Serikali kukodi ndege 2 na kuzirusha kwa mkupuo pamoja na anayotumia rais ni kubana matumizi

Labda wewe ulikuwa unatakaje utuambie...!?
Maana Wote wapo kazini, unataka wasubiri riporti ofisini..!?
Au unataka waende na baiskeli..!?
Ukisikia Garama za uendeshaji WA serikali Ndo huo..!!
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Mkuu, protokali hairuhusu kuwarundika viongozi wote waandamizi kwenye chombo kimoja. By the way, hayo matumizi yao yako ndani ya bajet sawa na stahiki ya vyeo vyao.
 
Saa ulitaka waende kwa bajaji?,
wote hao uliowataja wanakidhi vigezo vya usafiri huo,kuliko kuongoza msafara wa magari toka dar mpaka kilimanjaro
 
Saa ulitaka waende kwa bajaji?,
wote hao uliowataja wanakidhi vigezo vya usafiri huo,kuliko kuongoza msafara wa magari toka dar mpaka kilimanjaro
 
Kumbe ttzo ni kuogopa wasije kufa kwa pamoja?? Kwa hiyo mnapingana na Mungu kuwa kila nafs itaonja mauti??? Tupo zaidi ya 50m kwani hakuna wa kuchukua hizo nafas 3 pekee?? Msinitafute lakini sijamtaja MTU ati
 
Haah..watu kwa kulia lia hamjambo!! Hajaenda nchi za nje mmelia..hajasafiri safari za ndani kila mmoja analia.. mbona kajichimbia dar tu? Wamekodi ndege kwa ajiri ya kufanya kazi zao kwa mda muafaka..mmelia..heee...mwacheni afanye kazi na nyinyi fanyeni yenu.
 
Unawapakiaje viongozi wote wakubwa wa nchi kwenye ndege moja? Unajua madhara yake? Tufikiri kidogo.
Tunafikiri kama Masaburi alivyotuasa....Habyarimana n.a. Rais wa Burundi walipanda ndege moja....na wakamalizika pamoja
 
Ww unafikiri madhara ni wao kupata ajali hata wakianguka wote kwani watanzania so wengi kwa kuongoza au unawategemea hao tu
Wewe unafikiria gharama za kukodi ndege lakini gharama kubwa ya kufanya uchaguzi huwazi kwa kuwa moyo na fikra yako zimefuzibwa na chuki. Gharama ya kupoteza viongozi ni kubwa zaidi ya gharama ya fedha huwezi kujua kitachotokea hapo kwenye mpito.
 
Waulize wanyarwanda na warundi madhara waliyopata baada ya tarehe 6/4/1994. Siyo kila jambo la kushabikia.


President Habyarimana wa Rwanda na Ntaryamira wa Burundi walitunguliwa angani kwa Kombora lililorushwa na Wanamgambo wa RPF wakiongozwa na Paul Kagame waliokuwa karibu na Airport ya Kigali wakati Ndege ikijiandaa ku land!


Walikuwa wakitokea Arusha kwny Mkutano wa ulioitishwa na Rais Ally Hassan Mwinyi wa Tanzania kuhusu Usuluhishi wa Mgogoro wa Rwanda ndipo Rais wa Burundi akaomba Lifti kwny Ndege ya Rais Habyarimanama ndipo akajikuta kaingia kwny Target isiyomhusu!
 
Back
Top Bottom