Umemaliza chuo kwa mkopo, elimu uliyopata ni mbovu haikukuandaa kujiajiri tatizo ni serikali ndo inaandaa mitaala. Umekuja mtaani ajira hakuna, serikali "inayotujali" imeamua kusitisha ajira. Okey poa sio wote wataajiriwa serikalini unaamua kuomba private sector unasikia kampuni zimefungwa, sababu nini?serikali inayotujali imeweka sera mbovu za ulipaji kodi wawekezaji wanakimbia. Option iliyobaki ni kujiajiri kwa mtaji kidogo na kukopa mkopo, huko tena serikali hairuhusu mdaiwa "sugu" wa bodi kukopeshwa. Isitoshe unasikia watumishi hewa 19,000 watu hawaajiriwi na tumeokoa mabilioni, lakini hela hakuna na serikali inakopa...unaamua kujiajiri na hela kidogo unapigwa kodi karibu nusu ya mtaji hata hujaanza biashara lakini tena unasikia kampuni kubwa zinapewa miaka 5 kutafuta wateja lakini wewe hata wiki hupewi..umekaa unawaza unasikia picha yako itawekwa kwenye magazeti, unajiuliza kwa gharama zipi? Unalalamika unaambiwa ni mpiga dili wakati hata kazi hujapata. Unawaza je hela za ndege vijana wangekupeshwa kwenye vikundi ingekuwa imesaidia vijana wangapi kujiajiri?Vijana wa chato wangekopeshwa kwa hela zilizojengea uwanja je ni familia ngapi zingekwamuliwa kutoka katika umasikini? Unahoji unaambiwa kafanye kazi acha siasa, kazi gani ukafanye sasa ukalime bila mvua na mtaji? Je mnataka vijana tuwafikirieni vipi?