Tabutupu
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 13,185
- 18,513
Inasemekana kuwa serikali inaweza kuwa na mpango wa kuzirudisha shule za vipaji maalumu hasa kwa kuboresha zile zilizopo na kujenga nyingine kila mkoa ili kulinda na kukuza vipaji vya watoto wa kitanzania bila kujali vipato vya familia wanazo toka.
Shule hizo ambazo zitakuwa kwa kila kanda kwa Alevel na kila mkoa kwa Olevel zitachukua watoto walifanya vizuri kutoka shule za Olevel na msingi kama zilivyo kuwa hapo awali shule za ilboru ,mzumbe, Msalato etc.
Mpango huo utagusa kozi zote na combination zote hapa nchini na zitatuhusu hata vijana kutoka nchi za jirani kujiunga kwa ada kubwa au kwa ufadhili za serikali zao.
Mpango huo pia utaenda sambamba na kuandaa vyuo maalumu vya elimu ya juu kwa vijana wanao fanya vizuri ili kujenga uzalendo na kupata vijana wazuri watakao chukua majukumu makubwa hapa nchini.
Pamoja na hilo pia kuna uwezekano wa kufufua chuo cha siasa ambapo hakuna mtu atakaye gombea urais au ubunge bila kupitia chuo hicho ambacho kitajikita kwenye utawala, Katiba, uongozi, Mambo ya nje, Siasa na mambo yanayo ihusu Tanzania kwani kumebainika wengi wanaogombea ubunge hata urais hawaijui vizuri nchi yao.
kwa heri...