi ni la serikali
ili kupata mhandisi inahitaji mambo makuu mawili
1. mafunzo kutoka katika vyuo vinavyotoa elimu rasmi ya uhandisi
2. Practical experience isiyopungua miaka 5.
yaani unaweza kuwa na mtu amehitimu mafunzo ya uhandisi wa umeme lakini kama hajafanya mazoezi ya kutosha kuingiza nadharia katika vitendo basi mhandisi huyu mwenye nadharia tu anaweza kukucholea mambo mengi kwenye karatasi au kukuandikia mambo mengi lakini ukifungua kifaa cha umeme hawezi kukuonyesha hata fuse iko wapi. huyu si mhandisi bado maana mhandisi aliyekamilika anatakiwa kujua alama ya kitu kwenye karatasi kinafanana na practically kitu chenyewe kinafananaje.
unaweza kuwa na mhandisi wa majengo mwenye vyeti vizuri lakini hana practical experience anaweza kukutengenezea structural design nzuri sana kwenye karatsi lakini saiti haioni kama kweli kilichotengenezwa ni sahihi au la.
unaweza kuwa na mechanical engineer mwenye nadharia tu kichwani, akikaa kwenye drawing board anadesign gari lakini practicaly hawezi kuunda hata baiskeli.
maana yake ni kwamba ili taifa liweze kuwa na wataalamu hawa ambao ni nguzo kubwa katika uchumi wa taifa lolote inabidi kuweka mkakati wa kuwatengeneza na kuwatumia. mambo haya mawili yote yanaenda sambamba kwani kuwatumia ndiko huko kunawapa uzoefu.
lakini katika nchi yetu serikali imeshindwa kabisa kuweka kanuni zinazosimamia sekita zenye uhitaji wa wataalamu hawa ili kuhahakisha wanatumika na wanapata maarifa.
yapo mambo kadhaa ambayo yanadidimiza sekita hii katika nchi yetu
1. Ni muingiliano wa kada mbalimbali katika sekita za kihandisi. kwa kawaida sekita ya kihandisi ina kada ya chini kabisa ambayo ni yule mtu anayehitaji maarifa kidogo sana na kutumia nguvu nyingi na kada ya juu kabisa kwa yule mtu anayetumia nguvu kidogo sana na maarifa kwa wingi.
upo mkanganyiko mkubwa katika jamii kwa "laymans" kudhani yule anayetumia nguvu nyingi na maarifa kidogo ndiye anayefanya kazi na yule anayetakiwa kutumia akili zaidi pengine akiwa saiti haonekani akifanya lolote kumbe anatumia akili kuangalia kama kila kitu kinaenda kama kilivyopangwa. wakati akionekana mtu hafanyi lolote huwa tayari amekwisha kalili michoro akijua kila kitu kinatakiwa kwenda vipi na kujua ni njia zipi zinazotakiwa kutumika hivyo huwa wanakuwa wakifanya kazi vichwani mwao.
kadiri unavyopanda juu kutoka chini ndivyo kutumia nguvu hupungua na kutumia akili kukienda kukiongezeka.
mkanganyiko mkubwa ni katika maslahi au mishahara wanayotakiwa kulipwa kwa maana nguvu nyingi hulipwa kidogo na maarifa mengi hulipwa zaidi. hivyo waajiri wengi hupenda kutumia kada za chini kufanya kazi zinazohitaji kada juu ili walipe kidogo. Utakuta Technician ambaye ana uzoefu anachukuliwa na mkandarasi fulani ili achukue nafasi ya mhandisi kwa kuwa analipwa kidogo. hili ni tatizo kubwa hivyo serikaliinatakiwa kuweka taratibu zinazoonyesha kada fulani kwa maana ya vyeti na miaka ya uzoefu wanaweza kufanya kazi gani katika shughuli zote zinazofanyika katika taifa iwe sekita binafsi au umma na kuzisimamia. kanuni hizi zinatakiwa kuendana na mazingira ya nchi husika. yaani msikimbilie kusema mnahitaji watu wenye uzoefu wa miaka 30 na kulazimisha hivyo wakati katika taifa hamna na sheria inatumika kutoa ajira kwa wageni na kuwaacha watanzania vijiweni.
kwa tanzania yetu hili hakuna, unakuta sehemu technician au mtu anayetakiwa kuwa site foremen eti ndiye engineer incharge wa kazi.
