Hapo utachoka ndugu yangu.
Kuna siri kubwa sana katika hii issue ya Mafuta.
Hakukuwa na mantiki yoyote ile ya kupandisha kodi ya mafuta ya taa kwa lengo
la kukabiliana na wachakachuaji wa mafuta.
Kama uchakachuaji wa mafuta ni kosa, na ni kosa kweli, wahusika walitakiwa kushughulikiwa
kwa mujibu wa sheria na sio kupandisha kodi ya mafuta ya taa, ina maana wakipata
tecknologia ya kuchakachukua kwa mchanga watapandisha kodi ya nini? ya mchanga?
CCM walijua fika kabisa kwamba kupandisha kodi kwenye bei ya mafuta ni solution
ya kukabiliana na uchakachuaji wa petrol/diesel bila kuwakwaza wachakachuaji moja kwa moja.
kitu ambacho walikuja kukibaini siku ya cc yao ni kwamba haikuwa solution ya kushusha
bei fake ya mafuta (petrol/diesel) ambayo wameitengeneza kwa muda mrefu, na kwamba
ni bora bei ya petrol iliyochakachuliwa kuliko pure petrol kutokana pia na uovu ambao
wameisha ufanya, wanaujua vizuri sana mafisadi papa wakubwa hawa!!
Wanachotakiwa kufanya ni kushusha kodi ya mafuta ya taa haraka ili uchakachuaji
uendelee kwa manufaa ya UMA.