Serikali: Majeruhi atakayefikishwa hospitali atibiwe bila PF3 ili kuokoa maisha yake

falcon mombasa

JF-Expert Member
Mar 5, 2015
9,159
9,241
Serikali kupitia jeshi la polisi sasa imepitisha azimio kwa majeruhi wote kutibiwa bila pf3,ambapo hapo kabla majeruhi walitakiwa kuwa na form ya pf3 ili waweze kupata matibabu, lakini kupitia utaratibu huu mpya majeruhi wataanza kupata tiba huku pf3 ikifuatiliwa.
 
Habari nzuri sana hii, watu wengi walipoteza maisha kwa ajili kuchelewa hospital wakiwa wanafuatilia pf3
 
huenda ikawa mkomboz kwa wengi
 
Attachments

  • IMG-20170518-WA0069.jpg
    IMG-20170518-WA0069.jpg
    32.7 KB · Views: 35
Binafsi nawapa big up polisi wa arusha pale makao makuu,siku tulokuwa tukihitaji huduma ya pf 3 hatukupata usumbufu walitupatia haraka kimbembe tukaenda kukutana nacho hospital umefika na mgonjwa pale kabla wampokee mgonjwa hakuna waaguzi kuna walinzi wamesimama tu wanakuambia kitanda cha kumbebea mgonjwa ukifate mwenyewe mkikokote wenyewe umuingize kwa daktari kwa kwel usiku ule sikuona umuhimu wa watu kulipwa night allowance kupitia kodi zetu
 
Hili suala zuri ila Polisi waweke muda wkati majeruhi akiendelea na matibabu kabla ya kuondolewa chumba cha matibabu ndugu na jamaa waliomleta wahahakikishe wanaleta hiyo PF 3 maana ma DR. wasije wakatibu jambazi sugu linalotafutwa halafu baada ya matibau likatokomea kusikojulikana. Tukumbuke kutibu majeruhi bila PF 3 naunga mkona maana ajali pia zinatumaliza wengi hasa pale suala la PF 3 linapozuia matibabu.
 
Safi sana safi sana. Hili limekuwa linazungumzwa weeee. Asante Mh. Magufuli kwa kuchuka hatua!
 
Hizi ni habari njema sana. Majeruhi wengi sana walipoteza maisha kutokana na huo utaratibu wa kupata PF3 kabla ya matibatu.

Mimi nilikuwa nashauri kila hospital iwe na dawati la polisi kwa ajili ya kutoa hiyo huduma ya PF3. Hii itawasaidia wao katika swala zima la upelelezi (tukio/ajali inapohitaji upelelezi baadae) maana kigezo kikubwa cha PF3 ilikuwa ni kulinda/kutopoteza ushahidi.
 
tuwaombee

Back
Top Bottom