Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,292
- 15,750
Fuatilia yanayojiri Bungeni leo Aprili 19, 2023 kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 11, Kikao cha 9.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amesema "Kuna changamoto ya Popo wanaozunguka maeneo ya Dar es Salaam hususani maeneo yanayozunguka Ikulu, Serikali imeanza mchakato wa kuwaondoa, tunapowaondoa wanarudi, tumeanza utaratibu wa kuwaondoa kabisa.”
Amesema hayo baada ya Mbunge wa Ilala na Naibu Spika wa Bunge, Mussa Azan Zungu kuuliza juu ya hatua zinazochukuliwa na Serikali kuhusu Popo waharibifu na wachafuzi wa mazingira katika Kata ya Kivukoni.
Bajeti Ofisi ya Rais
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene amewasilisha Bajeti ya Tsh. Trilioni 1.1 kutoka Ofisi ya Rais na kufafanua matumizi yake ambapo Ofisi ya Rais Ikulu itatumia Tsh. Bil. 32, Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri Tsh. Bil. 678.19 za Matumzi ya Kawaida na Maendeleo Tsh. Bil. 181.99, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi Matumizi ya Kawaida Tsh. Bil. 10.8 na Maendeleo Tsh. Bil. 1.9
Menejimenti ya Utumishi wa Umma Tsh. Bil. 57.13 Matumizi ya Kawaida, Maendeleo Tsh. Bil. 12.187, Sekretarieti ya Ajira Matumizi ya Kawaida Tsh. Bil. 10.13 na Maendeleo Tsh. Bil. 2.5, Utumishi wa Umma Matumizi ya Kawaida Tsh. Bil. 8.3 na Maendeleo Tsh. Mil. 300 na Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Maumizi ya Kawaida Tsh. Bil. 3.8 na Maendeleo Tsh. Mil. 450