Serikali na Mkopo wa Stanbic

lukindo

JF-Expert Member
Mar 20, 2010
8,466
9,028
Wana jf nawasalimu.

Hizi ni image (attachments) mbili tofauti na samahani kama nimeziweka kwenye jukwaa lisilo sahihi.

Naomba msaada hasa kwa wale wataalamu wa uchumi juu ya athari ziazoweza kujitokeza kwa serikali kukopa moja kwa moja kwenye benki za biashara.

Pia nashangaa kidogo kuona benki ikitumia kigezo cha kuikopesha serikari katika 'kuboost' biashara zake kupitia advert kama hili tangazo lilivyo kama nilivyoliona kutoka kwenye moja ya magazeti leo (Mwananchi).

Binafsi ninadhani 'adha' ya kukopa kwenye benki ingeliweza kuondolewa kwa Serikali kuondoa sehemu ndogo ya matumizi yake yasiyo ya muhimu na kuokoa USD $250m. Maana serikari yenye budget ya tririon 12 kuanza kukopa kiasi kama hiki cha pesa inaanza kutia mashaka kama kweli inaweza kufikia malengo yake.

Nawakilisha
 

Attachments

  • loan stanbic.jpg
    loan stanbic.jpg
    71 KB · Views: 49
  • loan stanbic advert.jpg
    loan stanbic advert.jpg
    48.9 KB · Views: 46
Sababu za kutoaminika kwa utafiti wa Synovate

Sunday, 07 August 2011 11:49

Alexander makulilo
TAFITI za kura za maoni ni muhimu sana katika nchi inayofuata mfumo wa demokrasia. Hii ni kwa sababu tafiti hizo hutoa nafasi kwa wananchi kutoa maoni yao juu ya masuala mbalimbali yahusuyo siasa, uchumi, utamaduni, na maisha yao kwa ujumla wake. Halikadhalika, viongozi wa Serikali na taasisi mbalimbali za umma na hata binafsi huweza kujipima kwa maoni hayo na kuboresha ufanisi wa shughuli zao.

Ikumbukwe kuwa msingi mkuu wa tafiti hizi ni sayansi. Hivyo mara zote taasisi yoyote inayojihusisha na tafiti hizi hujenga hoja kuwa matokeo yake ni ya kisayansi. Hii ina maana kwamba, hayafungamani na upande wowote. Kawaida sayansi huwa inafanywa kwa uwazi na kwa utaratibu maalumu kiasi kwamba njia ileile iliyotumika inaweza kurudiwa ili kuthibitisha ukweli wa matokeo ya utafiti fulani.
Hata kama taasisi iliyofanya utafiti ilikuwa na ajenda ya siri ya kupendelea, muda wote itajitetea kuwa misingi ya sayansi ilifuatwa. Na kwa mantiki hiyo kuna msemo wa kujilinda toka kwa watafiti hawa kuwa “utafiti hupingwa kwa utafiti mwingine.” Hoja hii haina maana kwani inaonyesha uoga tu. Zaidi sana ni ujanja wa kutotaka kuwajibika. Mara kadhaa watu wa kawaida wamekuwa wakitishika kwani hawana taaluma ya kufanya tafiti hizo achilia mbali uwezo wa kubeba gharama za utafiti ili kuja kupinga utafiti wa “kisayansi.”

Katika makala hii itajikita kujadili utafiti wa SYNOVATE uliochapishwa kupitia gazeti la Mwananchi la Agosti 4, 2011. Ninachambua utafiti huu si kwakufanya utafiti mwingine ila nitafanya ulinganishi mara fulani na utafiti wa SYNOVATE wa tarehe 10 Oktoba 2010. Ni kwakufanya hivi tutaweza kuelewa vyema ubora wa utafiti wa sasa. Makala itaangalia vitu vitatu (a) malengo ya utafiti, (b) vigezo vya kisayansi, (c) lugha ya ripoti.

Malengo ya Utafiti

Utafiti wa 4 Agosti 2011 ulikuwa na malengo manne. Kwanza ni lengo la kiutamaduni. Hili linahusu tathimini ya unywaji wa dawa za jadi. Pili ni siasa. Hapa utafiti ulitaka kufanya yafuatayo: Kupata maoni ya Watanzania juu ya utendaji wa taasisi za Serikali na zisizo za kiserikali pamoja na watendaji wake; kufahamu mapenzi ya Watanzania juu ya taasisi za Serikali na zisizo za Serikali na watendaji wake; kutathimini athari za mageuzi yaliyofanywa ndani ya CCM; na kufahamu maoni ya Watanzania juu ya mgombea urais uchaguzi mkuu ujao kupitia CCM.

Lengo la tatu ni uchumi. Hapa utafiti ulijielekeza kupata maoni ya Watanzania juu ya kero zinazolikabili taifa; na kutathimini athari za tatizo la umeme kwenye sekta ya biashara. Na lengo la nne lilikuwa kupata maoni ya wananchi juu ya mapenzi yao kwa watangazaji bora wa luninga (TV) na Radio kwa mgawanyo wa kijinsia.

Kwa sababu Synovate ni kampuni ya kimataifa iliyopo zaidi ya nchi 60 duniani na inajihusisha zaidi na tafiti za kibiashara, ni vema kuanza kutafakari malengo ya utafiti wa sasa kwa kuangalia mtazamo mpana wa falsafa ya Synovate.

Katika mtandao wa Synovate kuna maneno yafuatayo kwa lugha ya Kiingereza “Synovate is a global market research firm…A truly borderless company with offices in over 60 countries, our approach combines best in class global research capabilities with personalised service, local knowledge and the flexibility to create teams and processes that meet clients' specific requirements. At Synovate, our clients sit at the top of our organisational chart, driving us to continually develop more innovative research solutions that predict actual business outcomes” (Global Market Research | Synovate).

Ieleweke kuwa Synovate Tanzania ni tawi la mtandao huu mpana. Pia ifahamike kuwa Synovate ni kampuni linalojihusisha na tafiti za kibiashara. Na hufanya tafiti hizo kama biashara. Yaani biashara ya kuuza tafiti. Si vibaya kutumia tafiti kama bidhaa sokoni kwa kujipatia kipato. Ila suala la msingi ni aina ya utafiti.

Kwa mfano, kampuni ya simu za mkononi inaweza kufanyiwa utafiti ili kujua ina wateja wangapi na wanapendelea aina gani za huduma na kwa gharama gani ili kampuni husika iweze kujipanga kutanua biashara zake. Kwa sababu biashara ya kutoa huduma za simu ni ya ushindani mkubwa, kampuni inaweza kupata hali halisi, ingawa katika macho ya umma lingependa kujiita mtandao nambari moja Tanzania. Hata katika hili utafiti unaweza kupindishwa ili mradi matakwa ya mfanyabiashara yatekelezwe. Kwa sababu utafiti haupasiki kupendelea, basi kupindisha utafiti ni kosa kubwa na linaweza kupoteza weledi wa mtafiti.

Tofauti na utafiti wa kufahamu nani anauza nini, kanunua nini, na kwa sababu gani; tafiti zinazoigusa jamii moja kwa moja hususani suala kama siasa ni hatari sana kuzifanya kama bidhaa. Hatari kubwa ni kuwa mtafiti mara zote ataangalia masilahi ya malipo ili kutekeleza matakwa ya mwenye fedha na kutimiza haja yake. Mfano, kama kuna mwanasiasa au hata chama kina fedha nyingi na kinashiriki katika chaguzi, tafiti zinazoendeshwa kama bidhaa ni hatari kwani zinaweza kutumiwa vibaya kupoteza hali halisi na hivyo kuwaandalia wananchi viongozi.

Hapa ieleweke pia utafiti juu ya masuala ya biashara na ule juu ya masuala ya siasa ni tofauti. Hata mbinu za kiutafiti zitatofautiana. Kutaka kutumia mbinu za tafiti za biashara kuichambua siasa ni upotoshaji na matumizi mabaya ya tafiti.

Baada ya kuifahamu Synovate walau kidogo, sasa tuelewe malengo ya utafiti wake. Labda swali la msingi litakuwa nani ni mteja wa utafiti wa sasa. Yaani nani katoa fedha ili utafiti ufanywe? Synovate haionyeshi nani katoa fedha hizo. Kwa hakika si rahisi kuamini kuwa Synovate iliandaa malengo ya utafiti wake pasipo masilahi ya mteja.

Undani wa malengo
Hata hivyo ukiangalia kwa undani utagundua kuwa utafiti wa Synovate ulijikita zaidi kuangalia masuala ya siasa. Yale malengo ya utamaduni, uchumi na vyombo vya habari yalitumika tu kama mbuzi wa kafara. Kwa uhakika utafiti unaiangalia CCM. Hata hivyo tunaweza kujiuliza kwamba je, Synovate iliweza kutimiza malengo elekezi katika utafiti wake?
Niseme kuwa ni lengo moja tu la uchumi ndilo limeainishwa katika ripoti kwa ukamilifu.

