Kamwambie na mkwepa kodi Magufuli naye alipe kodi na awakamate mafisadi wote akiwemo Lugumi, mnunuzi wa kivuko uozo kwa bilioni 8, Idd Simba, wale wa Escrow na wengine chungu nzima ndani ya chama cha wahuni, majangili na mafisadi.
Mfumo wa ulipaji kodi ulikuwa wa hovyo hovyo Sana, inawezekana kodi jamaa analipa lakini wajanja kumbukumbu walikuwa wanapoteza, hilo pia liangaliwe ili tusiumizane sana hii ni nchi yetu sote.
sehemu kama hii ndio sura zenu halisi huonekana ,any endelea kuamini kuwa wapinzania wanalipa kodi ,and wanachosema ndio ukweli ,Ila najua unakimbia kivuli chako maana ukweli unaujua ...
Kivuli changu sikikimbii kwa maana nipo mastari wa mbele kulipa kodi zangu.Umemuulizia Mtoto wa Mbunge alipigwa miaka mingapi baada ya kukutwa na Nyara za serikali zenye thamani ya milioni 138??
Na Lugumi alifungw ajela gani??Au yule wa bilioni nane akatuletea meli mbovu amefungwa Maweni au Keko??
Akalipe pesa za Serikali manaomtetea ni kupoteza muda,huyuhuyu ndiye aliyekuwa mtukanaji wa Serikali kuwa haikusanyi mapato kumbe nae mkwepaji maarufu alipe tu na kama wapo na wa ccm walipe hakuna namna
Kuna wapumbavu sana ambao hawaoni uharamia na madhambi chungu nzima yanayofanywa na Serikali na chama chao cha wahuni. Huyo motto wa Mbunge ambaye ni jangili aliachiwa eti kwa sababu uchunguzi wa ujangili wake, "ungechukua muda mrefu"!
Yawezekana ni kweli Mbowe anadaiwa kodi, na wala siyo jambo la ajabu. Lakini inawezekana vipi kila mahali waseme alikuwa hajalipa kodi kwa miaka 5 au 10, ina maana huyo Mbowe alikuwa na nguvu gani ya pekee kiasi cha kuifanya serikali hii ya CCM kutomdai kwa miaka yote hiyo? Hapa ndiyo tunapata wasiwasi kuwa huenda kuna chuki binafsi.
Serikali inataka kutuaminisha kwamba Mbowe alikuwa ameiweka mfukoni serikali ya CCM chini ya JK kiasi cha kujifanyia chochote anachiotaka?
Hivi awamu hii, wasimamizi wakuu wa makusanyo ya kodi ni wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa? Hawa wakuu wa mikoa na wilaya ni makada wa chama, kwa nini wasiwaachie maafisa wa TRA wafanye kazi zao kwa mujibu wa sheria? Ninachofahamu ni kuwa ni Kamishna wa Kodi au maafisa wake kwa maelekezo yake wana mamlaka kisheria kufungia biashara zinazodaiwa kodi na kutoonesha dalili za kuweza kulipa kodi. Sheria zinasemaje kuhusu mamlaka ya DC kusimamia na kuadhibu wasiolipa kodi?
Kuna wapumbavu sana ambao hawaoni uharamia na madhambi chungu nzima yanayofanywa na Serikali na chama chao cha wahuni. Huyo motto wa Mbunge ambaye ni jangili aliachiwa eti kwa sababu uchunguzi wa ujangili wake, "ungechukua muda mrefu"!
Kubwa ni mwenzao.Watapata wapi pesa za kuhonga wakati wa chaguzi??Sera na ilani number moja ya hili lichama lamajangili ni wizi,rushwa na ufisadi.Mkullu yuko busy kuvisema vyama vya upinzani wakati cha kwake ni hovyo mara elfu
Kubwa ni mwenzao.Watapata wapi pesa za kuhonga wakati wa chaguzi??Sera na ilani number moja ya hili lichama lamajangili ni wizi,rushwa na ufisadi.Mkullu yuko busy kuvisema vyama vya upinzani wakati cha kwake ni hovyo mara elfu
Naamini Mbowe kama mwananchi mwingine yeyote anapaswa alipe kodi.
Lakini hivi awamu hii ambaye halipi kodi ni mbowe tu!!? Kuna ulazima wa kumuandama kiasi hiko!?
