Serikali mbili

Serikali mbili

JEMA JEMA

Member
Joined
Apr 3, 2014
Posts
19
Reaction score
4
1. Hati ya makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 ndiyo msingi wa kuwa na muundo wa Serikali mbili ambapo Zanzibar ilikubali kuhamishia sehemu ya mamlaka yake hasa yanayohusu masuala ya muungano kwenye serikali ya muungano na Tanganyika ilikubali kuhamishia mamalaka yake yote kwenye serikali ya jamuhuri muungano, hivyo kuifufua serikali ya Tanganyika ni kuiua Tanzania na kuvunja muungano.

2. Muundo wa serikali mbili unaainisha vizuri vyombo vinavyotekeleza mamlaka katika jamuhuri ya Muungano. Katika sura ya sita ibara ya 60(1) muundo huu unapendekeza kuwa jamuhuri ya muungano wa Tanzania itakuwa na muundo wa serikali mbili ambazo ni:-

Serikali ya jamuhuri ya muungano, na

Serikali ya mapinduzi Zanzibar

60 (2) shughuli zote za mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma , na
Vyombo vyenye mamlaka ya utoaji haki
60(3) vyombo vyenye mamlaka ya utendaji vitakuwa ni;-
Serikali ya jamuhuri ya muungano, na
Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.

60(4) vyombo vyenye mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma vitakuwa ni;
Bunge la jamuhuri ya muungano, na
Baraza la wawakilishi.

60(5) vyombo vyenye mamlaka ya utoaji haki vitakuwa ni;
Mahakama ya jamuhuri ya muungano, na
Mahakama ya Zanzibar.
(6) Kila chombo kilichotajwa kwenye ibara ndogo ya (3),(4), (5) ya ibara hii, kitaundwa na kutekeleza majukumu yake kwa kufuata masharti ya katiba hii na katiba ya Zanzibar kadri itakavyokuwa na kwa kuzingatia sheria zitakazotungwa na bunge la jamuhuri ya muungano au baraza la wawakilishi kwa madhumuni hayo.

Muundo huu wa serikali mbili unatoa ufufanuzi moja kwa moja kuwa ni chombo gani kitahusika katika kutunga sheria, kusimamia sheria na haki katika serikali hizi mbli, Tofauti na ule muundo wa serikali tatu ambao umependekezwa katika tume ya warioba bila Kuainisha kwa ufasaha utekelezwaji wa majukumu katika serikali hizo tatu.

Katika rasimu sura ya sita ibara ya 60 (1) inaonesha muundo wa muungano kama ifuatavyo
Tanzania itakuwa na muundo wa shirikisho lenye serikali tatu ambazo ni;-
Serikali ya jamuhuri ya muungano

Serikali ya mapinduzi zanzibar, na
Serikali ya Tanganyika.

(2) Shughuli za jamuhuri ya muungano zitatekelezwa na kusimamiwa na

(a) Serikali ya jamuhuri ya muungano

(b) bunge la jamuhuri ya muungano, na

(c) Mahakama ya jamuhuri ya muungano.

(3) Muundo na madaraka na mambo mengine ya kiutendaji yuhusuyo serikali ya Tanganyika na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar, yataainishwa katika katiba na nchi washirika.

Muundo huu unapingwa kwasababu moja kuu kuwa Tanganyika haina katiba ila kuna katiba ya jamuhuri ya muungano na kuamua kuunda katiba ya Tanganyika ni kuvunja muungano maana kwa mujibu wa hati ya makubaliano ya muungano ya mwaka 1964, Tanganyika iliamua kuhamishia mamalaka yake yote kwenye serikali ya jamuhuri muungano, hivyo kuunda katiba Tanganyika ni kuifufua serikali ya Tanganyika na kuiua Tanzania hivyo kuvunja muungano.

