Serikali iwe na kauli moja kuhusu kusitishwa kwa msaada kutoka MCC

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
14,409
13,260
Wakati fulani niliwahi kutoa mapendekezo kupitia jukwaa hili kuwa ni vema serikali yetu ikafikiria kuwa na utaratubu wa kuwa na msemaji wa ikulu ambaye ndiye atakaye kuwa anatoa taarifa rasmi za serikali ambazo akishatoa yeye hakuna tena viongozi wengine wa serikali au chama kuandaa matamko na kuitisha mikutano ya waandishi wa habari kuzungumzia suala lie lile lililozungumzwa na Msemaji wa Ikulu.

Hii ni kwasababu katika nchi yetu kumekuwa na tabia ya kila kiongozi kuanzia kurugenzi ya mawasiliano ikulu, mawaziri, viongozi wa chama na wengine wengi wengi katika serikali na chama kutoa matamko yanayotofautina katika suala moja hivyo kuwa kama wahenga walivyo sema miluzi mingi humpoteza mbwa. Mfano hivi karibuni baada ya kusitishwa kwa msaada kutoka MCC alianza waziri wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa akatoa taarifa ya serikali kuelezwa kusikitishwa kwake na kusitishwa kwa msaada huo huku akilalamika sana kuwa serikali kuna mengi mazuri imefanya hivyo watoa misaada wangaeangalia na mema ya nyuma. Hatuja kaa sawa waziri mwingine anayehusika na nishati naye katoa yake kuwa kusitishwa kwa msaada huo hakuta athiri malengo ya serikali.

Hatuja kaa sawa kaja mwingine na kusema kuwa walishajua kuwa MCC watachukua hatua hiyo ndiyo maana hawakuweka hata kwenye bajeti ya serikali msaada huo. Hatuja kaa sawa rais naye kazungumza akiwa huko kwao Chato kuwa misaada ina masharti hivyo tujipange kujitegemea kwani sisi ni matajiri isipokuwa tumeukalia utajiri. Kwenye chama nako kuna magenge yameundwa kukandia uamzi wa MCC yakiongozwa na Haraka haraka. Bado utasikia kesho chama upande wa Zanzibar nao watakuwa na tamko. Ili mradi imekuwa ni matamko matamko kila kukicha kuhusu suala moja ambalo serikali ilipaswa kuja na kauli moja baada ya kulitafakari katika cabinet na sio kila mtu kutoa tamko

Hivyo ni vema serikali ikaanzisha utaratibu wa kuwa na utaratibu wa Msemaji wa Ikulu kama ilivyo katika nchi nyingine kama Marekani.
 
Hivi tuna wahisani au tuna wasanii maana nilifikiri kipindi hiki ambacho pesa zao zingesimamiwa vizuri wao ndiyo kwanza wanaleta vikwazo siwaelewi kimsingi kama kweli wana nia njema na sisi wataalamu wa mambo haya tujuzeni
 
kwa wenye akili wangechukua ushauri huu. maana kwa wanajukwaa wenzetu utawasikia hatuhitaji misaada huku serikali inahutaji mnooo!
 
Back
Top Bottom