MAKOLE
JF-Expert Member
- Feb 5, 2012
- 620
- 282
Wakati fulani nilipata kusikia kuwa Serikali ya Kenya imepiga marufuku utumaji wa meseji nyingi kwenye simu za viganjani pasipo makubaliano ya Mteja na watumaji. Hii ilikuja baada ya kuona tishio la uchochezi wa kikabila kupitia meseji za simu hizo.
Hapa kwetu kumekuwa na utumaji wa meseji nyingi zenye kulenga kuchochea hisia au vurugu za kidini. Natumaini makampuni ya simu yanapata faida kubwa sana kwa meseji hizi. Pia naamini mamlaka ya mawasiliano huwa wanafahamu ni nani wankuwa ndio vyanzo (source) wa meseji hizi. Kwa kweli hali ni mbaya sana.
Niliwahi kusikia kwamba zipo kampuni ambazo huwa zinaingia mikataba na Makampuni haya ya simu ili kutuma meseji nyingi (sijathibitisha jambo hili; wanaofahamu watanitanabaisha zaidi). Kama hivyo ndivyo, basi yapasa kuwa na uthibiti wa aina za meseji za kutuma,La si hivyo basi Serikali ipige marufuku hizi ofa za meseji kwani ndizo zinazoshawishi uchochezi huu.
Njia nyingine ni kwamba viwango vya meseji viwe juu kuliko kupiga ili watu wasipate hamu ya utumaji wameseji.
Hali hii twaweza kuipuuza sasa lakini yaweza kuwa na hatari juu yake! Alamsiki wapendwa.