Dah wakati mwingine inashangaza kuona JF ni sehemu ya kulalamika na kulialia juu ya kila uamuzi wa serikali. Ni serikali ipi duniani haikopi?
Serikali ina njia kadhaa ya kupata fedha, borrowing is among them. Wanaosema kwamba serikali haifanyi bihashara ni dhahiri kwamba elimu yao haijai kiganjani; serikali inauza na kununua securities takriba kila juwa linapochomoza. Kabla hatujaendeleza "tamaduni" ya kulalamika na kukemea ni bora tukarejea darasani kidogo na kuangalia mahusiano ya shughuli za serikali, benki, na uchumi wa nchi. Vinginevyo wanaotusoma hapa JF (including the Mkulos) wanatuona kana kwamba akili zetu ni mchanyato wa ubongo na togwa.
Nadhani ndugu yangu una uhuru wa kusema kama sie tulivyo na uhuru wa kusema. But unapotuhukumu kuwa sie tuna mtindio wa akili kwakweli unakuwa umetukosea haki kwani tunatumia haki yetu ya kikatiba kuzungumza lile tunaloliona. Sasa ngoja nikupe darasa kwanini sie tunalalamika maana umetwambia hatuendi darasani.
Serikali inapokopa kwa kukutumia T-bills, au government bonds ni kwamba zile ni securities ambazo inazitumia kuraise liquidity (mkusanyiko wa fedha). Lakini tofauti yake na mkopo ni kwamba serikali inatangaza gawio au interest inayotaka kulipa kwa kuazima hizo pesa hivyo basi unakuta maranyingi interest hiyo haiwi kubwa kulinganisha na mkopo wa kawaida. Vile vile Serikali inakuwa na discretion ya lini italipa hizo pesa mfano kuna 90 days bills, 180 days, 360 days, 1 year bond, 2 year, 5 year etc. Lakini unapokuwa umekopa katika mabenki mfano overdraft facility kila siku wanakuwa wana charges zinazoambatana na mkopo huo. Vilevile ile overdraft inachajiwa interest in accordance to the prevailing market rates.
Sasa kwa Tanzania interest katika loanable funds ni 18-23% kama haijabadiilika kuzidi. Wakati interest kwenye Tbills ni lower zaidi ya hiyo kwa akili ya mtu wa kawaida unadhani inamake sense kwenda kuchukua mkopo wenye riba ya juu ukaacha mkopo wenye riba ya chini unless uwe umekunywa pombe. Na kwanini wasiissue securities kuraise more capital? Unakuta kwamba serikali imekwama with liquidity shortage na sasa inatafuta a quick alternative ya kuraise cash.
Sasa katika bank njia rahisi ya kupata cash ni kuchukua overdraft facility ambayo ni mara moja kuipata kama wewe mteja mkubwa. Hatari iliyopo ni charges zinazoambatana na facility hiyo na interest inayochagiwa. Vilevile kama serikali ikishindwa kulipa inamaana serikali itakuwa imeweka collateral (rehani) rasilimali fulani ambazo sijui bunge lina taarifa nazo au la? Sasa kimkopo kama serikali yetu iko makini sio tatizo but kama serikali yetu haina misingi mizuri ya usimamiaji wa kodi matumizi ya mabovu ya pesa ni hatari kwasababu hizi pesa zinatakiwa kulipwa on time na ukichelewa deni linaongezeka.
Sasa usifikiri watu tunapayuka kama wendawazimu bali tuna akili zetu na vilevile tumeshaona vyanzo vyote unavyovitazama wewe tukaona kwamba hili linaweza kusababisha a sovereign debt crisis kama iliyopo Greece na Spain. Na vilevile hatulalamiki ila tunaleta changamoto kwasababu nchi ikishatawaliwa na mabenki ndio hatuna sauti wananchi zaidi ya kukubali mabadiliko hivyo kabla hatujafika huko tusema tusije tukaambiwa mlikuwa wapi wakati tunafanya maamuzi.
Kuna maswali matatu naomba niwaulize Mkulo na wenzie:
a. Wameshindwa nini kuraise funds kwenye capital market (soko la mitaji) kwa kuuza hisa za serikali mfano bonds?
b. Wameshindwa nini kwenda kukopa katika development banks kama World Bank, IMF, ADB, EADB kuna ishu gani inaendelea?
c. Wameshindwa nini kupunguza fiscal policy budget instead budget ya serikali inakua kila siku? Hawajui kuwa mtu ukiwa huna kitu unapunguza matumizi yako kuweza kusave kiasi kidogo cha pesa?