Serikali iweke adhabu ya kifo kwa wauzaji wa madawa ya kulevya na majangili wa faru na tembo

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,950
Wana jamii
Salaam

Ndugu Watanzania ili kuokoa kizazi hiki kisiendelee kuathirika haswa katika masuala mazima ya matumizi na biashara ya madawa ya kulevya ambayo yameathiri sana afya, akili na maadili kwa ujumla, Vilevile katika suala kupambana na majangili wa Tembo na Faru ambao ni wanyama adimu duniani, serikali ione haja ya kurekebisha kanuni za adhabu katika makosa hayo makuu mawili yaani kosa la kufanya biashara ya madawa ya kulevya na kosa na kuwinda na kusafirisha pembe za faru au meno ya tembo, adhabu iwe ni kunyongwa hadi kufa hii itasaidia sana katika kudhibiti biashara hizo na ujangili wa Faru na Tembo, kwani hukumu za sasa zinazotolewa za kumfunga mtu miaka kadhaa haisaidii kuondoa mtandao mzima wa uhalifu huo lakini unyongaji utasaidia sana kukata mawasiliano hayo.
 
Kazi bure mpaka sasa umewahi sikia kuna muuza sembe hata mmoja aliekamatwa hapa bongo? si unaskia wengi wao wanakamatwa china na baadhi ya nchi mfano dubai na brazili.
 
Wana jamii
Salaam

Ndugu Watanzania ili kuokoa kizazi hiki kisiendelee kuathirika haswa katika masuala mazima ya matumizi na biashara ya madawa ya kulevya ambayo yameathiri sana afya, akili na maadili kwa ujumla, Vilevile katika suala kupambana na majangili wa Tembo na Faru ambao ni wanyama adimu duniani, serikali ione haja ya kurekebisha kanuni za adhabu katika makosa hayo makuu mawili yaani kosa la kufanya biashara ya madawa ya kulevya na kosa na kuwinda na kusafirisha pembe za faru au meno ya tembo, adhabu iwe ni kunyongwa hadi kufa hii itasaidia sana katika kudhibiti biashara hizo na ujangili wa Faru na Tembo, kwani hukumu za sasa zinazotolewa za kumfunga mtu miaka kadhaa haisaidii kuondoa mtandao mzima wa uhalifu huo lakini unyongaji utasaidia sana kukata mawasiliano hayo.

Na vipi kuhusu majangili wa escrow?
 
Kifo ni adhabu stahiki kabisa I agree
Adhabu ya kifo kwa muuzaji haisaidii na ndiyo maana nchi zenye biashara kubwa za madawa ya kulevya hakuna adhabu kama hiyo.

Maadili kwa kijana wako ni njia muhimu sana na sahihi ktk kutoingia ktk vitendo viovu.

China wananyonga sana,Iran wanyanyonga sana Thailand ndiyo shida sana Myanmar ndiyo usiseme kwa mihadarati pamoja na adhabu Kali lakini kila kukicha mbinu mpya zinagunduliwa za uuzaji.

Walimaji wenyewe sasa Pakistan na Afghanistan ndiyo shida kubwa pamoja na sharia laws kutumika lakini bado.

Latin america nchi za america ya kati na kusini ni tatizo kubwa sana kiasi ambacho hata serikali wenyewe ziko alert muda wote kwani magenge haya ya wauzaji yana nguvu ya fedha na silaha mengine kupiga hata hizo serikali.

Hii ni vita ngumu sana ambayo Inahitaji maamuzi magumu ya kidunia yaani global world leaders kwa pamoja waamue jambo na si kila nchi na Sera zake ni ngumu sana.

Hawa wakina Guzman el campo wako wengi sana duniani ma tycoon ya kuuza hizi dawa wenye kumiliki vikundi vya kijeshi vyenye silaha ni vingi.
 
