Serikali iwamulike hawa manabii




wewe vp? yamekujaje haya?
 
Kuna Mmoja yupo Channel Ten Mimi Uwa nashangaa maana Majisifu, Majivuno na Maringo yake Utadhani ni Comedi. Kweli Manabii wengine ni wa uongo.

Eti Nabii Mkuu. Kwanza nabii wa kweli Uota ndoto na anayo Maono, tofauti na Misifa Wanayojitafutia Kwenye TV. Hapana Manabii Kama huyu Jamaa Mimi Naona Hakuna Kitu na Deal tu. Mtu anajiinua na Kujitukuza hata Kuliko Mungu.

Hata sheltani alipata kuwa malaika Mkuu lakini tusisahau bado Sheltani alibaki na Nguvu Kuu alipotelemshwa hapa Duniani.Nikujiinua, Kujiinua na Kutafuta popularity Kwa Kwenda Mbele. Mtumishi wa Mungu Siku zote Ujishusha na Wala sio Kujikweza na Kujipandisha kama awa Manabii wa ajabu.
 

Nahisi una tatizo la kutumia kilichomo katikati Masaburi ktk kufikiri badala ya Ubongo uliomo Kichwani
 


mungu/MUNGU yote yana maana moja....kuandika herufi ndogo hakupotezi maana ya neno MUNGU
 

Wanyang.'anyi wanao wanyang.'anya watu walio nyang.'a nyang.'a .!
 
Acha mtapeliwe si mnasali ktk makanisa ya wanadamu baala ya kanisa alililoacha Yesu ambalo ni Catholics! badala yake mnatapeliwa kule 'mlima wa baridi', 'kanisa la kufukua', 'kanisa la efwatwa' kwa 'mzee wa upwakwa' 'kanisa la kikobe' nk

Wewe umepotoshwa, halafu unataka kupotosha wengine! Acha upotoshaji wewe, tafuta Kitabu cha BWANA ukasome! (ISAYA 34:16). Yesu hakuacha kamwe kanisa la Catholics! Yesu hakuwa Mkatoliki. Yeye alibatizwa katika maji tele (MATHAYO 3:13-17), tofauti na Wakatoliki. Vilevile, tofauti na Wakatoliki wanaopinga juu ya kuokolewa, Kanisa aliloliacha Yesu lilikuwa la watu waliookolewa: MATENDO YA MITUME 2:47,"...Bwana akalizidisha KANISA kwa wale waliokuwa WAKIOKOLEWA." Eti Makanisa ya wanadamu! Kwa taarifa yako, Mungu anafanya kazi na wanadamu (1WAKORINTHO 3:9; EZEKIELI 22:30). Tangu Kitabu cha MWANZO, Mungu anatajwa kufanya kazi na wanadamu, ambao hata taasisi zao hazitajwi: Nuhu, Ibrahimu, Isaka, Yakobo, Musa, Yoshua, Eliya, Elisha, Yohana Mbatizaji, Petro, Yohana, Paulo n.k.
 

Mkuu wewe unasali wapi? kanisani au 'nyumbani kwa mtu'? Pole mkuu!
 

Mkuu mi nafikiri ungejadili usahihi wa alichowasilisha na si kumvamia yeye kama yeye. Sioni hata kosa lake ni nini maana yeye amesema anachokiona, ni vizuri na wewe ukasema kile ambacho sicho
 
Acha mtapeliwe si mnasali ktk makanisa ya wanadamu baala ya kanisa alililoacha Yesu ambalo ni Catholics! badala yake mnatapeliwa kule 'mlima wa baridi', 'kanisa la kufukua', 'kanisa la efwatwa' kwa 'mzee wa upwakwa' 'kanisa la kikobe' nk

Hebu onesha aya kwenye Biblia kwamba Yesu aliacha kanisa katoliki duniani!
 
Acha mtapeliwe si mnasali ktk makanisa ya wanadamu baala ya kanisa alililoacha Yesu ambalo ni Catholics! badala yake mnatapeliwa kule 'mlima wa baridi', 'kanisa la kufukua', 'kanisa la efwatwa' kwa 'mzee wa upwakwa' 'kanisa la kikobe' nk

Ni kweli Yesu amelihacha kanisa catolic yupo kwenye msingi ambao ni mitume na manabii.
 
mungu/MUNGU yote yana maana moja....kuandika herufi ndogo hakupotezi maana ya neno MUNGU

Ukiona neno mungu kwenye biblia maana yake si MWENYE ENZI MUNGU hata shetani anaitwa mungu.
 
Mambo Ya Rohoni Utambuliwa Na Watu Wa Rohoni Tu, Kwa Iyo Kama Wewe Ni Mkristo Lkn Hujaokoka Bado Huwez Kuelewa Mambo Ya Mungu. Sasa Ni Wakati Wako Kumkiri Yesu Na Kumwamini Kuwa Mwokozi Na Roho Mt. Atakufundisha Yote. Injili Pia Inahtj Pesa.
 
kweli umenena ila sikuungi mkono kutaka serikali iwamulike. wananchi ndio watafakari mara mbili kama kweli hao matajiri wanaweza kuwapeleka mbinguni wanakoamini. kuna mmoja wa arusha anatishaaaa!
 
ibanezafrica

Mathayo 24-26
Yesu akajibu akawaambia,"angalieni mtu asiwadanganye,kwa maana wengi watakuja kwa jina langu wakisema,Mimi ni kristo.nao watadanganya wengi.
Kwa maana watatokea MAKRISTO WA UONGO,na MANABII WA UONGO.
Nao watatoa ishara kubwa na maajabu,ili wapate kuwapoteza.....

Sio kila anayeita bwana bwana.....
 
Last edited by a moderator:

Wewe ni waku-ban kabisa maana ni mwongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…