Serikali: Marufuku kutibiwa nje maradhi yanayotibika katika hospitali za nyumbani

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
Serikali imebana fursa ya safari za matibabu nje ya nchi kwa kuondoa urahisi uliokuwepo kwa maafisa wake na wabunge kupata kibali cha kwenda kutibiwa ughaibuni na hasa India.

Kwa sasa ni marufuku kwenda kutibiwa nje kwa maradhi ambayo yanaponyeka katika hospitali nchini.

Kwa sasa ili kwenda kutibiwa nje ya nchi, ni lazima mfanyakazi awe na matatizo ya kiafya ambayo matibabu yake hayapatikani nchini lakini pia safari yake italazimika kuidhinishwa na jopo la madaktari bingwa wa hospitali ya Muhimbili.

Awali watumishi wa Umma wakiwepo wabunge walikuwa wanapata idhini/ushauri wa kwenda kutibiwa nje ya nchi kutoka kwa daktari mmoja tu huku serikali ikibeba gharama kubwa za matibabu, nauli na posho kwa wale waliokuwa wakisafiri kwenda kupata matibabu huku wengine wakiambatana na waangalizi.

12507499_1020620594669065_6637494011819071735_n.jpg
 
Last edited by a moderator:
Nilimsikia juzi Spika wa Bunge la Tanzania, Ndugai akidai eti alikwenda kuangaliwa afya yake India baada ya uchovu wa kampeni za Uchaguzi Mkuu.

Yaani uchovu wa kampeni unaenda kufanyia health check up India! This is fun to say the least!

Siyo ajabu hata ndugu zake hawana pesa za kwenda kununua dawa kwenye hospitali nchini lakini yeye anasafiri kwenda India kufanya health check up!

Nilijiuliza hivi zingekuwa ni pesa zake angeenda India kwenda kuangaliwa kiwango cha uchovu wake?

Kweli Tanzania ilikuwa ni shamba la bibi!
 
One man government, if all government decisions are made by the president it is clear that we are heading somewhere that many of us have not anticipated
I see my beloved country Tanzania in a paralyzed state in the near future.
 
Serikali imebana fursa ya safari za matibabu nje ya nchi kwa kuondoa urahisi uliokuwepo kwa maafisa wake na wabunge kupata kibali cha kwenda kutibiwa ughaibuni na hasa India.

Kwa sasa ni marufuku kwenda kutibiwa nje kwa maradhi ambayo yanaponyeka katika hospitali nchini.

Kwa sasa ili kwenda kutibiwa nje ya nchi, ni lazima mfanyakazi awe na matatizo ya kiafya ambayo matibabu yake hayapatikani nchini lakini pia safari yake italazimika kuidhinishwa na jopo la madaktari bingwa wa hospitali ya Muhimbili.

Awali watumishi wa Umma wakiwepo wabunge walikuwa wanapata idhini/ushauri wa kwenda kutibiwa nje ya nchi kutoka kwa daktari mmoja tu huku serikali ikibeba gharama kubwa za matibabu, nauli na posho kwa wale waliokuwa wakisafiri kwenda kupata matibabu huku wengine wakiambatana na waangalizi.

12507499_1020620594669065_6637494011819071735_n.jpg
 
Spika anadai alienda india kufanya medical check up baada ya uchovu wa kampeni.
Unalizungumziaje hili?
Jamani mtu si afadhali amesema ukweli! sasa mlitaka afiche asemeje wakati kundi zima ndiyo walikea wakifanya! mnamlaumu mtu kuwatonya ufisadi ambao amekuwa akiufanya!!!
 
Amefanya vizuri. Mama T yuko India mwezi wa sita sasa. Gharama hizo angetibiwa hapa. Juzi tumemzika Mama D alienda kutibiwa India bahati mbaya akatwaliwa, ilikuwa gharama sana kurudisha mwili huku.

Watendaji wakuu wote wanaenda kucheck afya india kama vile wataishi milele.

