Serikali kufunga shule na vyuo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali kufunga shule na vyuo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Michael Amon, Mar 26, 2012.

 1. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #1
  Mar 26, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  SERIKALI imesema, itafunga shule na vyuo vyote ambavyo havijasajiliwa na ambavyo havijakidhi vigezo na viwango vya kutoa elimu nchini ili kulinda hadhi ya elimu ya Tanzania iliyovamiwa na soko holela.
  Hayo yalibainishwa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo Stadi nchini, Philiph Mulugo wakati wa akihitimisha kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Mamlaka Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta), yaliyofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Tangamano jijini Tanga.
  Akizungumza kwa ukali, Mulugo alisema sekta ya elimu haiwezi kuachwa hivi hivi kama haina mwenyewe, haiwezekani elimu ikaendeshwa kiholela.

  Alisema haiwezekani mwanafunzi wa darasa la saba anajiunga na shule ya sekondari huku hajui kusoma na kuandika.
  “Siku hizi kuna matangazo mengi ya shule na vyuo kwenye vyombo vya habari ambavyo havijasajiliwa, hivyo nimeagiza Veta kufanya ukaguzi na kuvibaini vyuo holela na kuvifunga ili kulinda hadhi ya elimu yetu,”alisema.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Veta, Profesa Idrissa Mshoro aliwataka Watanzania kubadili mtazamo kuhusu vyuo vya Veta, wakidhani ni kwa ajili ya wale waliofeli darasa la saba au kidato cha nne.
  Alisema Veta sasa inatoa mafunzo kwa wote na kuna fani mpya ambazo zinahitaji wahitimu waliofaulu vizuri.
  Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Veta, Zebadia Moshi aliwataka wadau wa elimu kujenga zaidi vyuo vya ufundi na kwa kuwa ni suluhisho pekee la tatizo la ajira kwa vijana.
  Alisema vijana wakipatiwa elimu ya ufundi, na kupewa vifaa, wataweza kujiajiri wenyewe baada ya kumaliza mafunzo ya Veta.
   
 2. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Nchi hii bwana mabo yake valivali kweli akiongea na wahandishi wa habari huku mishipa ya shingo ikimtoka,yule mama wa Baraza la mitihani alisema wote walio faulu mtihani wa darasa la saba watafanya mtihani wa kuchujwa hukohuko hadi leo mitihani haijafanywa wala nini kama hujafanya uchunguzi ya nini unaongea ni JK na watendaji wake hao,yote kwa yote Tanzania nchi yangu nakupenda kwa moyo wangu woooooote,lakini CCM siwapendi kwa mwili wangu wote
   
 3. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #3
  Mar 26, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,036
  Likes Received: 3,065
  Trophy Points: 280
  Tatizo lilianza pale viongozi wa umma waliporuhusiwa kujishughurisha na biashara bila kuzingatia taratibu za kiutumishi na kiuadilifu katika biashara hizi make wengi wao wameanzisha miradi hii siyo tu kufanya biashara bali kuwaibia wananchi na serikali kwani ukifuatilia kwa karibu ndo miradi hii isiyokuwa na maelezo imeanzishwa katika mazingira gani lakini pia kupitia miradi yao wanakwepa kulipa kodi na huku wakitumia mali za serikali kuendeshea miradi yao binafsi...yaani,we acha tu mwana wa kwetu maana 2015 siyo mbali tena,tujipe moyo na tujipange upya
   
 4. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #4
  Mar 26, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Kama huipendi CCM kwa mwili wako wote basi utakuwa unaipenda kwa akili yako yote.
   
 5. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #5
  Mar 26, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Usije ukashangaa 2015 inafika na bado Wananchi wakaichagua CCM.
   
 6. C Programming

  C Programming JF-Expert Member

  #6
  Mar 26, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 2,741
  Likes Received: 1,748
  Trophy Points: 280
  computing center.....kufugwaa
   
 7. z

  zee la weza Senior Member

  #7
  Mar 26, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 191
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  huyo naibu waziri jina lake halisi ni amimu mlugo, hilo laphilipo mlugo ni la ndugu yake, alitumia vyeti vya ndugu yake, yeye alifeli peleleza watu waliosoma nae songea boys. Halafu huyu kilaza eti ndie kawekwa wizara ya elimu. Je, tutafika?
   
 8. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #8
  Mar 26, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  mnh makubwa....
   
 9. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #9
  Mar 27, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Computing center ipi hiyo mkuu?
   
 10. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #10
  Mar 27, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Kumbe huyu jamaa ni kilaza eee??? Na ndio maana serikali yetu haishiwi kuwa na viongozi wa ajabu ajabu. Embu tupe data zake mkuu,
   
 11. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #11
  Mar 27, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Madogo yana nafuu.
   
 12. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #12
  Mar 27, 2012
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  I don't know why they have to say in stead and place of doing it!!!
   
 13. l

  lemikaoforo Member

  #13
  Mar 27, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Je,serikali itafunga shule zake ambazo wanafunzi wanamaliza darasa la saba bila kujua kusoma na kuandika? Huko english medium mara chache ktoke ahivyo
   
 14. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #14
  Mar 27, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,036
  Likes Received: 3,065
  Trophy Points: 280
  Mkuu ya Wade haujayasikia nini?Tumeanza ghana tukaja Zambia na sasa ni Senegal,tuambizane nani anafuatia,ama Kas,ama Kus ama Mash...M4C is now on the way down to yr home
   
 15. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #15
  Mar 27, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Sina habari mkuu. Embu nipe data za wade
   
Loading...