3. Tukiwa na serikali tatu, tutakuwa na watanganyika, wazanzibari na hivyo hakutokuwa na watanzania wenye uzalendo na Taifa lao ila titaishi kwa kunyoosheana vidole na kusema huyu ni mtanganyika, mara huyu ni mzanzibari mambo ambayo hatukuwahi kuwa nayo kwa muda wa miaka hamsini tokea kuungana. Hivyo mfumo wa serikali mbili unajenga uzalendo wa kitanzania zaidi kuliko utanganyika na uzanzibari, na kuondoa utabaka, ukabila na udini ndani ya jamuhuri.

4. Mfumo wa serikali mbili unapunguza gharama kubwa za uendeshaji ikilinganishawa na ule wa serikali tatu uliopendekezwa. Ukizangatia katika rasimu serikali ya muungano haina vyanzo vya mapato. Ibara ya 231 imeeleza vyanzo vya serikali ya jamuhuri ya muungano vitakuwa ni:-
Ushuru wa bidhaa

Mapato yasiyikuwa na kodi yatokanayo na taasisi za muungano.

Mchango kutoka kwa washirika.

Mkopo toka ndani na nje ya nchi.

Huu ni mzigo kwa hiserikali mbili kwani kwanza nchi hii bado ni masikini, kuibebesha mzigo mwingine ni kuionea,
Pia tume imependekeza hivyo vyanzo vya mapato lakini imeshndwa kutoa ni njia gani itatumika kuwabana nchi washirika kutoa mchango ya kueendesha serikali ya tatu.
Lakini pia imeshindwa kujua kuwa ili ukope lazima uwe na rasilimali, na serikali hii ya tatu hoitokuwa na rasilimali sasa itakopesha vipi toka nje?


5. Muundo huu wa serikali mbili unatoa fursa za kisiasa, kiuchumi, kijamii na kisiasa ambapo watu wote kutoka pande zote za muungano watakuwa na fursa sawa za kutumia fursa zilizpo katika jamuhuri.

Mfano fursa za kijamii, wanamuungano watakuwa nam fursa ya kupata huduma za matibabu popote alipo bila usumbufu au kuulizwa utaifa wake, lakini pia kupata elimu kama ilivyo sasa hususani katika chuo kikuu cha Dodoma kuna wanafunzi wengi kutoka Zanzibar wanasoma katika chuo kikuu cha ddodoma kilichopo Dodoma- Tanzania.

Kiuchumi, mfumo huu unatoa fursa kwa wanamuungano kwenda sehemu zote za muungano na kufanya biashara yeyote halali bila kuvunja sheria au utaratibu uliowekwa, kama ilivyoasasa wazanzibari wengi wapo maeneo ya kariakoo Dar es salaamu wakifanya biashara zao mbalimbali bila ya kujali utaifa wao, hivyo hivyo kwa watanzania bara wanaenda Zanzibar kufanya biashara za simu, magari na mengine mengi bila ya kujali utaifa ila tukileta suala la serikali tatu ninahakika utaifa utatutafuna.

Kisiasa, mfumo huu unaruhusu vijana kupata fursa za kisiasa katika pande zote za muungano kama ilivyo sasa ambapo vijana kwa wazee wamekuwa wakipata nafasi za kisiasa katika pande zote za muungano. Mfano mwenyekiti wa uvccm taifa Mh. Sadifa na katibu wake ni sixtus Mapunda kutoka bara, hivyo ni wazi kuwa fursa za kisiasa katika pande zote zipo.
Hivyo mfumo wa serikali tatu unapunguzia Zanzibar na wazanzibar fursa walizonazosasa kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa Tanzania bara na fursa wanazozipata wananchi wa bara kwa upande wa Zanzibar.
Serikali tatu ni janga la kitaifa niwaombe watanzania tusikalibishe adui mwingne, maadaui tulionao kama njaa, maradhi na umaskini wanatosha tuungane mkono katika kuangalia jinsi ya kudumisha serikali mbili ili kuondikana na maadui hao na sio kuongeza adui.

Niwaombe tujumuike pamoja kuidumisha Tanzania.
 
Dawa hapa ni kura ya maoni wananchi waamue ni Serikali mbili au tatu... then Bunge ndo liendelee!!!!
 
Back
Top Bottom