SERIKALI: Katiba mpya 2014 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SERIKALI: Katiba mpya 2014

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Elba, Mar 24, 2011.

 1. Elba

  Elba JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 383
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  SERIKALI imesema mchakato wa mabadiliko ya Katiba utaanza hivi karibuni na itahakikisha kuwa Katiba mpya inapatikana mwaka 2014.

  Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba, Oliver Mhaiki, alipokuwa akijibu hoja za wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Sheria, Katiba na Utawala inayoongozwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Pindi Chana, iliyotaka kufahamu jinsi serikali ilivyojipanga kwa mchakato huo.

  Alisema maandalizi ya kuanza kwa mchakato huo yamekamilika na tayari muswada wake umeshapita katika vikao husika na kwamba kinachosubiriwa kwa sasa ni kufikishwa bungeni.

  “Mchakato wa katiba itakayotokana na ridhaa ya wananchi utakamilika baada ya miaka miwili kutoka sasa. Wizara ilishaandaa waraka kuhusu suala hilo na ulishafikishwa katika kikao cha kamati ya ufundi ya serikali inayoongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, kwa hatua zaidi.

  “Kamati ya Luhanjo ilishaujadili waraka na iliupeleka katika kikao cha baraza la mawaziri ambalo lilishaketi na kuupitisha waraka huo…hatua inayofuatia sasa ni waraka huo kupitiwa kama muswada kwa ajili ya kuwasilishwa kati ya mwezi Juni au lile Bunge la Novemba,” alisema Mhaiki.

  Ufafanuzi huo ulitokana na maswali yaliyoulizwa na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Angellah Kairuki na Mbunge wa Jimbo la Muhambwe, Felix Mkosamali (NCCR-Mageuzi), ambao kimsingi walitaka kujua Katiba mpya itapatikana lini na kutaka kujua nini kinaendelea tangu Rais Jakaya Kikwete atoe tamko lake kuhusu suala hilo.

  Source: Tanzania Daima

  Wanajamvi, siamini kama sisiem inaanza kuchimba kaburi lake!
   
 2. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,689
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  sawa tunaisubiri hiyo katiba mpya ila tunawaomba ule usemi wa U cant c the gud of it until is gone usi-take place tafadhali
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hilo tamko halikubaliki hata tone:

  Sasa ndio tutaonana wabaya kila kona ya nchi hii na wanachi tutajikamilishia kila kitu kuhusiana na Katiba Mpya ifikapo Decemba 2012 'WITH OR WITHOUT CCM IN POWER'!!!

  Ratiba ya utungaji wa Katiba mpya uende vipi wala si miliki ya watu wachache serikalini; tamko hilo linaweza tu kutolewa na MKUTANO MKUU WA TAIFA KUHUSU KATIBA hivyo CCM isijisumbue kutangaza jambo ambalo hawana haki nayo.

  Katiba ni wa watu wote hivyo huwezi kuamka asubuhi moja na kujiamulia tu juu ya ratiba inyohusu Wa-Tanzania wote tukakubaliana wote.

  Oliver ametumia vigezo gani kufikia tarehe aliyoitamka, kwa ruksa ya nani na nani kamtuma??? Mtu yeyote asithubutu hata dakika moja kuleta utani kwenye swala la ktiba na huo mswada mlioahidi kwenda bungeni Aprili maana juu ya hili vijana tumejiandaa ile mbaya usipime!
   
 4. N

  Nonda JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  This gvt is not serious at all, 2014 mwishoni ndio wataleta katiba. 1 year kuipitisha .Uchaguzi mkuu. baada ya uchaguzi mkuu then 1 year after kuunda tume ya uchaguzi..vyama vya upinzani vimepigwa bao la kiufundi kama watakubali ratiba hii.
  au ndio wanajaribu kupima upepo?

  CCM na serikali wanafanya utani ambao haustahiki kabisa. Ni dalili wameshaichoka"amani na utulivu".
   
 5. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #5
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  CHADEMA TUPENI MELEZO HARAKA JUU YA SWALA ZIMA KATIBA MPYA NA
  TUME HURU YA UCHAGUZI

  Uongozi wa juu CHADEMA, kama jambo la dharura kitaifa, tunaomba ufafanuzi wenu juu ya hizi KERO ZA KUPIGISHA DANADANA SWALA ZIMA LA KATIBA MPYA NCHINI na vile vile mtufahamishe kwamba mpaka hivi sasa nyinyi wenyewe mnafahamu nini na mmeshirikiswa kiasi gani juu ya SWALA MASWALA NYETI ya:

  1. Tarehe ya muswada kupelekwa bungeni???
  2. Muswada wenyewe huo ni wa aina gani na je unasema kama wananchi tunavyotaka wenyewe???
  3. Haki ya serikali ya CCM kujipangia ratiba ya zoezi hili muhimu sana kwa maisha yetu kitaifa wamepata wapi??
  4. Je, inamaana CHADEMA hamtaki kutii amri yetu wananchi kupeleka mswada wetu kule bungeni kupitia kwa dogo Mnyika???

  NB: CHADEMA tupeni majibu ya uhakika na kwa haraka sana juu ya hili swala ambalo kumbe huko serikalini wameligeuza mdoli. Mungu wangu kumbe hawa CCM wapuuzi hivi?? Ngoja!!!!!
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Haitoshi kusema katiba mwaka 2014; tunataka uchaguzi mkuu ujao ufanyike chini ya Katiba Mpya...
   
 7. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #7
  Mar 24, 2011
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,076
  Likes Received: 1,111
  Trophy Points: 280
  Haya mambo ya kutufanya sisi watoto wala hatukubaliani nayo kabisa

  • Ni kwanini tungoje mpaka 2014?
  • Ni kwanini iwe karibu na uchaguzi? Je hii ni hila nyingine ya kuifanya katiba mpya isiwe effective wakati wa uchanguzi 2015?
  • Ni wanini wakurupuke na hiyo tarehe
   
 8. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #8
  Mar 24, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Msisahau na tume huru wajameni. Hiyo pia ni lazima iwe priority pamoja na katiba mpya.
   
 9. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #9
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Hawa jamaa wanatuona sisi watoto sana ndio maana kwa nini wanataka hiyo katiba ifike mpaka mwaka 2014 wanajuwa kwamba watu nguvu zitakuwa zimeisha au vipi??Tunahitaji hiyo katiba mpya ishughulikiwe mapema hatuhitaji longolong la mpaka 2014.........
   
 10. n

  niweze JF-Expert Member

  #10
  Mar 24, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hivi Kikwete anafikiri yeye ni leader kama Gadaffi au Raisi mteule? Hii tarehe na muda unaotolewa ni yeye peke yake ndio anaamua lini na mpaka lini Watanzania wapete democratic reforms. Kuna kitu kimoja tunajua Kikwete ni mjeuri na very arrogant person. Haoni threat kubwa ya yeye kutotimiza matakwa ya Watanzania. Hili swala la consitustinal and democratic reforms, ccm wanajifanya they have some kind authority.

  Hakuna democratic reforms katika dunia nzima iyaoongozwa na hao hao watawala na wanyima haki. Chadema na wananchi hakika hatuta kaa kimya na hii ndio itatufanye tuandamane kwa nguvu na kufanya kila njia kumwondoa Kikwete na ccm. CCM moment had passed long long time ago and their ideas are down the drain.
  Democratic Reforms And Accountability - ModernGhana.com
   
 11. m

  mzambia JF-Expert Member

  #11
  Mar 24, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  wanafanya hivyo makusudi na hawasemi KATIBA MPYA ITAKUWA TAYARI 2014 BALI MCHAKATO UTAANZA 2014 NA BADO SUALA LA KATIBA MPYA KIMYA MPAKA SASA SIJAMSIKIA HUYO K/MKUU AKIZUNGUMZIA AU LIPO BEYOND HIS/HER SCOPE AU NDO KAULI YA MAKAMBA KWAMBA WATANZANIA NI WASAHAULIFU SANA?
   
 12. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #12
  Mar 24, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Wakati Jk anatangaza mwezi December, wengine tulionya kuwa halikuwa suala la kushangalia bali kutizamwa kwa undan. Jk alifanya vile kuzima hoja za akina Mnyika kwa kumtumia Anne Makinda, na walifanikiwa.Tulionya tume za JK hazina suluhu wala utashi wa kitaifa.

  Katiba ni ya wananchi na si CCM, na nilishangaa hata viongozi wa upinzani hawakuliona hili na kumpongeza JK kwa usikivu! Inaweza kufika 2014 wakaja na visingizio vya kipuuzi na tukaenda 2015 kwa katiba hii.

  2014 ni kumpa Jk muda wa kutawala bila bughudha ili kufanya anayoyataka kwa wakati huo bila kujali maslahi ya taifa zaidi ya CCM na genge la wahujumu.

