Serikali: Katika awamu ya 5 viwanda 8,477 vimeanzishwa katika mikoa 26 ya Tanzania Bara

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Serikali imesema tangu Awamu ya Tano iingie madarakani, viwanda 8,477 vimeanzishwa katika mikoa 26 ya Tanzania Bara na kati ya hivyo, vikubwa ni 201, vya kati ni 460 vidogo ni 3,406 na vidogo sana ni 4,410.

Hayo yalielezwa jana bungeni na Wizara ya Viwanda na Biashara wakati ikijibu swali la Mbunge wa Mbulu Mjini, Zacharia Issaay (CCM).

Katika swali lake, Issay alihoji ni lini Serikali itaanza kufanya tathmini ya mafanikio ya viwanda 100 kwa kila wilaya ili kuchochea uchumi wa nchi.

Ikijibu swali hilo, Wizara ya Viwanda na Biashara ilieleza kuwa Serikali ilifanya tathmini ya jumla ya upimaji wa mafanikio ya azma ya ujenzi wa viwanda Februari, mwaka huu ambayo ilionyesha jumla ya viwanda 8,477 vimeanzishwa katika mikoa 26 ya Tanzania Bara tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani.

Vilevile wizara ilisema kuwa kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tamisemi na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, imeandaa mpango mahsusi wa kufanya tathmini pana ya viwanda vyote vilivyopo Tanzania Bara mwaka 2020/2021 kupitia mpango maalumu unaojulikana kama Industrial Mapping.

Ilieleza kuwa mpango huo utazingatia pia kufanya tathimini ya mpango wa viwanda 100 kila mkoa na utabainisha idadi na aina ya viwanda vilivyopo nchini, ajira, bidhaa zinazozalishwa, mapato, teknolojia zinazohitajika pamoja na malighafi zinazotumika ili uanzishwaji wa viwanda uendane pia na malighafi zinazopatikana hapa nchini ili kuwa na viwanda endelevu.

Aidha, wizara hiyo ilieleza kuwa kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za Serikali pamoja na sekta binafsi, inaendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ya kuendeleza ujenzi wa viwanda ili azma ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati unaojengwa kupitia viwanda, iweze kufanikiwa ifikapo mwaka 2025.

Pia, wizara hiyo iliweka kumbukumbu sahihi kwamba Ofisi ya Rais Tamisemi kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara ilianzisha kampeni mahsusi yenye lengo la kufanikisha ujenzi wa viwanda vipya 100 kwa kila mkoa ili kuunga mkono azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya ujenzi wa uchumi wa viwanda, na si viwanda 100 kwa kila wilaya kama swali la msingi lilivyouliza.
 
Hivi viwanda vimefunguliwa wapi? Vinazalisha nini? Halafu mwenye kujua mfano wa kiwanda kidogo sana anitajie kimojawapo
 
Hivi viwanda vimefunguliwa wapi? Vinazalisha nini? Halafu mwenye kujua mfano wa kiwanda kidogo sana anitajie kimojawapo
Kiongozi, hizo ni hallucinations za Jiwe.

Hata barabara za enzi ya Mzee Mkapa kazifungua upya kwamba ni za awamu ya tano.

Halafu, watupe maana ya kiwanda kidogo. Kama vyerehani vinne ni kiwanda kidogo, hapo wamefeli sana maana hata wazamani wamefunga maana hakuna pesa kwa sababu kazuia mzunguko wa hela.
 
Kitu hupimwa kwa output, viwanda 8000+ vipya lazima uagizaji bidhaa toka nje ya nchi ungepungua kwa walau kwa 30 - 40%.

Vipi watanzania wenzangu kama mmeshayaona mabadiliko ya upatikanaji wa bidhaa bora nchini ...local content imepaa?

Output detais ni kama:-
1. Viwanda hivyo vinatengeneza bidhaa X, Y,Z
2. Uzalishaji wa bidhaa zetu nchini umependa toka X kufikia Y
3. Uagizaji bidhaa nje umeshuka toka X hadi Y (%).
4. Ajira kwa watanzania hasa vijana imependa toka X hadi Y ni walioajiriwa ama kujiajiri kwenye viwanda hivi.
5. Exportation ratio imepanda toka X hadi Y kwa mwaka huu wa fedha.

Bila haya basi watanzania endeleeni nakusikiliza ngojera kama zile za shule ya msingi...
 
Nilishaomba sana tuache kuhesabia vyerehani na machine za kusaga mahindi kwenye "viwanda" vyetu. Tunajidanganya.
 
Jf hebu anzisheni jukwaaa la liberty, huko tuwe tunaruhusiwa kuongea chochote bila kupingwa.
Hivi viwanda viko wapi, mimi Niko Dar tangu 2014 naona viwanda vilevile vya wahindi na wachina.
 
Kitu hupimwa kwa output, viwanda 8000+ vipya lazima uagizaji bidhaa toka nje ya nchi ungepungua kwa walau kwa 30 - 40%.

Vipi watanzania wenzangu kama mmeshayaona mabadiliko ya upatikanaji wa bidhaa bora nchini ...local content imepaa?

Output detais ni kama:-
1. Viwanda hivyo vinatengeneza bidhaa X, Y,Z
2. Uzalishaji wa bidhaa zetu nchini umependa toka X kufikia Y
3. Uagizaji bidhaa nje umeshuka toka X hadi Y (%).
4. Ajira kwa watanzania hasa vijana imependa toka X hadi Y ni walioajiriwa ama kujiajiri kwenye viwanda hivi.
5. Exportation ratio imepanda toka X hadi Y kwa mwaka huu wa fedha.

Bila haya basi watanzania endeleeni nakusikiliza ngojera kama zile za shule ya msingi...
Kiongozi, hamna haja ya kuumiza vichwa vyetu kuhusu viwanda hewa.

Uhaba wa sukari ni jibu tosha. Hadi leo sehemu kubwa ya mafuta ya kupitia yanatoka nje. Bado tuna sabuni za nje ya nchi. Dawa kama paracetamol bado zinatoka India.

Kazuia maziwa ya brookside toka Kenya. Ya kwetu hayana kiwango. Lakini wanamlinda mchangiaji qa CCM auze maziwa yake.
 
Viwanda 8000? Mbona hatuoni impact yeyote katika uchumi wetu, sukar tumefeli ..viwanda vyote hivyo lakn bdo import vibirit stick sindano viwembe n.k sasa hivyo viwanda ni vya nn?
 
Back
Top Bottom