Bahati furaha
JF-Expert Member
- Jul 11, 2012
- 3,077
- 1,438
Tunalazimika tena leo kuitahadharisha Serikali kuhusu athari zinazotokana na utamaduni wake wa kutolipa madeni.
Miezi minne tu iliyopita tuliitahadharisha kuhusu jambo hilo na kusema dunia sasa inajua kwamba Serikali yetu imelimbikiza madeni kiasi cha kudaiwa kila kona, huku ikielekeza fedha nyingi katika matumizi yasiyo ya lazima.
Tulionyesha wasiwasi kuhusu kasi yake ya kukopa na kusema Deni la Taifa lipatalo zaidi ya Sh30 trilioni linazidi kupaa na sio muda mrefu nchi yetu itakuwa haikopesheki iwapo Serikali haitabadili mwelekeo. Itakumbukwa kuwa, Machi mwaka jana deni hilo lilikuwa Sh23.6 trilioni.
Inasikitisha kuona kwamba hadhari yetu hiyo bado haijachukuliwa kwa uzito stahiki na Serikali, kwani imeendeleza dhana kwamba bado nchi inakopesheka na kwamba Deni la Taifa bado ni endelevu.
Dhana hiyo tunayoweza kuiita potofu imeongezwa nguvu na kauli iliyotolewa hivi karibuni na Mkurugenzi wa Shirika la Fedha Duniani (IMF), Kanda ya Afrika, Antoinette Sayeh kwamba Deni la Taifa halijavuka kiwango na kwamba Tanzania inaweza kuendelea kukopa iwapo tu fedha hizo zitaelekezwa kwenye ujenzi wa miundombinu na miradi ya maendeleo.
Wakati mkurugenzi huyo wa IMF akitoa kauli hiyo, zimekuja taarifa kwamba madeni sugu ya Serikali yanatishia uhai wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii hapa nchini, huku Mamlaka ya Usimamizi ya Mifuko hiyo (SSRA), ikitoa angalizo kwa Serikali kwamba deni lake la Sh8.43 trilioni kwa mifuko hiyo litaifilisi mifuko hiyo siyo tu kiasi cha kushindwa kujiendesha, bali pia kuikwamisha na kushindwa kuwalipa mafao wanachama wake.
Deni hilo, ambalo baadhi ya wataalamu wa uchumi wanasema haliwezi kulipika kirahisi, linatokana na Serikali na taasisi zake kukopa kwenye mifuko hiyo na kutopeleka michango ya wanachama.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), juzi ililazimika kuwakutanisha wakurugenzi wa mifuko hiyo, Wizara ya Fedha, Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Gavana wa Benki Kuu (BoT) na SSRA kwa lengo la kutafuta suluhisho la tatizo hilo.
Pande zote zilikubaliana kwamba suluhisho pekee ni Serikali kulipa madeni hayo, ambayo ni takribani nusu ya bajeti ya Serikali kwa mwaka, vinginevyo mifuko hiyo itafilisika na kusababisha madhara makubwa kiuchumi.
Tunaambiwa kwamba katika mazungumzo hayo, Serikali ilithibitisha kulitambua deni hilo, lakini ilishindwa kueleza lini italilipa wala utaratibu utakaotumika kulilipa. Hata hivyo, sisi hatuna ugomvi kuhusu Serikali kukopa, isipokuwa kinachopaswa kuangaliwa kwanza ni Serikali inakopa fedha kufanya shughuli gani.
Ndiyo maana tulipaza sauti kupinga Bajeti ya mwaka wa fedha uliopita, ambapo ilitenga zaidi ya asilimia 60 ya bajeti kwa matumizi ya kawaida, huku miradi na shughuli za maendeleo zikipewa chini ya asilimia 40.
Katika Bajeti ya mwaka huu wa fedha, miradi na shughuli za maendeleo zimetengewa Sh6,445 trilioni sawa na asilimia 32.4 ya bajeti nzima ya Sh19.9 trilioni, huku matumizi ya kawaida yakitengewa Sh13.408 trilioni sawa na asilimia 67.4 ya bajeti hiyo.
Hapo ndipo lilipo tatizo. Serikali inakopa fedha kwa matumizi yasiyo na tija kwa nchi. Kwa utamaduni huu wa kukopa na kutolipa madeni, nchi yetu huko tuendako haiwezi kuepuka kufilisi mifuko hiyo na hivyo kuathiri ustawi wa wafanyakazi ambao ni wanachama na kugeuza wastaafu kuwa ombaomba.
Chanzo: Gazeti Mwananchi