Serikali kusaini mikataba na wabanguaji Korosho

Serikali kusaini mikataba na wabanguaji Korosho

diana chumbikino

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
428
Reaction score
368
_102231932_79a09ca1-a549-449d-86b5-19e38a736399.jpg


SERIKALI leo inasaini mikataba na wamiliki wa viwanda vya ubanguaji wa korosho waliojitokeza kwa ajili ya kubangua korosho msimu wa mwaka 2018/19 zilizonunuliwa kwa bei ya Sh 3,300 kwa kilo. Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga alisema hayo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari mjini hapa. Alisema hivi karibuni serikali ilitangaza kuwa korosho gha zote zitabanguliwa nchini hivyo utekelezaji wa jambo hilo umeanza na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko itaingia mikataba ya ubanguaji.

Pamoja na wamiliki wa viwanda kupewa kazi ya kubangua korosho lakini pia serikali imewakaribisha wananchi kujitokeza kubangua korosho za serikali kupitia vikundi au mtu mmoja mmoja. "Wananchi wenye uwezo wa kubangua tunawaomba waende Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (Sido) kwa ajili ya kujiandikisha ambapo mpaka sasa watu 126 kwa ajili ya ubanguaji na tani 29 zimechukuliwa kwa ajili ya kuanza kubanguliwa," alisema Hasunga.

Katika mkutano huo, Hasunga alimpongeza Rais John Magufuli kwa kushuhudia utiaji wa saini mkataba wa mauziano ya mahindi kati ya Wakala wa Taifa wa hifadhi ya Chakula (NFRA) na Shirika la Chakula Duniani (WFP) wa Sh bilioni 21 zitakazoiwezesha NFRA kununua mahindi kwa wakulima hivyo kuimarisha soko la nafaka nchini.

Hasunga alisema kuwa pamoja na kuanza ubanguaji kupitia Sido lakini serikali imeanza mchakato wa kufufua viwanda vya ubanguaji vya serikali na watu binafsi nchini ili kuongeza ajira kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuanzisha vituo vya wabanguaji wadogo. Akizungumzia kuhusu malipo ya korosho na uhakiki wa wakulima alisema kuwa tayari kiasi cha korosho ambayo imekusanywa kwenye maghala makuu ni tani 203,938.3 wakati korosho iliyopo kwenye vyama vikuu vya ushirika ni tani 29,803.53.

Idadi hiyo inafanya jumla ya korosho yote iliyopokelewa kwenye vyama vya ushirika na maghala makuu kuwa tani 233,741.83 sawa na asilimia 84.7 ya lengo lililowekwa la ukusanyaji katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma na Pwani. Kuhusu malipo ya wakulima alisema kuwa miamala ya malipo ambayo imefanyika ni 261,458 yenye jumla ya watu 203,569. Aidha, kati ya vyama 617, vyama 490 vilimelipwa.
Katika Mkoa wa Mtwara jumla ya vyama 39 havijalipwa, Mkoa wa Lindi ni vyama vitano na Ruvuma ni viwili. Serikali imejipanga ndani ya wiki mbili vyama hivyo vitakuwa vimelipwa.

Waziri Hasunga alisema zaidi ya Sh bilioni 30.7 zilizohakikiwa hazijaingizwa kwenye akaunti za wakulima kutokana na taarifa za baadhi ya wakulima hao kutofautiana majina. "Tunawaomba sana wananchi kwenda benki kujiridhisha kama akaunti zao zinafanya kazi kwani serikali ina fedha za kuwalipa wakulima wote wa korosho," alisema "Tena nisisitize kwa wale wanaofanya biashara ya korosho kinyume na utaratibu maarufu kama Kangomba wajisalimishe na kuomba radhi wenyewe kuliko kusubiri serikali iwabaini," alisema Alisema wizara yake imeweka mikakati mbalimbali ambapo hadi kukia Januari 31 mwaka huu uhakiki wa wakulima wanaostahili kulipwa uwe umekamilika na zaidi ya asilimia 80 ya wakulima wawe wamelipwa. Pia aliwataka wananchi kupuuza taarifa mbalimbali zizotolewa na baadhi ya wananchi wasiolitakia mema taifa kupitia mitandao ya kijamii kuwa serikali hailipi wakulima badala yake amesisitiza kuwa serikali ina fedha za kutosha kulipa wakulima wa korosho isipokuwa kangomba wao hawatalipwa.
 
Back
Top Bottom