2. Muingiliano wa taaluma mbalimbali.
wahandisi wamegawanyika katika makundi mengi. wapo wa ujenzi ambao wanatizama majengo na barabara, wapo wa maji wanaotizama miundombinu ya maji, wapo wa umeme wanotizama miundombinu ya kuzalisha, kusafirisha na kutumia umeme, wapo wa madini wanaotizama uchimbaji wa madini, wapo wa uzalishaji bidhaa wanaotizama uzalishaji, wapo wa mitambo kutizama mashine na kadhalika.
tatizo hapa limekuwa shughuli inayohitaji wahandisi wa aina tatu mtu anatumia mhandisi mmoja na huyo kumtumia kufanya kazi hata ambazo si zake.
mfano ujenzi wa nyumba unahitaji wahandisi wa aina tatu, yupo civil engineer ambaye ni structural engineer, yupo mechanical engineer kutizama plumbing na ac na yupo electrical engineer kutizama mifumo ya umeme.
lakini utakuta wakandarasi au washauri wa miradi au wamiriki wa viwanda au waajiri kwa ujumla anamuajiri mhandisi mmoja alafu huyo ndiye wanayemtumia kufanya shughuli hata ambazo si taaluma zake. hii ni hasara kwa taifa out put yake ni very poor na vilevile inaminya nafasi kwa wataalamu kuongeza ujuzi au uzoefu.
3. Serikali kuweka nguvu ya ziada kuzalisha na kutumia wataalamu.
kwa kawaida serikali inayotaka kutengeneza wataalamu wake na kuwatumia hujaribu kutumia kanuni au sheria kulazimisha shughuli zilizoko katika nchi yake au zinazotumia rasilimali yake hata kama ni nje ya nchi kutumia wataalamu wake. mfano nchi nyingi tajiri zinatumia mikopo na misaada kulazimisha wataalamu wake kwenda kufanya kazi katika nchi nyingine na huko wanafaninikisha fedha hizo kurudishwa au kuchuma zaidi na kupeleka kwao na kuendelea kufanya kazi na kuongeza ujuzi.
hapa tulitegemea serikali kutunga kanuni ambazo kila mradi unaofanywa na serikali kwa kutumia fedha za ndani au mikopo isiyo na masharti kipaumbele cha kwanza ni kutumia wataalamu wazalendo ili kubakisha fedha hizo katika mzunguko wetu na kuwajengea uzoefu, pili kutunga sheria za kuzuia kampuni yeyote ya nje kufanya kazi nchini bila kuingia ubia na kampuni za kizalendo, tatu kuhakikisha kila mradi unaofanyika wa serikali ni lazima uwe na wataalamu wa fani zote zinazohitajika pamoja na wanakuwepo kwa kila fani senior ili kuwatumia na kuwaongezea ujuzi na junior ili kuwapa uzoefu pia.
ni jambo la kusikitisha kuona viongozi wetu badala ya kuweka mifumo ya kutengeneza wataalamu na kuweka active taasisi ya kuregulate ubora wao ndio wamekuwa mstari wa mbele kuponda wataalamu wake kwenye jamii, kupigia debe wageni na kuwasema wazalendo kuwa hawafai. Viongozi hawa wamegeuka kama IMF na WB kwa nchi masikini wakiwatungia masharti yasiyotekelezeka na kuwalaumu kwa matatizo yaliyoletwa na mfumo.
Yupo bwana alidhani ni faida kutumia wageni kama wanataka kufanya kazi kwa gharama nafuu kuliko wazalendo na akadai wageni wanafanya kwa ubora zaidi.
binafsi nilimshangaa nikamueleza unatumia macho ya ki laymana kutizama jambo hilo. nikamueleza kwa uzoefu wangu wataalamu wazalendo wana ujuzi mkubwa ila wanakosa mitaji na wageni wengi wanakuja na kutumia wataalamu wa hapa hapa kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa hivyo swala la ujuzi halina mantiki ingawa kwa wenzetu unakuta mtu ameona miradi mingi na ameshiriki miradi mingi hivyo katofauti kadogo hakakosekani lakini nikamuambia labda jaribu kuchukua bilioni 10 serikali inataka kutekeleza mradi. chukua kumpa mkandarasi mzalendo ukampa masharti ya kutumia materials na vifaa vinavypatikana nchini kwanza na vile anavyokosa ndio anunue nje utizame effect ya fedha hizo bilioni kumi katika jamii kuanzia ule mradi uliompa na baadae kuifuatilia hiyo fedha inakokwenda ujiulize baada ya kujenga mradi fedha hiyo hiyo itafanya nini kwenye jamii yetu kupitia kodi na transactions na watataalamu utakaozalisha kupitia kuwapa watu wako fursa.
ulinganishe na kumpa bilioni kumi hizo mgeni utizame effect ya fedha hizo katika jamii yetu let say kwa miaka saba.
akasema kweli no matter how expensive a local contractor can be huwezi kupata faida zaidi kwa kutumia watu wa nje.
na hili ni tatizo kubwa kuwa tunakwenda mabenki ya kimataifa kukopa huduma na sio fedha. unapokopa fedha ukampa mgeni akachukua 90% ya fedha hizo akazirudisha ki msingi umekopa huduma sio fedha. ukikopa fedha kujenga mradi mmoja jaribu kuzipigia hesabu fedha hizohizo ziingie kwenye mzunguko wako kuleta manufaa zaidi ya mradi uliokopea na hili linaweza kufanyika kwa kutumia wataaalamu wazalendo na bidhaa zinazozalishwa katika nchi.