Kulipa kodi ni wajibu wa kila mwananchi. Haya ya mh Mbowe na serikali ya awamu ya tano ni kama hadithi ya askari trafiki wasio na maadili na madereva. Askari akipania kupata kosa atamuamrisha dereva hata kuwasha wiper hata kama mvua hainyeshi. Wafanyabiashara wasiolipa kodi nchi hii ni kibao.
U bark under the wrong tree...Umeshondwa kula nyama unang'ang'ania mfupa nyo***** nijibu habari ya makontena imeishia wapi na sio Kama hakukuwa na watu maarufu. If it's all about kodi mbona rais halipi kodi? Go to hell with your cheap thinking mind..
Unaweza kuthibitisha kuwa,rais halipe Kodi???, Je mbowe analipa Kodi??kwa mtazamo WA akili ndogo tu uliyonayo rais halipe Kodi ,kama nani tumeambiwa na tra mbowe halipi Kodi .Unataka tukuamini wewe nani?
Mambo yoyote yanayofanyika kwa chuki visasi hayana baraka. Tumeona Sumaye akinyanganywa shamba, wakati Mkapa ana shamba kubwa sana barabara ya baobab sec kwenda kibaha. Shamba halijalimwa miaka mingi sana. Mbona yeye hawamnyanganyi? Hii nikuwatia hofu viongozi wengine wasiiache CCM.
Unaweza kuthibitisha kuwa,rais halipe Kodi???, Je mbowe analipa Kodi??kwa mtazamo WA akili ndogo tu uliyonayo rais halipe Kodi ,kama nani tumeambiwa na tra mbowe halipi Kodi .Unataka tukuamini wewe nani?
MIEZI takribani mitano tangu aondolewe Bilicanas, siku moja tangu Serikali imzuie asiendelee na shughuli za kilimo katika shamba lake, jana tena Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, amepewa siku 14 awe amelipa kodi inayokadiriwa kufikia Sh. milioni 13.5 ya hoteli yake ya Aishi iliyoko Machame mkoani Kilimanjaro vinginevyo itafungwa.
Uamuzi huu mpya wa Serikali ya Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, umekuja ikiwa ni siku moja tu baada ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Gellasius Byakanwa, kutangaza kusitisha shughuli za kilimo katika shamba la Veggies analolimiliki Mbowe kutokana na kile alichosema kuwa lipo ndani ya chanzo cha maji ya Mto Weruweru.
Takribani miezi mitano iliyopita, Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lilivamia na kutoa vitu vyote katika jengo maarufu la Bilicanas lililopo Mtaa wa Mkwepu na Makunganya, Dar es Salaam.
Jengo hilo lililovunjwa wiki mbili zilizopita lilidaiwa kumilikiwa na familia ya marehemu Aikael Mbowe ambaye ni baba mzazi wa Freeman Mbowe.
Hata hivyo, NHC ilieleza kuchukua uamuzi huo kutokana na mteja wake (Mbowe) kushindwa kulipa kodi ya pango zaidi ya sh bilioni 1.172 ambayo ni malimbikizo tangu miaka ya 1990.
Ingawa Mbowe mwenyewe amepata kusema kuwa jambo hilo limefanywa kwa sababu za kisiasa, lakini alipolifikisha Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi, kesi yake ilifutwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mara baada ya kutembelea Hoteli ya Aishi, Mkuu wa Wilaya ya Hai, Byakanwa, alisema amepata taarifa kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa jalmashauri hiyo kuwa Mbowe amekwepa kulipa kodi ya huduma ya biashara kwa takribani miaka mitano iliyopita.
Alisema hali hiyo imesababisha halmashauri kushindwa kufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato.
Byakanwa alisema Serikali ya awamu ya tano imelenga kukusanya mapato ili iweze kutekeleza majukumu yake ikiwamo kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Alisema kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, mbunge huyo ambaye ni mmiliki wa hoteli hiyo iliyopo Kijiji cha Nshara, hajawahi kulipa kodi ya huduma licha ya kuandikiwa barua Januri 21, 2016 ya kumtaka kulipa kodi hiyo ambayo hakuijibu.
“Hatuwezi kufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato yetu ya ndani kama kuna wafanyabiashara wakubwa kama huyo wanakwepa kulipa kodi, na tena kwa kipindi chote hicho ameshindwa kuleta hali ya mauzo yake ambayo yataweza kujulikana kiasi anachostahili kulipa kodi.