Lengo la tiba
Lengo la masuala ya tiba za jadi lililenga zaidi kufanya kampeni ya dawa za babu maarufu kama “Kikombe”.
Inashangaza kuona kuwa ingawa vikombe vingi kama vya kule Mbeya, Tabora n.k, vimeonyeshwa Synovate waliendelea kupigia upatu “kikombe cha Babu wa Loliondo” na hata kuonyesha kwa kiasi gani watu wanapona. Vikombe vingine au hata tiba nyingine za jadi katika ripoti yake haionyeshi vinaponya kwa kiasi gani.

Hapa kuna upungufu wa Sayansi. Sayansi imeelekezwa Loliondo tu. Inaweza kuchukuliwa kuwa Babu au hata wenye masilahi katika tiba zake wametoa fedha ili tiba yake iweze kuthibitishwa “kisayansi.”

Lengo la siasa
Lengo la siasa lina shida kubwa. Inaonyesha fika Synovate hawaifahamu vizuri siasa ya Tanzania. Hapa nitaeleza vizuri wakati wa kujadili vigezo vya kisayansi. Iweje Synovate ianze kufanya utafiti wa nani atakuwa Rais baada ya Rais Kikwete wakati Serikali iliyochaguliwa haijamaliza hata mwaka mmoja madarakani? Na mbaya zaidi kwa nini malengo hayo yaangalie mrithi wa Rais ndani ya CCM? Hapa kuna fumbo na si utamaduni wa kisiasa uliozoeleka hapa nchini tangu Uhuru wa 1961.

Wasiwasi wangu ni kuwa lengo hili huenda limelipiwa na watu fulani ndani ya CCM kwa malengo fulani. Nisisitize kuwa vyama vya upinzani havikuwa katika malengo ya utafiti yaliyoainishwa na Synovate. Ni swali tena la mwisho lililopachikwa kupotezea lengo la madhumuni ya utafiti wa Synovate. Sina hakika kama CHADEMA au CUF vililipia utafiti huu ili malengo yao yatimizwe. Nashawishika kuamini kuwa vimetumiwa tu hapa ili kutekeleza mchezo wa siasa ndani ya CCM. Tatizo lingine katika lengo hili ni kuwa hakuna athari zozote zinazoonyeshwa kwa CCM kujivua gamba. Na pia hakuna tathimini ya maoni ya Wananchi juu ya utendaji kazi wa taasisi za Serikali au hata binafsi na watendaji wake kama ilivyoahidiwa. Lengo la nne juu ya mtangazaji bora wa kike na wakiume katika luninga na redio halionekani kabisa katika ripoti ya Synovate licha ya kuonyeshwa kwenye orodha ya malengo ya utafiti.

Vigezo vya kisayansi

Sasa tuangalie vigezo vya kisayansi katika kufanya utafiti huu. Tofauti na utafiti wake uliotangazwa Oktoba 10, 2010 ambapo Synovate ilikuwa walau wazi zaidi kuonyesha mbinu za kitafiti zilizotumika, katika utafiti wa sasa imeficha mbinu hizi hivyo kuleta mashaka kama kweli utafiti huu ulifanyika au walijifungia ofisini kwao na kuupika tu. Sina maana kuwa utafiti wa Oktoba ulitumia vigezo sahihi vya kisayansi, bali kwakulinganisha na wa sasa ule ni bora zaidi.

Kwa mfano, katika utafiti wa Oktoba, Synovate ilisema mgombea wa Urais kupitia CCM atashinda ilifanya hojaji na watu 2000 katika mikoa 21 tu ya Tanzania Bara. Hili lilikuwa ni tatizo kubwa kwani suala la Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linahusu Tanzania Bara na Zanzibar. Iweje Synovate ihoji upande mmoja tu wa Muungano? Huku ni kutofahamu mfumo wa upatikanaji wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika utafiti wa hivi karibuni Synovate haisemi hata idadi ya mikoa au wilaya au vijiji ambapo utafiti ulifanyika.
Hapa inakuwa vigumu hata kurudiwa kwa utafiti ili kuthibitisha ubora ua hata uhalali wa matokeo ya Synovate.

Pili, katika utafiti wa Oktoba, Synovate ilisema ilihoji kwa kuzingatia maeneo ya mijini na vijijini kwa alimia 60 vijijini na ailimia 40 mijini. Katika utafiti wa hivi karibuni asilimia zilizotumiwa kuonyesha uwiano huo hazionyeshwi jambo ambalo linotia shaka zaidi. Ripoti inasema tu utafiti ulizingatia maeneo ya mijini na vijijini.

Tatu, katika utafiti wa Oktoba Synovate ilionyesha namna ilivyofanya kuhakikisha ubora wa utafiti wake unafikiwa. Hii ni kinyume na utafiti wa sasa ambapo ubora huo hauzungumziwi. Hili linazidi kutia doa kwa utafiti huu.

