Serikali kutoa Miradi ya Bilioni 15 kwa wakandarasi wazawa

jembejembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
677
1,000
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amesema kuwa serikali ipo katika mkakati wa kuweka sheria ya kuwapatia zabuni za chini ya Tsh. bilioni 15 wakandarasi wazawa wa ndani ili waweze kuondokana na changamoto mbalimbali.

Ameyasema hayo mapema leo desemba 5,mkoani Arusha wakati akizungumza katika kongamano la 30 la Taasisi ya wahandisi Tanzania (IET) linalofanyika katika hotel ya Ngurdoto nje kidogo ya jiji LA Arusha.

Mhandisi Kamwelwe amesema kuwa ,utaratibu huo wa kuwapa zabuni wakandarasi wazawa utasaidia kuondoa malalamiko yaliyopo kwa wakandarasi hao ya kutokupewa kazi badala yake wanapewa wakandarasi kutoka nje ya nchi.

Amesema kuwa, wakandarasi wazawa wana uwezo mkubwa wa kutekeleza miradi mbalimbali ila changamoto kubwa ipo katika mitaji kwa ajili ya kuifanikisha miradi hiyo ,hivyo uwepo wa utaratibu huo utasaidia Sana kutekeleza kazi zao kwa ufanisi mkubwa.

Aidha amewataka wahandisi hao mbali na kuwa na taaluma ya uhandisi wahakikishe wanakuwa na taaluma nyingine ya utalaamu wa fedha ambao utawawezesha kuendesha miradi mbalimbali .

Hata hivyo amewataka wahandisi hao kujiendeleza zaidi na kufahamu Mabadiliko katika sayansi na teknolojia ,pamoja na kujifunza mbinu mpya za kazi ambazo zitawawezesha kuwa wabunifu zaidi.

Naye Raisi wa Chama cha wahandisi Tanzania ,Wakili Menye Manga amesema kuwa,mkutano huo umelenga kuangalia jinsi ya kuwajengea uwezo endelevu wahandisi na kuweza kuangalia changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi.

Amesema kuwa, changamoto kubwa inayowakabili wahandisi hao ni kutokuwa na sehemu maalumu ya kufanyia mazoezi pindi wanapohitimu kozi zao ,hivyo waliomba kupatiwa eneo maalumu kwa ajili ya kufanyia mazoezi ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wao.

Manga amewataka wahandisi hao kujipanga katika kusomea maswala ya sheria ambayo yatasaidia wahandisi hao kushughulika na maswala ya kisheria na kuweza kupata maamuzi muhimu.

Naye Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo amewataka wahandisi hao kufanya kazi zao kwa weledi mkubwa huku wakitanguliza maslahi ya nchi yao mbele katika maendeleo endelevu na maslahi mapna ya taifa kuweza kuangalia namna ya kuondokana na changamoto mbalimbali.

images%20(2).jpeg
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
172,741
2,000
Watalipwa kwa wakati?
Hawatalipwa pungufu?
Hawatatishiwa maisha wakidai haki yao?
Hawatasotea na kuzungushwa malipo yao?
 

mulaga

JF-Expert Member
Sep 2, 2019
3,156
2,000
Ttzo la wazawa si wazalendo. Mimi nadhani tungewapa nguvu JKT pamoja na JWTZ kipindi hiki cha amani ndio wapewe kandarasi nyingi angalau wao kidogo sio hizi kandarasi za wazawa wengi ni wababaishaji tu.
 

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
9,921
2,000
jembejembe,
Too late.
Watu waliahidiwa 2015 maneno hayo hayo.
Leo watu wanazimia kwa masimango ya Awamu ya 5.
Bora Kamwelwe ange toa tamko juu ya udhalilishaji wa wadau katika sekta yake.
Mengine ni bla bla tu.
 

Danp36

JF-Expert Member
Jul 31, 2010
1,957
2,000
Ttzo la wazawa si wazalendo. Mimi nadhani tungewapa nguvu JKT pamoja na JWTZ kipindi hiki cha amani ndio wapewe kandarasi nyingi angalau wao kidogo sio hizi kandarasi za wazawa wengi ni wababaishaji tu.
Kuu mbona kuna miradi jkt walishindwa maliza ? Tatizo litafutiwe dawa sio kutoa upendeleo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom