Serikali iunde upya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) imeutelekeza wajibu wake

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
18,800
22,505
Shirika la Viwango la Taifa (TBS) lina umuhimu sana kwa taifa kuliko wengi tujuavyo. Bidhaa zetu zikiuzika nje ya nchi basi inatokana na ubora uliohakikishwa na TBS.

Hivi sasa TBS imetelekeza wajibu wake wa kudhibiti ubora wa bidhaa zetu. Mfano: Mimi ni mnunuaji sana wa mafuta ya Sundrop ya lita moja, lita tano na lita kumi inawezekana yako kwenye kiwango kizuri lakini vifungashio vyake hasa vifuniko havifai kabisa kwani hupasuka vikiwa dukani!

TBS imeweka viwango kwenye mikate huko ndiyo usiseme kabisa kwani mingi iko kama ugali na haieleweki, kwa wale waliowahi kula mikate ya SIHA, Shoprite na Gloria kwa uchache watanielewa.

Unga wa sembe na dona unaosagwa mitaani mwingi unanyuzinyuzi za viroba na bidhaa nyinginezo za vyakula haviko salama pamoja na vibiriti vyenye viwango hafifu vinauzwa mitaani.

Kwa haya machache TBS izilinde afya zetu wanunuzi kuliko kuvilinda viwanda kwanza.
 
Weledi wa watendaji ndio unatakiwa. Miongozo kwenye makaratasi ipo vizuri.
 
Uko sahihi mkuu, umesahau bidhaa za Mo karibu zote, mafuta yake ya dumu 20ltr ni hatari sana, kifungashio cheke unaweza kufungua na kuweka sumu na ukafunga tena bila mtu kujua.

TBS na TFDA wapo ofisini wanapunga upepo tu wakisubiri mwisho wa mwezi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom