Serikali legelege....... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali legelege.......

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Elizabeth Dominic, Jul 12, 2011.

 1. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #1
  Jul 12, 2011
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Kafulila kazua jambo SERIKALI LEGE LEGE haiwezi kukusanya kodi. Duh Bunge shurti hakuna mwelekeo lakini message delivered.
   
 2. Islam005

  Islam005 JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2011
  Joined: Nov 1, 2008
  Messages: 2,539
  Likes Received: 958
  Trophy Points: 280
  halafu mwenyekiti anasema eti afute kauli yake,, mimi nasema "SERIKALI WAPUMBAVU" na sifuti kauli yangu maisha.tumechoshwa na hii tabia ya kulindana.
   
 3. Mosachaoghoko

  Mosachaoghoko Senior Member

  #3
  Jul 12, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 137
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mi naongezea juu SERIKALI FISADI TANGU LINI IKUSANYE KODI KUHUDUMIA WANANCHI WAKE na siondoi kauli
   
 4. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  kama lugha ya kuudhi imetolewa bungeni leo, basi aliyeitoa ni mzee Sitta.
   
 5. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #5
  Jul 12, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  30% ya Mshahara wangu unaenda kwenye kodi!
  Bado nikinunua vitu kwa ajili ya mahitaji yangu nakatwa 18% VAT. Kwa mahesabu ya haraka haraka 48% ya Income yangu ni KODI
  Sasa hapo unaweza kuilaumu Serikali?
   
 6. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #6
  Jul 12, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Makubwa!
   
 7. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #7
  Jul 12, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  vyanzo vya kodi viko vingi sana na si mishahara tu. jiulize nchii hii inawafanyakazi wangapi? km wakati ule wa hadithi za mbayuwayu tuliambiwa kuna wafanyakazi laki tatu serikalini ukichanganya na sekta binafsi waweza kuta wanafika laki tano ht milioni bd. kwa hiyo nchi yenye watu milioni arobaini wanaolipa kodi ht milioni hawafiki. wafanyabishara wakubwa kila siku wanapewa tax holidays wanaolipa ni wachache mnoo. hii serikali si legelege tu ni serikali TEPETEVU yaani wapo wapo tuuu nadhani wengi wao waligombea ubunge ili waongeze idadi ya nyumba ndogo walizonazo na si kuwalete watu maendeleo.
   
 8. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #8
  Jul 12, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Neno linakuwa uongo au kashfa pale tu linapothibitika kua ni uongo,...kwa hili la serikali kua legelege na kua wapumbafu ni ukweli ulio dhahiri hivyo hakuna haja ya kukanusha na kufuta kauli.....serikali ni wanafiki
   
 9. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #9
  Jul 12, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  unaandikaga upepo ww
   
 10. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #10
  Jul 12, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Serikali ya kizabazabina - Sifuti KAULI yangu!
   
 11. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #11
  Jul 12, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Serikali yenye viongozi wajinga,majizi,waongo etc haitufai kabisa
   
 12. kanta

  kanta JF-Expert Member

  #12
  Jul 12, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Serikali ya '.COM' Usanii mtupu na ujinga.
   
 13. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #13
  Jul 12, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Unapinga na kutetea nini sasa?
   
 14. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #14
  Jul 12, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Kasemaje??
   
 15. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #15
  Jul 12, 2011
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  tazama hizi picha mbili, ni Za Mawaziri makini wakifuatilia Mijadala miwili tofauti katika mazingira tofauti. wataachaje kuunda serikali mbovu, chovu, legelege na isiyojali maslahi ya wengi...hili ni genge la mawaziri posho na wasio jali maisha ya maskini na wanaoteseka..

  [​IMG]

  [​IMG]
   
 16. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #16
  Jul 12, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Picha zinaongea mara 10 kuliko maneno!
   
