Tetesi: Serikali kujipatia Tender yenyewe....

boja

Member
Nov 8, 2012
74
189
Habari wakuu..
Nimejaribu kufuatilia uvumi wa Serikali kuanza kujipa tenda mbalimbali zikiwemo za ukandarasi
1.kuna zile Hostel za Udsm Serikali imejipa tenda yenyew....

2.Kuna ujenzi wa NHC nako Serikali imejipa Tender yenyew...

Sasa swali hivi huo mzunguko wa Pesa utatoka wapi ile hali pesa inarudi kwa huyo hyo alieitoa..?
Na kodi itapatikana aje...??
IMG_20170119_141006.png
IMG_20170119_141027.png
 
Habari wakuu..
Nimejaribu kufuatilia uvumi wa Serikali kuanza kujipa tenda mbalimbali zikiwemo za ukandarasi
1.kuna zile Hostel za Udsm Serikali imejipa tenda yenyew....

2.Kuna ujenzi wa NHC nako Serikali imejipa Tender yenyew...

Sasa swali hivi huo mzunguko wa Pesa utatoka wapi ile hali pesa inarudi kwa huyo hyo alieitoa..?
Na kodi itapatikana aje...??View attachment 461622View attachment 461623
hii ni shida uchukue pesa za wananchi kupitia kodi tozo mbalimbali fine nk then uzirudishe kwa mishahara ya watu kama laki 500 na utegemehe kupata mzunguko ni ndoto
 
Hii lazima ihojiwe Bungeni japo hoja hii itashindwa kutokana na wingi wa Wabunge wa CCM lakini ni vyema ibaki kwenye kumbukumbu za Hansard kwa matumizi ya hapo baadaye. Ya Leo sio ya Kesho!! Tafakari....
 
Hakuna cha tender wala nini, sema taasisi za serikali zimegeuzwa taasisi za madali, hao wote hawana uwezo wa kujenga majengo hayo, wana sub kazi zote wao wanapata profit tu.
 
JPM anavuruga utaratibu wa PPRA.....tender zote amempa mtoto wa dada yake! Ina maana ni kampuni yake! Anafanya biashara akiwa ikulu kumbe ukali ule ni kutisha watu Ili aibe vizurii
 
Mbona miradi mingi sana imejengwa na makampuni ya kigeni? Hakuna aliyelalamika na juzi mmeleta mada kupitia zitto kwamba wachina wanataka kampuni ya kwao ijenge reli kwa sababu wanatoa pesa kwa maana nyingine wanataka irudi kwao. Halafu makampuni mengi ya kizalendo estimates ziko juu sasa serikali imeamua kutumia ili ipate kujua estimates nzuri. Kuhusu hosteli za chuo si walipambanishwa wengine wakatoa gharama za juu karibu mara mbili ya tba hata kama wewe utachagua IPI? Pili nhc wakipata mjenzi cheap hata gharama za nyumba zinashuka, kama tba atadeliver halafu makampuni mengine yaendelee kuweka gharama za juu kweli wataendelea kukosa tender.
 
na akikuta bei anakuchana laivu kwenye mkutano jengo lake kajenga la bei ghali ni bilion kumi tu ubora mtajijua wenyewe hata liwe refu had kwa Mungu ni bilion kumi tu mnabagein nae mzee wa vitengo vyote.
 
NI WAKATI WA KULIMA WATANZANIA SI LAZIMA MFANYE BIASHARA ZA UJENZI. MKALIMEEEE.
 
Mkuu, katika huo ujenzi, Serikali inauza materials kama mchanga, kokoto, nondo, bati, misumari. Tiles nk kwenye miradi yake? Au bidhaa hizo zinanunuliwa kwa wafanyabiashara na hivyo kuongeza fedha kwenye mzunguko?

Je vibarua wanaoshiriki kwenye miradk hiyo wote ni waajiriwa wa Serikali na kwamba wanaposhiriki kwenye miradi hiyo ni sehemu ya kazi zao na hivyo hawalipwi chochte?

Najaribu kuwaza tu maana hoja zingine ukizisoma unapatwa na hasira kwa jinsi Watanzania wasivyo na uwezo wa kufikiri
 
Back
Top Bottom