Serikali kuongeza bajeti NIMR | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali kuongeza bajeti NIMR

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Josh Michael, Feb 27, 2010.

 1. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #1
  Feb 27, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  SERIKALI imesema inakusudia kuiongezea bajeti Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) ili iweze kutekeleza malengo ya milenia kwa ajili ya utafiti.
  Akizungumza wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya taasisi hiyo jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa, alisema hatua hiyo itasaidia kuboresha utendaji wa NIMR, kuinua viwango vya maisha ya jamii na kukuza uchumi.
  “Serikali inathamini sana mchango wa NIMR katika suala zima la kuendeleza afya za jamii yetu, napenda kuihakikishia bodi hii kuwa tutatenga asilimia mbili ya bajeti ya wizara yangu kwa shughuli za utafiti,” alisema Waziri Mwakyusa.
  Alisema katika ulimwengu wa sasa kuna magonjwa mengi ambayo yamekuwa yakiibuka, kama vile saratani, shinikizo la damu, kiharusi, kisukari na magonjwa ya moyo ambayo katika nchi zilizoendelea yanasababisha vifo kwa asilimia zaidi ya 60.
  Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NIMR, Dk. Mwele Malicela alisema pamoja na mafanikio hayo, taasisi hiyo bado inakabiliwa na uhaba wa fedha kwa ajili ya utafiti, maabara, vitendea kazi, magari na majengo ya ofisi za taasisi hasa katika vituo vya utafiti vya Amani, Tabora, Muhimbili na Tanga.
  “Mbali na tatizo hili, NIMR bado inakabiliwa na uhaba wa watafiti katika nyanja za sayansi ya jamii, demografia, afya ya mazingira, takwimu na uchanganuzi wa taarifa za utafiti na sera,” alisema Malicela. Bodi mpya iliyoteuliwa inaundwa na wajumbe 12 ambao ni Dk. Hassan Mshinda, Dk. Luka Siyame, Dk. Edith Ngirwamungu, Jonathan Tangwa, Dk. Malick Abdallah Juma, Profesa Eligius Lyamuya, Dk. Catherine Kuwite, Elli Pallangyo, Profesa William Mahalu na Dk. Salim Mohamed Abdulla.  [​IMG]


  juu[​IMG][​IMG]
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...