 17. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #17
  Jul 12, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  serikari ni 'ndevi', ya walevi wa kila aina.
  Sifuti kauli, na wakija majimboni tutawaonyesha hatufurahishwi na unafiki wa sita na wenzake.
   
 18. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #18
  Jul 12, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  Nilimuheshimu sana sitta lakini kauli yake ya leo ni ya kinafiki na yenye dharau mno.shame on u 6.
   
 19. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #19
  Jul 13, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD] WABUNGE WATAHARUKI, WASEMA BILA MPANGO

  MBUNGE wa Kigoma Kusini, Davidi Kafulila (NCCR-Mageuzi), amezua balaa bungeni baada ya kutoa kauli iliyozua mjadala mkali bungeni, huku wabunge wa CCM wakiomba mwongozo wa mwenyekiti na kumtaka afute kauli.

  Akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa mwaka 2011/12 jana, Kafulila alisema Serikali imekuwa legelege na ndiyo maana imeshindwa kukusanya kodi za kutosha na kutoa huduma duni za afya nchini.Kauli hiyo ilizua mtafauruku huku wabunge wa CCM wakimtaka afute kauli lakini alikataa.

  Kufuatia mtafaruku huo ulitokana na wabunge kuanza kuzungumza bila mpangilio, Mwenyekiti wa Kikao cha Bunge, Jenista Mhagama, kuhairisha kikao dakika saba kabla ya wakati ili kupunguza mvutano uliokuwepo.Wakati Mhagama anatangaza kuhairisha kikao sehemu kubwa ya wabunge wa CCM na upinzani walikuwa wamesimama wakiwa na shauku ya kuomba mwongozo wa mwenyekiti kuhusiana hoja hiyo.

  Mvurugano
  Kabla ya kuahirisha kikao, Mhagama alitoa fursa ya mbunge au waziri kuchangia, lakini kulikuwa na sauti zilizokuwa zinasikika kupitia vipaza sauti za wabunge waliokuwa wamewasha vinasa sauti kinyume na taratibu za Bunge.Maneno ya wabunge yaliyokuwa yanasikakika ni kama vile: "…cha ubishi…", "…so what…," "…hiyo siyo taarafa…," "…hujui…" "Nani hana heshima nani, hana heshima…"

  Hata Kaimu Kiongozi Mkuu wa Shughuli za Serikali Bungeni, Samwel Sitta aliposimama kujaribu kuokoa jahazi, kauli yake ilionekana kama kamwaga petroli kwenye moto, kwani wabunge waliendelea kubishana bila utaratibu. Hata Mhagama aliposimama ili kutoa ufafanuzi, alivurugugwa na sauti za wabunge zilizokuwa zinampinga kupitia kwenye vipaza sauti.

  Baada ya kuona hivyo alisema: "Hata kama mnazungumza huko, kauli ninayoitoa mimi ndiyo yenye nguvu, kwa kuwa ni Spika wa kikao hiki."Pamoja na Mhagama kusisitiza kuwa anaposimama kuzungumza, au mtu mwingine anapopewa ruhusa na Spika, au Mwenyekiti kuzungumza, mtu mwingine hairuhusiwi kuwasha kinasa sauti na kuzungumza, wabunge hawakuvizima.

  Chazo cha mvutano
  Kuchafuka kwa hali ya hewa kulianza hivi; Kafulila alipewa fursa ya kuchangia hotuba ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, alisema fedha zilizoombwa na Wizara ni kidogo sana kwa sababu ni sawa na asilimia 10 ya mapato yote ya Serikali, kiwango ambacho ni kinyume na maazimio ya Abuja ambayo Tanzania imesaini.

  Alisema maazimio hayo yanaelekeza nchi kutumia asilimia 15 kwa ajili ya huduma za afya."Serikali imekosa dhamira ya kutekeleza mipango mizuri ambayo itasaidia Huduma za Afya," alilalamika Kafulila na kuongeza kuwa wanaoumia ni walalahoi.Alipandisha hasira za wabunge wengi aliposema Serikali imekuwa haiwaonei huruma Watanzania wengi wanaoteseka kwa kukosa matibabu, kwa vile wao wana mishahara mikubwa ambayo inawawezesha kutibiwa mahali popote wanapotaka.

  Alitoa mfano kuwa Sitta na familia yake kuwa hawana tatizo kuhusu tiba kwa sababu wanaweza kutibiwa popote.Alisistiza kuwa uwezo wa Tanzania kuweza kuiwezesha sekta ya afya nchini na kutoa huduma bora ipo, lakini Serikali imekuwa ikizembea hata katika suala la ukusanyaji wa kodi.

  Alijenga hoja zake huku akinukuu jarida linalochanganua mambo ya kiuchumi duniani la Economist, kitabu cha taarifa za Serikali na kauli alizowahi kuzitoa Baba waTaifa, Mwalimu Julius Nyerere.Alisema kwamba, Tanzania inatimiza miaka 50 ya Uhuru huku wakishindwa kuboresha huduma za afya, lakini akasema hamlaumu Waziri wa Afya kwa sababu suala hilo halipo ndani ya uwezo wake.

  Akasema takwimu zinaonyesha kuwa hapa nchini hakuna uwiano mzuri wa kitaalamu kati ya idadi ya daktari na Watanzania.Alisema zamani watoto wa wabunge na wakurugenzi walikuwa wakitibiwa kwenye hospitali za Serikali, lakini sasa wanatibiwa kwenye hospitali za kisasa za sekta ya binafsi ambako dawa zipo kwa wingi.

  Utetezi wa mawaziri
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, alipopewa nafasi alisema maelezo ya Kafulila siyo ya kweli kwa sababu familia yake wakati wote inatibiwa katika hospitali za Serikali.Wakati anazungumza hayo, zilisikika sauti kwenye vipaza sauti zikisema: "Hiyo siyo taarifa! Hujui! Wabunge wote wanaweza."

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Dk Mary Nagu naye alisimama na kutetea hoja ya Maige akisema kuwa siku zote amekuwa akijitahidi kuboresha huduma za hospitali ya Serikali iliyopo jimboni kwake.

  Mhagama
  Mhagama alimtaka Kafulila aendelee kuchangia, lakini awe mwangalifu na kauli zake ambazo zinaweza kusababisha utata.Kafulila alisimama na kutetea kauli yake akisema: "Mimi nasema mbunge ana uwezo wa kutibiwa sehemu yoyote, iwe nchini au nje ya nchi. Ndiyo maana hamuwekezi vizuri kwenye sekta ya afya."

  Dk Kigwangalla
  Baada ya kumaliza, Dk Hamis Kingwangalla (Nzega-CCM) alisimama na kuomba mwongozo wa Spika akisema Kafulila ametoa lugha ya maudhi dhidi yake, chama chake cha CCM na Serikali yake aliposema kuwa, serikali legelege hushindwa kukusanya kodi.Kigwangalla alisema, siyo kweli kwa sababu takwimu zinaonyesha kuwa makusanyo ya kodi yamekuwa yakiongezeka kwa kadri muda unavyokwenda.

  Mhagama ilibidi amtake Kafulila ajibu hoja ikiwezekana aifute, lakini wakati huo kulikuwa na wabunge kadhaa waliokuwa wanaomba muongozo wa Mwenyekiti.Mhagama aliwanyamazisha akisema; "Huwezi kutoa muongozo juu ya muongozo mwingine. Subiri kwanza ajibu ndio uombe nafasi."

  Kafulila alijibu akisema hayupo tayari kufuta kauli yake kwa vile ukweli ni kwamba, mazingira halisi hapa nchini yanampa mbunge yeyote kutibiwa popote na hata ikiwezekana nje ya nchi.Alisema wabunge wengi hawatibiwi kwenye hospitali za Serikali ndiyo maana hawaoni umuhimu wa kutenga fedha za kutosha ili kuboresha huduma za afya.Kuhusu kauli kwamba, Serikali ni legelege na imeshindwa kukusanya kodi, alisema maneno hayo siyo yake, bali ni ya Baba wa Taifa.