“Hatufanyi hivi kwa kumwonea mtu, bali ni kwa mujibu wa sheria na endapo mtu atafuata sheria hakuna wa kumfuata, kila mtu ni lazima afuate utaratibu bila kujali cheo alichonacho,” alisema.
Alisema deni hilo lilipwe ndani ya siku 14 na akishindwa atachukua hatua ikiwa ni pamoja na kufunga biashara.
“Ikiwezekana tufafunga biashara hii, kwa kuwa amekuwa na tabia ya kutokujali kama nilivyomwita ofisini kwangu na hakufika na wala kujibu barua, sasa na hili puuzeni tutachukua hatua,” alisema Byakanwa.
“Mnaweza kusema kuwa DC labda anamwonea, mimi nakwenda na vielelezo na hapa pia nina taarifa nyingine kutoka Mamlaka ya Mapato (TRA) kuwa hajapeleka taarifa ya mauzo ili aweze kukadiriwa kodi kwa kipindi cha miaka mitano,” alisema mkuu huyo wa wilaya ambaye alikuwa ameambatana na Ofisa Mapato wa Halmashauri ya Hai, David Mlay.
Gazeti hili jana lilimtafuta Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai, lakini hakupatikana.
Jana hiyo hiyo MTANZANIA Jumapili lilifanikiwa kuzungumza na dada wa Mbowe aitwae Neel Mbowe, anayesimamia shamba la Veggies, ambaye alisema nyaraka na taratibu zote za umiliki wa shamba hilo anazo kaka yake huyo.
Kuhusu umiliki wa shamba hilo, Neel alisema lilikuwa likimilikiwa na babu yao tangu mwaka 1940 na baadae akampa baba yao, marehemu Aikael Mbowe.
Kwa mujibu wa Neel, walimua kulima katika eneo hilo ambalo lilikuwa pori kwa muda mrefu ili kuongeza ajira kwa vijana wanaolizunguka.
Kuhusu sheria ya mazingira na umiliki wa shamba hilo, alisema anayejua yote hayo ni kaka yake Mbowe.
Juzi Byakanwa alitoa amri ya kusitisha shughuli za kilimo katika shamba hilo lenye ukubwa wa zaidi ya hekari mbili lililoko Kijiji cha Nshara.
Byakanwa alimshutumu Mbowe kwa kufanya uharibifu wa mazingira kwa kuvuna miti ya asili bila kibali cha mkuu wa wilaya kulingana na uamuzi wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) pamoja na kuvuta maji kwa kutumia mashine kinyume na kibali na taratibu za utumiaji wa maji ya mfereji.
“Nasitisha shughuli zote za kilimo zinazofanywa katika eneo hili ambalo ni chanzo cha maji ya Mto Weruweru kuanzia leo (juzi) mpaka pale mamlaka nyingine zitakapojiridhirisha na utapaswa kulipa faini zote kulingana na sheria ya mazingira.
“Pia naliagiza Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kufanya tathmini ya uharibifu wa mazingira katika eneo hili na kuchukua hatua pamoja na kuniletea taarifa walizochukua. Maofisa maliasili wa wilaya wafanye tathmini ya miti iliyokatwa bila kibali na kuleta kiasi cha faini ndani ya siku 14,” alikaririwa Byakanwa.
Naamini kabisa kwamba kati ya watu wote wanao mtuhumu Mbowe kwamba halipi kodi!hamna hata mtu mmoja wapo aliewasiliana nae kusikiliza upande wake,Naamini kama angesikilizwa na kumpa nafasi kueleza ya upande wake tena kwa kwa kutoa nyaraka za udhibitisho!pengine hizi dhihaka juu yake sisingekuwepo, just for natural justice!ni dhambi kubwa sana kumhukumu mtu bila kumsikiliza kisa kaongea mkuu wa wilaya au Mkurugenzi Mkuu wa NHC! tuhuma sio kigezo cha ukweli na ndio sababu zinaitwa tuhuma, TAFAKARI
Na huyu mkwepa kodi anayepokea mshahara wa milioni 410!? Na wale mafisadi wa lugumi, boti uozo, Wabunge wapiga madili je!? Wao wanaruhusiwa kutofuata sheria za nchi!?
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.