cjilo
JF-Expert Member
- Sep 8, 2011
- 884
- 444
Naandika uzi huu kwa masikitiko makubwa, serikali ya CCM imetufikisha pabaya sana kiuchumi.
Pamoja na ushauri uliokuwa ukitolewa na viongozi wa dini, asasi za kiraia na wapinzani kuwa mchakato wa katiba mpya uvunjwe na bunge lisiendelee na vikao vya kuijadili serikali ikiongozwa na Sita ilijifanya kichwa ngumu.
Mchakato huo toka mwanzo haukuonesha kama utakamilika zaidi ya kutupotezea muda na fedha. Pamoja na hayo bado mchakato umeacha aibu kubwa kwa CCM na Mh Kikwete.
Ni wazi kuwa huu mchakato hauwezi kuwepo tena kabla ya uchaguzi mkuu au hata baada ya uchaguzi mkuu.
Mamilion yaliyopotea yangeweza kutumika kununua madawa ya hospitalini na kuokoa maisha ya watanzania wagonjwa.
Serikali ilikosea, inakosea na itakosea pasipo kujitokeza hadharani na kukiri makosa na kutuomba msamaha.