  Mhagama alimpa nafasi Sitta kwa kuwa anakaimu nafasi ya Waziri Mkuu bungeni, lakini hoja yake ilimalizika kwa kuonyesha shauku ya wabunge wa upinzani kutaka kuomba muongozo wa spika.Sitta aliwataka wabunge wa CCM kutoendelea kubishana na wabunge wa kambi ya upinzani kwa sababu ya kutoa maneno ya kuudhi dhidi ya Serikali iliyopo madarakani ni wajibu wao.

  "Nawasihi wenzangu wa CCM wasihangaike kubishana kwa sababu kauli za kuundhi ni kazi yao. Ukishindana nao utapata shida bure," alishauri Sitta.Lakini Sitta aliwasha moto zaidi aliposema kwamba, wabunge wa kambi ya upinzani ni wanafiki kwa vile wamekuwa wakitoa kauli nyingi za namna hiyo.Sitta alisema hivi karibuni wabunge hao wa kambi ya upinzani walisema bungeni kuwa posho za wabunge ni kuwaibia wananchi lakini wanazipokea.

  Baada ya hapo wabuge waliendelea kubishana bila utaratibu, mpaka muda wa kikao ulipokaribia kwisha alitumia madaraka yake kuahirisha kikao hicho akisema: "Sasa muda umekwisha Nanahairisha shughuli za Bunge hadi jioni."Baada ya hapo wabunge walikaa kimya hadi alipotoka ukumbini na baadhi ya wabunge wakalipuka na kuanza kuimba wakisema: "CCJ! CCJ! CCJ!…."

  Ole Sendeka ataka bunge livunjwe
  Katika hatua nyingine Mbunge wa Simanjiro, Chrispher Ole- Sendeka (CCM), amemtaka Rais wa Jakaya Kikwete kutumia nafasi yake na kulivunja Bunge mara moja ili warudi katika uchaguzi kwa kile alichokieleza kuwa Bunge limejaa wahuni wengi.Ole Sendeka alitoa kauli hiyo jana nje ya viwanja vya Bunge wakati akizungumza na Mwananchi kufuatia mjadala mkali uliozua mabishano wakati wa kujadili hotuba ya bajeti ya Wizara ya afya na Ustawi wa Jamii.Sendeka alisema Bunge limekosa mvuto na hata jamii inayowasikiliza wanaona kuwa hakuna maana yoyote ya kuwa na Bunge ambalo limekosa mwelekeo kama ilivyo sasa kwa bunge la kumi.

  Mwanasheria Mkuu
  Hata hivyo, kauli ya Sendeka ilitofautiana na maoni nya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, aliyesema kuwa suala la malumbano ndani ya ukumbi wa Bunge ni kitu cha kawaida na kwamba halipaswi kuchukuliwa kama ni jambo kubwa kiasi hicho."Hapa sio jambo kubwa sana, wala sioni sababu za kusema ichukuliwe hatua gani kwakuwa mahali popote ambako kuna mabunge ya vyama vingi, lazima vitu kama hivi vitokee kwa hiyo naona ni vitu vya kawaida kabisa,'' alisema Werema.

  Source: Mwananchi
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 20. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #20
  Jul 13, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,176
  Trophy Points: 280
  Hiyo ya Sendeka Nimeipenda na angeongezea Wabunge Wa viti maalum wasiteuliwe Tena kupunguza Matumizi ya Serikali kwani hawana Faida yeyote kwa jamii zaidi ya kufanya fujo na kuzomea Bungen na kuuchapa usingizi! na wale wanaochangia hoja mia kwa mia then wanalia lia majimbini mwao kuna matatizo waondolewe kwa manufaa ya uma
   
Loading...