Serikali na CCM: Bei ya Mafuta ya Taa

Cha Moto

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
945
153
Rais Kikwete na serikali yake walipandisha bei ya mafuta ya Taa kwa kisingizio cha kuzuia uchakachuaji. Mwenyekiti Kikwete wa CCM, wamesema bei ya mafuta ishushwe! Jamani mbona sielewi, utendaji wa CHAMA na SERIKALI, nisaidieni, Kuna Tatizo hapa!
 
Hapo utachoka ndugu yangu.
Kuna siri kubwa sana katika hii issue ya Mafuta.
Hakukuwa na mantiki yoyote ile ya kupandisha kodi ya mafuta ya taa kwa lengo
la kukabiliana na wachakachuaji wa mafuta.

Kama uchakachuaji wa mafuta ni kosa, na ni kosa kweli, wahusika walitakiwa kushughulikiwa
kwa mujibu wa sheria na sio kupandisha kodi ya mafuta ya taa, ina maana wakipata
tecknologia ya kuchakachukua kwa mchanga watapandisha kodi ya nini? ya mchanga?

CCM walijua fika kabisa kwamba kupandisha kodi kwenye bei ya mafuta ni solution
ya kukabiliana na uchakachuaji wa petrol/diesel bila kuwakwaza wachakachuaji moja kwa moja.
kitu ambacho walikuja kukibaini siku ya cc yao ni kwamba haikuwa solution ya kushusha
bei fake ya mafuta (petrol/diesel) ambayo wameitengeneza kwa muda mrefu, na kwamba
ni bora bei ya petrol iliyochakachuliwa kuliko pure petrol kutokana pia na uovu ambao
wameisha ufanya, wanaujua vizuri sana mafisadi papa wakubwa hawa!!

Wanachotakiwa kufanya ni kushusha kodi ya mafuta ya taa haraka ili uchakachuaji
uendelee kwa manufaa ya UMA.
 
Hivi kuna mtu ameshakaa akafikiri kama lile punguzo la kodi kwenye mafuta ya diesel na petrol halijawa just offsetted na ongezeko la kodi kwenye mafuta ya taa? Hivyo hakuna kilichopungua badala yake ni just shifting of cost kuto kwa wenye magari kwenda kwa wenye vibatari?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom