SERIKALI IWAPANGIA WANANCHI IDADI YA MANENO YA KUONGEA KWA SIKU

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,902
52,003
Nimetafiti nikagundua nchi zilizoendelea watu si waongeaji sana.Huongea maneno machache sana.Mfano WAJAPAN,Wazungu,Wakorea na Wachina.Nikaona kuna uhsiano kati ya kuongea na maendeleo.Wale wanaoongea sana hawana maendeleo wale wanaoongea maneno machache wana maendeleo.

Watanzania wanaongea sana iwe bungeni,kazini,mitaani yaani ni kuongea kuongea kuongea utafikiri midomo imewekwa pilipili

Watanzania wanaongea sana tena sana. Kama mwenyezi Mungu angekuwa aliweka idadi ya maneno ya kuongea mfano kuwa katika maisha ya mtu akiongea maneno elfu kumi anakuwa kamaliza mgao wake na anakuwa bubu,Tanzania ingeshakuwa nchi ya mabubu WATUPU kuanzia kwa wabunge hadi wananchi wa kawaida maana mgao wao ungekuwa ulishafikia kikomo.

Ili nchi iendelee nashauri serikali ipeleke mswada bungeni wa idadi ya maneno ambayo mtanzania anatakiwa kuongea kwa siku awe bungeni,kazini au popote ili ule usemi wa Hapa Kazi tu uweze kufanya kazi.
 
Back
Top Bottom