Hata hapa kwetu nadhan haya makund yapo na huenda wanaendesha biashara yao chin ya intelijensia ya hali ya juu...
Hata kwa kipind hiki ambacho biashara nyng zmepata msukosuko nchin lkn jamaa bado wanapiga pesa kama kawa viashiria vikiwa ni kuongezeka kwa mateja mitaan kila iitwapo leo...
Mungu Baba aingilie kati maana hakuna namna nyingne
 
Sisi tz bado kama ni biashara ni kidogo sana hata hao unaowaita mateja watumiaji wa madawa ni kidogo sana.

Tz ni kama njia ya kupita tu hayo madawa si destination ya biashara hakuna watumishi hapa.

Tatizo letu Tanzania tukishaona mwanamziki au msanii au mchezaji Moira mmoja ameandikwa ktk gazeti na redio zikasoma zile habari na mitandao ikarusha picha zake basi tu najua sasa Tanzania imeoza kabisa kwa biashara ya madawa ya kulevya kumbe hata ukucha haujai.

Sikatai kuwa hatuna shida hapana shida IPO ila siyo kwa jinsi ilivyopokelewa na jamii kupitia vyombo vya habari.

Time ya kudhibiti ya madawa ya kulevya na Wizara ya afya wanatakiwa watoe takwimu sahihi kuonyesha ukubwa wa Tanzania kitu ambacho hakijawi kufanyika kwasababu utumiaji madawa ni against the law na Drug Act ya 2015.
 
Mtoa post huna nia njema na CCM. Huna hata habari kuna vikundi vya ujangiri vya chama? Huna habari ya mgao wa fedha toka kwa drug dealers, mnakomalia mateja mkidhani ndio wauzaji. Huna hata habari kuwa faru John aliuzwa kugharamia kampeni ila wakubwa hawakuwa na habari?! Walipokomalia faru John faru John yuko wapi ikabidi waambiwe ukweli, tangu hapo serikali ikaagiza hakuna kuongelea tena habari za faru John. Wewe unaishi Tanzaniaya wapi wewe??
 
IDD azan chama gani vile.Nina wasiwasi makada wengi wa ccm.watakwenda na maji.
 
Mtoa post huna nia njema na CCM. Huna hata habari kuna vikundi vya ujangiri vya chama? Huna habari ya mgao wa fedha toka kwa drug dealers, mnakomalia mateja mkidhani ndio wauzaji. Huna hata habari kuwa faru John
aliuzwa kugharamia kampeni ila
wakubwa hawakuwa na habari?! Walipokomalia faru John faru John yuko wapi ikabidi waambiwe ukweli, tangu hapo serikali ikaagiza hakuna kuongelea tena habari za faru
John. Wewe unaishi Tanzaniaya wapi wewe??

Mkuu Kwani ccm inahusikaje hapo sasa, mi nimetoa rai kwamba majangili wa faru na tembo na wauza ngada wanyongwe tu,
 
Mtu akikamatwa kwa ujangili na akathibitika, dawa yake ni kupelekwa kwenye kundi la Nyati akabidhiwe huko, bila kumfunga kamba wala kupepesa macho. Nafikiri nyati wakimaliza kazi yao, fisi watasaidia mazishi
 
Hahaha umetisha mkuu
 
Hao hawaitwi majangili , wanaitwa mafisadirization na wahujumu economization hahahahah

Vyovyote vile mkuu. Hata wangeitwa wenyenchi or anyhow, je madhara yake kwa taifa yanapewa uzito gani ukilinganisha na yanapoiba mali asili zetu? Ni madhara yapi yana ahueni?

Ni majambazi yote tu, yanaua taifa kwa ubinafsi yakena hayapaswhi kutofautishwa.
 
Hayo yameshatengewa mahakama yao inaitwa mahakama ya majizi na mafisadi
 
Haijalishi ni mahakama gani inasimamia. Kikubwa ni tafsiri ya kosa kisheria, uzito ambao sheria inalipa hilo kosa na hukumu ya kosa hilo kisheria kama linaendana na madhara ya kosa hilo kwa muathirika ambalo ni taifa.

Kukosekana kwa nguvu katika sheria ya haya madudu, ndiyo imewapa ujasiri wasimamizi wa serikali kutamka bila hay akwamba Tanzania hakuna mafisadi!.
 
Back
Top Bottom