Dr Magufuli keep it.
 
and without exaggerating the facts we are heading back to dictatorship ...zidumu fikira za Mtukufu Rais....iam afraid so
Kikwete alikuwa anacheka full time na kutokuwa na dictorship mkasema raisi gani anacheka cheka yuko soft hivyo? Kaja Magufuli hacheki na mtu anaangalia hapa kazi tu mnaanza kubwata.Tatizo la watu kutibiwa nje wakisharudi si mitusi watakayotukana serikali hiyo angalia hospitali za Tanzania hovyo na kura hatuwapi.Hiyo ndio shukrani yao baada ya kutoka kutibiwa ulaya na india kwa gharama za serikali.Utasikia serikali haijafanya chochote!! Watu kama Sumaye,Lowasa wakati wakikohoa tu mbio wanakimbizwa ujerumani,marekani nk kutibiwa kwa gharama za serikali

Pesa zilizokuwa zikipeleka watu kutibiwa india na ulaya zielekezwe hospitali za serikali na kuboresha maslahi ya madaktari na wauguzi.Tubanane hapa hapa.Kwanza wanaofaidi hiyo huduma ni asilimia ngapi ya watanzania hadi tushindwe kuwakatalia? Ukisema wao muhimu hata mkulima ni muhimu kwani anazalisha chakula tunachokula asingezalishe tungekufa.Kama ni kujali umuhimu wa mtu mkulima akiugua alitakiwa kuwa wa kwanza kupelekwa India na Ulaya kutibiwa apone haraka aje kutuzalishia chakula.

Naunga mkono hoja ya Magufuli kupiga marufuku watu kutibiwa nje.Magufuli kaza buti kanyaga moto songa mbele wakuite dictator au nani watajijua wengine tunapenda hiyo staili yako ya uongozi sana tu.
 
Job
Nilimsikia juzi Spika wa Bunge la Tanzania, Ndugai akidai eti alikwenda kuangaliwa afya yake India baada ya uchovu wa kampeni za Uchaguzi Mkuu.

Yaani uchovu wa kampeni unaenda kufanyia health check up India! This is fun to say the least!

Siyo ajabu hata ndugu zake hawana pesa za kwenda kununua dawa kwenye hospitali nchini lakini yeye anasafiri kwenda India kufanya health check up!

Nilijiuliza hivi zingekuwa ni pesa zake angeenda India kwenda kuangaliwa kiwango cha uchovu wake?

Kweli Tanzania ilikuwa ni shamba la bibi!
Job Ndugai alipigana masumbwi mpaka akachoka ndio alienda kufanya medical check.
 
na ingefaa matibabu chini ya gharama ya umma yafanyike katika hospital za umma na sio private na waanzie ngazi za chini kama dispensary huko ndio wapewe refferal kadri tatizo lilivyo kuelekea ngazi za juu na sio self refferal to MNH bila hata kupitia hospital ya wilaya or refferal hospital za kanda/mikoa
 
Kuna sheria yoyote iliyowekwa ili kufanya hili jambo kutojirudia tena? Maana naona kuweka jipo la madaktari tu haitoshi maana akiingia Rais mwingine asiyefuatilia sheria sana kama tulikotoka basi hata hayo majopo hayatazingatiwa sana au wataambiwa tu andikeni nikatibiwe nje.

Tatizo ni mamlaka moja kuingilia mamlaka nyingine na kuweza kupewa vitisho vya kufungwa nk,hivyo visipodhibitiwa kwa sheria ninaona hatari ya kujirudia kwa kasi miaka ijayo...kuwe na mipaka ya kuingilia mambo ya kitaalamu kwa hawa wanasiasa wetu,hilo tu basi kwa mani yangu.
 
na ingefaa matibabu chini ya gharama ya umma yafanyike katika hospital za umma na sio private

Mkuu naunga mkono hoja.

Kuna jipu lingine liko kwa wafanyakazi wa serikali na mashirika ya umma kutibiwa hospitali binafsi.Pesa nyingi na ufisadi mwingi hufanyika huko.Kuna wizi mkubwa wa ukwapuaji pesa kupitia hospitali binafsi.Hospitali za serikali zilianzishwa za nini kama wafanyakazi wa serikali na mashirika ya umma na wabunge hawatibiwi huko wanakimbilia za binafsi?
Pesa wanazolipa hospitali binafsi zipelekwe hospitali za serikali ziboreshe huduma huko.
Wafanyakazi wote wa serikali na mashirika ya umma wote watibiwe hospitali za serikali tu wakitaka kutibiwa hospitali binafsi watumie gharama zao binafsi toka mifukoni mwao sio mifuko ya serikali au shirika.
 
Back
Top Bottom