Serikali: Kama ulighushi vyeti vya form 4&6 na una shahada hata tatu, tutazifuta zote na utaondolewa

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,885
SERIKALI imesema watumishi wa umma wenye shahada ya kwanza hadi ya tatu ambao watabainika kughushi vyeti vya kidato nne na sita watafutiwa taaluma zao.

Wakizungumza na MTANZANIA jana, Naibu Makatibu Wakuu Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Simon Msanjila na Dk. Avemaria Semakafu, walisema kosa lolote la kitaaluma linapobainika kwa mujibu wa sheria litasababisha kufutwa taaluma ya muhusika.

Makatibu hao walikuwa wakizungumza baada ya kufungua mkutano wa baraza la 24 la wafanyakazi wa wizara hiyo mkoani hapa.

"Hata kama ukiwa na elimu ya juu kiasi gani lakini ikibainika kuna ngazi moja umeghushi basi kwa mujibu wa kanuni taaluma yako itafutwa mara moja," alisema Profesa Msanjila.

Alisema zipo mamlaka maalumu zikijiridhisha kama muhusika ana vyeti feki basi taaluma yake itafutwa bila pingamizi lolote.

Naye Dk. Semakafu alisema lengo la uhakiki wa vyeti feki ni kuwa na watumishi wenye sifa na weledi kwa mujibu wa elimu stahiki.

Alisema ukaguzi wa vyeti ni mkakati wa siku nyingi lengo likiwa ni kuboresha elimu nchini.

"Lengo ni kila mtu akae kwenye nafasi na viwango stahiki," alisema Dk. Semakafu.

Awali akifungua mkutano huo, Profesa Msanjila aliwataka wafanyakazi wa wizara hiyo kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake kuwa wabunifu kutokana na mabadiliko.

Alisema serikali imejipanga kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya elimu na imeweka vipaumbele vya msingi kuinua ubora wa elimu katika nyanja zote.

"Serikali imejipanga kuwa na elimu yenye ubora katika viwango vya ndani na nje ya nchi kwa kusambaza vifaa vya maabara, hivyo acheni kufanya kazi kwa mazoea. Mnatakiwa kujituma kwa weledi mkubwa na kuangalia matokeo ya kazi,” alisema.

Wakati huo huo, Serikali imesema watumishi ambao wamekata rufaa baada ya kubainika kuwa na vyeti feki hawaruhusiwi kuendelea na kazi hadi rufaa zao zitakaposikilizwa.

Chanzo: Mtanzania
 
Nadhani tunakoenda inabidi watafutwe popote walipo na kuvutwa sharubu na kama hawana sharubu basi wavutwe maziwa. Maumivu kwa nchi sasa yamepata mwarobaini wake. Kisiki cha mpingo, JPM May almighty God keep on sanctifying the Nation.
 
Hivi nao waandishi wanapoambiwa hizo ngonjera hakuna mwenye ubavu wa kuuliza kwanini wanasiasa hawaguswi, tena ikibidi waulize khs mteule wa Rais.......IPO haja mashirika ya haki yakaingilia kati hili suala, kwanini iwe kwa baadhi ya watu, wote ni Watanzania na tuna haki sawa.
 
Profesa Paramagamba John Aidan Kabudi

Sawa kabisa wewe Mtu mdogo. Unadhani kwa nini mkuu kamteua haraka kabla ya kufunuliwa walio kwenye orodha?? Hapo sasa, tujifiche kwenye siasa halaf vumbi likitulia, tuendelee na vyeti vyetu mkuu. Wote fukuza na ondoa kwenye listi ya wasomi Tz kasoro Bashite na ikabudi
 
Back
Top Bottom