Serikali kutoa bilioni 235 Kuufungua Mkoa wa Mtwara Kwa Barabara za Lami

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,115
49,833
Hayo yameelezwa na Waziri wa Ujenzi prof.Makame Mbarawa Wakati Akishuhudia Utiaji Saini wa Ujenzi wa Barabara ya Mnivata-Newala-Masasi km 160.

======
BIL 234.5 KUUFUNGUA MKOA WA MTWARA KWA BARABARA ZA LAMI

Serikali imesaini mikataba miwili ya kuanza ujenzi wa barabara ya Mnivata – Newala – Masasi (km 160) pamoja na ujenzi wa daraja la Mwiti yenye jumla ya shilingi Bilioni 234.512 kwa lengo la kuwaondolea wananchi wa Mtwara kero ya usafiri na usafirishaji.

Tukio hilo limefanyika wilayani Newala mkoani humo ambapo limeshuhudiwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa na viongozi wengine wa mkoa, wabunge na wananchi ambapo pamoja na mambo mengine Prof. Mbarawa amesema kuwa ujenzi wa barabara hiyo utaboresha mtandao wa barabara na madaraja katika ukanda wa Kusini.

Akizungumza na wananchi wa mkoa huo wakati wa hafla hiyo, Waziri Prof. Mbarawa ameeleza kuwa barabara hiyo itaboresha usafiri na usafirishaji wa malighafi za viwandani kama makaa ya mawe na saruji, mazao ya chakula na kilimo, mifugo, uvuvi, bidhaa za kibiashara na mazao ya misitu kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mtwara pamoja na mikoa jirani ya Lindi, Ruvuma na Pwani kwenda maeneo mbalimbali nchini.

Aidha, Prof. Mbarawa, amewaasa wananchi wa Mtwara kutoa ushirikiano kwa makandarasi waliopata kazi ya ujenzi wa barabara hiyo pamoja na kujiepusha na vitendo vya uhalifu katika miradi hiyo.

"Hakikisheni mnatoa ushirikiano kwa vijana mtakaopata kazi katika mradi huu, muache tabia ya wizi wa vifaa, mkifanya hivi mtasababisha miradi kukamilika kwa wakati", amesema Prof. Mbarawa.

Waziri Prof. Mbarawa ameahidi kuendelea kuufungua mkoa wa Mtwara kwa kuunganisha mkoa wa Lindi na mikoa jirani kwa barabara za lami pamaoja na ujenzi wa reli na bandari.

"Nimepokea maombi ya barabara mbalimbali ikiwemo ya kuunganisha kwa lami barabara ya Newala-Mtama, Mtama-Tandahimba, Mtwara-Kilambo, Newala - Mbuyuni ambapo fedha zimetengwa na upembuzi yakinifu na usanifu wa kina unaendelea", amefafanua Prof. Mbarawa.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas, amesema utekelezaji wa mradi huo unaunganisha wilaya zote za mkoa huo na hivyo kutaimarisha shughuli za kiuchumi na kijamii na kupunguza gharama za maisha kwa mwananchi mmoja mmoja.

My Take
Kazi ya Kuifungua Nchi Kwa Lami Inaendelea,Waliodai Walijenga Sana Barabara Waoneshe walikuwa wanajenga Barabara zipi?
 
Hayo yameelezwa na Waziri wa Ujenzi prof.Makame Mbarawa Wakati Akishuhudia Utiaji Saini wa Ujenzi wa Barabara ya Mnivata-Newala-Masasi.

My Take
Kazi ya Kuifungua Nchi Kwa Lami Inaendelea,Waliodai Walijenga Sana Barabara Waoneshe walikuwa wanajenga Barabara Gani?

Tatizo unaleta taarifa kwa kushindana na marehemu, japo samia naye anaupiga mwingi.
 
Tunawazodoa wanaomponda na kudai hakuna kitu anafanya
Mama anafanya makubwa sana, japo na nyie mnazidisha sana kusifu mpaka watu wanahisi na wewe ni chawa promax, pia punguza kumzodoa marehemu, naye alifanya mazuri mengi na pia alifanya mabaya tuache kushindana naye, pambaneni kuleta maendeleo watu wataona wenyewe.
 
Mimi sio chawa na kama ni chawa basi ni WA kujitolea
 
Hayo yameelezwa na Waziri wa Ujenzi prof.Makame Mbarawa Wakati Akishuhudia Utiaji Saini wa Ujenzi wa Barabara ya Mnivata-Newala-Masasi.

My Take
Kazi ya Kuifungua Nchi Kwa Lami Inaendelea,Waliodai Walijenga Sana Barabara Waoneshe walikuwa wanajenga Barabara Gani?

Hizi bilioni za nani?
 
Mama anafanya makubwa sana, japo na nyie mnazidisha sana kusifu mpaka watu wanahisi na wewe ni chawa promax, pia punguza kumzodoa marehemu, naye alifanya mazuri mengi na pia alifanya mabaya tuache kushindana naye, pambaneni kuleta maendeleo watu wataona wenyewe.
Hizo pesa zilikuwa na kazi nyingine. DP World inawazungusha Wazanzibari Tanganyika.
 
Back
Top Bottom