Nne, ni hata juu ya muda wenyewe utafiti ulipofanywa yaani Mei 2 hadi Mei 29. Matokeo ya utafiti huu yametolewa takribani miezi miwili (2) baadaye. Hiki ni kipindi kirefu sana kutoa matokeo ya kura za maoni. Mara nyingi kura za maoni hutolewa haraka utafiti unapomalizika. Lakini cha kushangaza zaidi, ni kwa nini matokeo yatolewe katika kipindi hiki kukiwa na mfululizo wa matukio ya vikao vya CCM juu ya kujivua gamba? Na hata wengine wakiwa wameanza kujivua gamba? Haya ni maswali yanayohitaji majibu yakinifu ili kuamini utafiti wa Synovate.

Lugha ya ripoti
Suala la tatu katika uchambuzi wa utafiti wa Synovate ni lugha ya ripoti yake. Ripoti ya Synovate imeandikwa kwa Kiingereza. Hii ni lugha ambayo watu wengi hawaifahamu hapa nchini. Kama Synovate ilihoji watu wa vijijini ambapo lugha hii ni tatizo kubwa sana, iweje wasitoe ripoti kwa Kiswahili ili wahojiwa wapate mrejesho wa majibu yao na hata kuthibitisha kama kimeandikwa ni maoni yao? Sina maana hapa kuwa watu wote wa mijini hufahamu Kiingereza. Ikiwa wadau walipinga mswada wa katiba kuwa katika lugha ya Kiingereza iweje Synovate wasijifunze katika hili? Wangekuwa na ripoti ya Kiingereza na Kiswahili. Au ni maelekezo ya wateja wao?

Lakini zaidi sana nimeshangazwa na ukweli kwamba, hata Syovate wenyewe hawaifahamu vizuri lugha ya Kiingereza. Nitatoa tu mifano michache ya sentensi hizi kuthibitisha hoja yangu: “Which herbalists medicine have u ever taken (Page 4)?”; “Do you want Tanzania to a new constitution (Page 15)?”; “Who do you will be the next CCM flag beare come 2015? (Page 21).

Nilishtuka sana kuona kampuni inayojipambanua kama ya kimataifa inashindwa kuandika Kiingereza sanifu. Labda hili tatizo linaonyesha kuwa ni bora wangetumia lugha ya Kiswahili.

Hitimisho
Nihitimishe makala hii kwa kusema kuwa tafiti za kura za maoni si unajimu. Ni sayansi. Lakini kuaminika kwake mbele ya wadau ni lazima zifanywe bila kupendelea na ripoti zionyeshe wazi mbinu zote za kisayansi zilizotumika.

Taasisi zinazoendesha kura za maoni zisijaribu kujificha kuonyesha ubora wa kazi zake. Aidha ziache kuwatisha watu kuwa “utafiti hupingwa kwa utafiti mwingine.” Maana hata baadhi ya watafiti wasomi katika vyuo vikuu hapa nchini wamekuwa wakirudiarudia kauli hii lakini husimamia au husahihisha tafiti za wanafunzi wao katika ngazi tofauti, ikiwa ni pamoja na shahada za uzamili na uzamivu pasipokufanya utafiti mwingine kwanza. Iweje katika kuchambua utafiti wa kura za maoni tena unaotumia wiki mbili hadi tatu wa majibu ya “ndiyo”, au “hapana”; “najua” au “sijui”, “kakataa kujibu” n.k, tuhitaji utafiti mwingine? Ifahamike kuwa tafiti hizi huwa hazina hata uchambuzi wa kina. Huu ni ulaghai na upotoshaji katika tafiti.

Kwa kuwa tafiti za kura ya maoni zimepigiwa kelele sana hapa nchini, hasa katika uchaguzi uliomalizika wa mwaka 2010, nimeamua kufanya utafiti mkubwa unaohusisha taasisi zote za utafiti zimekuwa zikijishughulisha na kura za maoni. Utafiti umefikia hatua za mwisho. Utafiti huu unaainisha kwa kina kasoro za makusudi au za bahati mbaya zimezikumba tafiti hizi. Inatazamiwa utafiti huo utasaidia wadau kuboresha utendaji wao. Aidha utafiti huo utachapishwa na jarida la kimataifa hivi karibuni na wadau wote watajulishwa ili wajipime wenyewe na kujivua gamba.

 
Niliwahi kupropose serikali iwe na debt ceiling inayosimamiwa na bunge ili kuleta accountability na ufatiliaji wa mikopo tunayokopa watu hawakunielewa waacheni tu wakope. Hilo watakuja kulia watoto wetu na wajukuu zao na vizazi vinavyokuja. Kwa ufupi subiri nchi itawaliwe na mabenki mtalia na kusaga meno.
 
Back
Top Bottom