Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,694
- 149,917
Uamuzi wa serikali kufuta sherehe za muungano ni jambo jema kabisa na bado naamini kuna maeneo mengine mengi tu ambayo tunaweza kuokoa fedha kwa style hii.
Hata hivyo,kututajia tu kuwa zilitengwa zaidi ya shilingi bilioni 2 kwa ajili ya sherehe hizo pasipo kutupa mchanganuo wake si jambo jema sana hivyo ni vizuri serikali ikatoa mchanganuo ulivyokuwa maana hicho kiasi cha fedha ni kikubwa mno kiasi kwamba kinahitaji kuambatana na ufafanuzi/mchanganuo wake.
Tukijua mchanganua huo leo hii tunaweza kukuta kuna matumizi yasiyoingia akilini na hivyo mwakani tunaweza kuepukana nayo kwani tutakuwa tumeyabaini hivi sasa na hivyo kuyaondoa katika bajeti ya mwakani maana hizi sherehe bado zipo na wala hazijafutwa rasimi.
Naongea haya kwa nia njema tu maana tunaweza kujikuta "tunatakatisha fedha haramu" kwa mtindo huu pasipo kujijua.
Tuchukue hatua zitakazosaidia kutupatia "permanent solution" na si "temporary solution".