Serikali: Miaka 2 ya Rais Magufuli, tumeongeza ari na nidhamu kwa watumishi! Mapato yapanda toka trion 9.9 hadi trion 14

Pia tunajivunia sukari ilikua 5000 lakini imeshuka hadi 3000 na inaendelea kushuka.
 
Mie nimefurahi sana kusikia kauli ya watumishi wote mwezi huu watacheka na mimi nikacheka kwa tabasamu la kujificha. Ngoja nisubiri mwisho wa mwezi sio mbali bado siku 17 tu
 
Fungulieni magazeti acheni porojo, fungieni mwandishi na sio mnaadhibu jamii nzima ya wafanya kazi wa kampuni husika na wasomaji wao, kuhusu hela ni nani alisema tunataka mgawo? Tatizo ni hofu tu miongoni mwa Watanzania, Mh muda wote yeye hasira na ukali, miaka miwili hata kahotuba ka matumaini na faraja hakuna,,,!!!!!!!!! KUKOSEKANA PESA MTAANI NI KWELI KWA SABABU NYIE MNAKUSANYA HELA YOTE HAZINA NA CENTRAL BANK, JE ITARUDI VIPI KWENYE CIRCLE MZEE???? KUFANYA KAZI NA NJAA NI KUJIDANGANYA.
 

Zitto Kabwe na wenzake hawataki kabisa kuona Raisi magufuli akifanikiwa (kiuchumi na kisiasa)

Wakisikia hii ya makusanyo kufikia tilioni 14 wanaweza hata wakalipua Hazina na BOT kuendeleza kumkomesha JPM

 
Acha hizo Mbona ufisadi uliofanyika kule arumeru dhidi ya DC kwa kuwarubuni madiwani wa chadema kwa fedha haramu matokeo yake wakati jambo hilo lipo PCB cha ajabu kapongezwa kwa kupandishwa cheo na kuwa mkuu wa mkoa wa manyara.hapo utasema rushwa inakomeshwa kama sio comedi ninini?
 
Wamefanikiwa kuigeuza Chato kuwa sawa na Geneva ingawa Geneva traffic lights ni kwa magari na si ng'ombe na punda.

Jana jiwe la msingi la Chato International Airpor likiwekwa rasmi, hata kama hakuna resources za kutosha kupata idadi ya wasafiri watakaorudisha gharama za ujenzi.

Mpinzani aliye kuwa na sauti kubwa ya kuikemea serikali ni mgonjwa na bado amelazwa hospitali

MNASTAHILI PONGEZI
 
Naona Abbas ameamua kuanza kampeni za udiwani mapema. Hiyo janja ya kizamani sana. Nyie mlioipigia kura ccm 2015 mungu anawaona
 
tumetokomeza rushwa
tumejenga bomba la mafuta
tumetokomeza wafanyakazi hewa
tumejenga reli ya umeme
tumeimarisha ukabila
tumeua upinzani
tunaendelea kuua uchumi taratibu
tumezibaka mahakama na bunge
tupo chato tunapumzika
.......
.
.
.
kuna lingine kaongea?????
Kama hawatasema haya ni waongo.
 


Dkt. Hassan Abbasi anaongea;

View attachment 624637

"Katika miaka miwili hii tumefarijika kuona watanzania wengi wanaunga mkono mageuzi makubwa nchini"

"Tunajivunia kuongezeka kwa ari na nidhamu kwa watumishi wa umma"

"Mpaka sasa tumebaini watumishi hewa elfu ishirini ambao kama wangelipwa ingegharimu Tzs bil. 236"

"Eneo lingine ni kubaini watumishi wenye vyeti feki 12,000 ambapo kama wangelipwa ingegharimu TZS Bil. 142.9"

"Kwa mwezi Serikali inatumia Tzs Bil. 23 kwa mwezi kwa ajili ya Elimu Bure"

"Serikali ilianzisha Mahakama ya Mafisadi ambapo mpaka sasa kesi 3 za uhujumu uchumi zimeanza kusikilizwa"

"Miaka ya 2014-2015 safari za nje za watumishi na viongozi wa serikali ziligharimu sh. 216 bilioni"

"Miaka miwili ya serikali ya awamu ya 5 safari za nje zimegharimu kiasi kisichozidi sh. 25 bilioni"

"Makusanyo ya mwaka yameongezeka kutoka trilioni 9.9 mwaka 2015 hadi trilioni 14 mwaka 2017"

"Uzalishaji wa madini ya Tanzanite na Almasi umeongezeka kutoka karati 15,000 - 18,000 hadi karati 28,000 - 32,000"

"Kama nchi, safari ya kuelekea kujitegemea tumeshaianza kwa njia nyingi"

"Kwa mwaka 2015, Bajeti ya dawa na vifaa tiba ilikua TZS Bil. 30, kwa miaka 2 bajeti imefikia TZS Bil. 261"

"Katika kipindi cha uongozi wa Rais Magufuli tumefanikiwa kufufua viwanda 17 kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina"

"Tupo kwenye awamu ya mageuzi, vyombo vya habari vinapaswa kuungana na matamanio ya wananchi"

"Mkoani Arusha kuna mradi wa maji wa TZS Bil. 476 unaendelea na mingine ya TZS Tril.1.2 inaendelea katika miji 17"

"Kuanzia mwisho wa mwezi huu watumishi wataanza kuongezewa mishahara na kupandisha madaraja, na kulipwa stahiki zao"

"Katika sekta ya kilimo tumeondoa Tozo na Kodi nyingi zilizokuwa kero kwa watanzania"

"Tumefanya udhibiti katika bei za mazao na juzi nimesikia Mtwara bei ya korosho imefika Tsh. 4100/= kwa kilo"

"Wafanyakazi kwa sasa wanauhakika na misharaha ikifika tarehe 25 ya mwezi hela imeshaingia"

"Kipande cha reli ya kisasa kinachojengwa kutoka Dar hadi Dom kitagharimu TZS Tril 7.1 ikiwa ni fedha za ndani"

"Mradi wa Kinyerezi 2 wa megawati 240 uko katika 84% kukamilika, mtambo wa 1 wa megawati 30 utawashwa Desemba,2017

Hapa Kazi Tu.
 
Kuhusu nidhamu ya watumishi, ni utafiti gani umefanyika kuprove kuwa nidhamu ya watumishi imeongezeka?
 
Toeni na tathimini ya madhara yaliyojitokeza baada ya kuachishwa hao wa vyeti feki. Pia nini kimeongezeka au kupungua zaidi ya fedha kwa kuzuia safari za nje.

Je huko nyuma kulikuwa na waganyakazi wa serikali waliokuwa hawalipwi mishahara kwa wakati?
 
Back
Top Bottom