  Misri walikuwa na tatizo kama letu kwa muda mrefu tu, lakini ni hivi karibuni wameweza tena kwa muda mfupi tu. Sisi Tanzania hatuna matatizo makubwa ya kijamii, matatizo yetu ni ya kiuongozi na kiutawala. Hivi ni kwanini ichukue miaka 2?

  Tuna 'play book' jinsi wenzetu wa nchi kama South Africa na Kenya walivyoweza kufanya na kufanikiwa. Tuna mapendekezo ya tume kama za Nyalali, Kisanga na taasisi za kitaaluma vinavyotupa mwanga wa wapi tuanzie na wapi tujikite zaidi.
  Tunachohitaji ni ushirikishwaji wa umma kutoa maoni.

  Swali la kujiuliza kwanini hili linafanywa na wanasiasa zaidi kuliko wataalam?
  Kwanini suala nyeti kama hili linatolewa ufafanuzi na katibu mkuu na si viongozi wa kitaifa? (litmus test !!!)
  Katiba ni yetu kwanini serikali inaogopa kuwa na mkutano wa kitaifa au kushirikishi makundi jamii kuanzia mwanzo wa mchakato hadi mwisho!.Tukiendeleza dhana ya ukimya na utulivu, tutaongea haya haya 2016.

  Hii ni fursa kwa wapinzani kusimama na kuonyesha njia, kuongoza na kusimamia kile wanachoamini, kuwatoa shaka watanzania kuwa dhamira ipo na wakiungwa mkono wanauwezo wa kuongoza.
   
 13. Jimbi

  Jimbi JF-Expert Member

  #13
  Mar 24, 2011
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 870
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Hawa sisiem wapuuzi kweli! Wanataka kutufanyia "kaunta-attack" kwenye uchaguzi mkuu 2015?

  Hatutakubali kamwe!! Wakati wa katiba mpya, yenye maslahi kwa wananchi wote NI SASA!!!
   
 14. l

  luhwege Member

  #14
  Mar 24, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 90
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Nasikitika sana kuona kioja hicho naita kioja kwa maana naona ccm ndiyo inatoa mwongozo nini kifanyike na lini kifanyike tafadhali wananchi hii ni nchi yetu wote haijalishi ww ni fukara au tajiri tuamke tuanze mageuzi kwa pamoja tutashinda udhalimu huu.
   
 15. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #15
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,403
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Katiba mpya si jambo la kuharakia hata kidogo ili kupisha muda wa kutosha wananchi watoe maoni yao ili katiba iwe ya wananchi na si kikundi cha watu fulani.
  wananchi tushiriki kwa ukaribu mchakato huu mwanzo hadi mwisho.
   
 16. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #16
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  CHADEMA TUPENI MELEZO HARAKA JUU YA SWALA ZIMA KATIBA MPYA NA
  TUME HURU YA UCHAGUZI

  Tafadhali Mhe Dr Slaa, Mhe Mbowe, Tundu Lissu, John Mnyika na Uongozi wetu Mzima wa BAVICHA pamoja na Matawi yetu kote nchini na Vyuo Vikuu, tupeni majibu sisi wapenzi na wanachama wa CHADEMA kwamba haya ya Oliver Mhaki yatoka wapi na kwa ruksa ya nani tena???

  Chonde tuokoeni na hizi hasira na kinyaa cha ofisi za Waziri Mkuu na Wizara ya sheria: Uongozi wa juu CHADEMA, kama jambo la dharura kitaifa, tunaomba ufafanuzi wenu juu ya hizi KERO ZA KUPIGISHA DANADANA SWALA ZIMA LA KATIBA MPYA NCHINI na vile vile mtufahamishe kwamba mpaka hivi sasa nyinyi wenyewe mnafahamu nini na mmeshirikiswa kiasi gani juu ya SWALA MASWALA NYETI ya:

  1. Tarehe ya muswada kupelekwa bungeni???
  2. Muswada wenyewe huo ni wa aina gani na je unasema kama wananchi tunavyotaka wenyewe???
  3. Haki ya serikali ya CCM kujipangia ratiba ya zoezi hili muhimu sana kwa maisha yetu kitaifa wamepata wapi??
  4. Je, inamaana CHADEMA hamtaki kutii amri yetu wananchi kupeleka mswada wetu kule bungeni kupitia kwa dogo Mnyika???

  NB: CHADEMA tupeni majibu ya uhakika na kwa haraka sana juu ya hili swala ambalo kumbe huko serikalini wameligeuza mdoli. Mungu wangu kumbe hawa CCM wapuuzi hivi?? Ngoja!!!!!
   
Loading...