Serikali kuua zao la tumbaku ni mkakati wa wahisani au ni kuteleza kwa mbinu mbadala

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Zao la tumbaku ni moja ya zao la biashara ambalo lilikuwa linaingiza pato kubwa sana serikali,lakini ndilo zao lililokuwa na utitiri wa kodi unao mgusa mkulima moja kwa moja na kumtia umaskini wa kupindukia.

Ni miongoni mwa mazao ya siasa yanayo lengwa kimkakati na kuzungumzwa sana kipindi cha uchaguzi mkuu nchini ni pamoja Tumbaku,pamba,katani,kahawa n.k.

Angukola zao hili limezchagizwa na utitiri wa kodi za mateso huku makampuni yakitajirika, lakini pamoja na umaskini wa wakulima ndilo zao lilikuwa kuwa angalau lina unyanyua mkoa wa Tabora.

Tumbaku ina majani yasiyo zidi nane lakini limetengenezewa grades zaidi ya 72,kama njia ya kunyonya nokoa huyu wa jembe la mkono.

Anguko la za hili mpk leo serikali haojaainisha sababu zake,na hakuna mkakati madhubuti wa serikali kutafuta mbadala wa zao hili kwa wananchi wa Tabora na sehemu zinazo lima zao hili nchini.

Hii maanake nini,serikali haina mbinu mbadala ya kumnyanyua mkulima mdogo ambaye takribani 85% ya wananchi ni wakulima,na bajeti yetu ina kadiriwa zaidi ya 40% toka sekta hii binafsi(wakulima).

Ajabu ndilo zao na mazao mengine yaliyoundiwa board za mazao,zilizo kosa weredi wa kutatua changamoto za wakulima wa nchi hii.

Ukisikiliza kauli mbiu za serikali kuwataka vijana wajiajiri utasema ni kichekesho,kwa kuwa kauli zao hazina mkakati wa kuwaokoa vijana hawa wasio na ajira.

Wabunge wapo, wamebaki kusimamia posho na mishahara isiguswe na kusahau kuwa wao ni wawakilishi wa wnanchi pamoja na wakulima miongoni mwao.

Tujadili tutafute muafaka wa jambo hili, vinginevyo taifa linaanguka kwa kupoteza mwelekeo.
 
Ilani kwa serikali ipi,Ilani ya mwisho ilikuwa kwa awamu ya tano,hatujasikia kama rais wa awamu ya sita baada ya mwendazake aliendelea kuisimamia ilani hiyo hiyo.
Sawa, 2023 unaweza nikuta naelekea njia aliyotuchagulia mzee wa single dar. Maana!!!!
 
Hivi Tabora korosho haikubali, jaribuni bandugu, najua TBR kuna ardhi bora sana ya karanga, tulikuwa hadi tunatumia mafuta ya karanga, sijui Kama bado yapo, kwa kuwa madam kafungua masoko tulime, kule Burundi, Rwanda DRC ni soko zuri la karanga na mihogo
 
Zao kuu lilikuwa Tumbaku lakini jumba bovu kadondoshewa mrajisi. Karanga wanalima,ila walipeleka zao la jiopatroza kama mbadala lakini soko lake kizungumkuti
 
Hivi Tabora korosho haikubali, jaribuni bandugu, najua TBR kuna ardhi bora sana ya karanga, tulikuwa hadi tunatumia mafuta ya karanga, sijui Kama bado yapo, kwa kuwa madam kafungua masoko tulime, kule Burundi, Rwanda DRC ni soko zuri la karanga na mihogo
Mafuta ya karanga uliza na ya pamba toka VOIL walioiua ni akina nani. Acha kabisa nchi hii ngumu kuliko unavyotegemea!!! 😭 🙃
 
Back
Top Bottom