Serikali moja ni suruhu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali moja ni suruhu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Head teacher, May 4, 2012.

 1. Head teacher

  Head teacher JF-Expert Member

  #1
  May 4, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,811
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nimecheka sana jana nilipokuwa naangalia itv, pale kikundi cha uamsho kilipopigwa stop na kutoa maoni kuhusu kuvunja muungano. Kwa jinsi jamaa walivyokuwa mbogo kutaka kuvunja muungano, hebu tusubiri leo watakuja na single gani. Na ikumbukwe kuwa kuingilia majukumu ya tume ya warioba ni kosa la jinai.

  Mimi niwatoe hofu uamsho znz, kuwa sisi wabara tutapendekeza serikali moja, hivyo hakutakuwa na kero za muungano.
   
 2. Petiro

  Petiro JF-Expert Member

  #2
  May 4, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 312
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hata mm nasupport serikali moja ya JMT na serikali za majimbo chini ya governer
   
 3. GEMBESON

  GEMBESON JF-Expert Member

  #3
  May 4, 2012
  Joined: Apr 15, 2012
  Messages: 256
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Usi2mie masaburi ww, Peleka hayo mawazo yako kwa Wariba. Na hayo sio mawazo ya wabara. mbona mimi ni mtanganyika na mawazo yangu nitakayompa warioba ni kwamba napendekeza serekali tatu. Usihalarishe mawazo yako kwa kuwa wewe sio msemaji wa wabara.
   
 4. l

  lum JF-Expert Member

  #4
  May 4, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 343
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  kuhusu UAMSHO leo wapo uwanja wa maisara mchana huu anotaka kuwazuiya na aende sasa hivi kabla hawajamaliza

  nawapenda hawa jamaa wanajiamini,wanajua sheria,wanakubalika zanzibar na kila kanda ya jamii ,wanajua wanachofanya na wanaongea point tupu kisha wanaamsha zanzibar (kwa pamoja tutashinda) non stop mpaka kieleweke.


  kama atatokea mtanzania kutaka serekali moja huo ndio uhuru wa kutoa maoni...lakini kwa wazanzibar hilo halipo kabisaaaaa na kama likitiwa kwenye katiba bure kwa sababu mwisho kuna kura kila upande peke yake tanganyka na zanzibar
   
 5. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #5
  May 4, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,112
  Likes Received: 1,499
  Trophy Points: 280
  zanzibar wapewe uhuru wa kuamua ama wanataka muungano hau hawataki kama hawataki tuwaondoe na waondoke huku bara warudishe na ardhi yetu pamoja na fursa zote walizopata kupitia muungano lakini kama wanataka muungano ama wakubaliane na muundo tulionao au tuwe na seriksli moja wasitutishe kwani wao wanahitaji muungano kuliko sisi tunavyohitaji na wako salama zaidi tukiwaachia watachinjana pemba na unguja hizo porojo za serikali tatu wakati hawachangii chochote kwenye kuendesha serikali ikiwa ni pamoja na kushindwa kulipa umeme kusoma bure elimu ya juu na bado hawaridhiki
   
 6. k

  kicha JF-Expert Member

  #6
  May 4, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 511
  Likes Received: 536
  Trophy Points: 180
  acha mawazo mgando ayo fikiri kama great thinker sio kukurupuka tu, kama kuzuia kuchinjana mngezuia arusha na mwanza, suala la kuchangia muungano fatilia tume iloundwa kuchunguza matumizi baina ya serekali mbili sio kuropoka tu, suala la umeme jiulize kwa nini smz walikataa kulipa deni hadharani bila ya hatua zozote kuchukliwa[ sheria ndio iliwalinda], wewe ni wale mnaohadithiwa halafu ukawa una nguvu ya kuongea bila kujitambua kama ni pumba tupu huku vipovu vikikutoka, acha uvivu ili uwe na nguvu ya kuongea utafiti ni lazima ili usichekwe, eti wazenji tunawabeba... hivi hujiulizi ni kwa nini wananchi walio wengi wanaulalamikia uko kutubeba? tumia akili kufikiri, suala la wazenji walio bara sidhani kama una point bcs huku kwetu vilevile mpo wengi tu na tumeshazaana binafsi ndugu zangu ni wabara lkn hii sio sbb ya kutowaskiliza wazenji au wabara kuamua hatma ya muungano wanoutaka au la,
  Angalizo ni kua kama wewe unastahili kua hapa jamvini basi tafuta mapungufu au pointi zenye ushahidi uweze kujadili bila ya kejeli bcs mwisho wa siku sisi ni ndugu au watu tuliopakana karibu zaidi, uhasama wowote tutakaouanzisha utapelekea machafuko ya wasio na hatia ambapo mimi wewe na mwengine tutakua wahanga wakubwa.
   
Loading...