Serikali itoe tamko juu ya hili. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali itoe tamko juu ya hili.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mkulia, Sep 28, 2012.

 1. M

  Mkulia JF-Expert Member

  #1
  Sep 28, 2012
  Joined: Apr 26, 2012
  Messages: 343
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Naomba serikali yetu hususa wizara ya utumishi itoe tamko juu ya mavazi sehemu za kazi. Hivi sasa imekuwa ni majezi ya timu mbalimbali kuvaliwa sehemu za kazi. Utamaduni huu jamani unatokea wapi? Hebu fikiria mwalimu anavaa jezi darasani au nguo zenye kubana wenyewe wanaita "modal" au suruali chini ya makalio. Je,mwanafunzi anajifunza nini kupitia kwa walimu hawa? Naomba serikali ione athari juu ya utamaduni huu na itoe tamko.:nono:
   
 2. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #2
  Sep 28, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  mbona muongozo wa mavazi katika serikali na taasisi za umma umeelezwa vyema kwenye kanuni za kudumu za kazi(standing orders).unataka kauli ya nini?
   
 3. B

  Bahati Risiki JF-Expert Member

  #3
  Sep 28, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 531
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hivi kweli unaiona Tanzania kuwa ina serikali? Mbona isitoe tamko kuhusu swala la Ulimboka, Daudi Mwangosi, Ally na wengine wengi waliofanyiwa vitendo vya aina hyo. Kama inayafumbia macho haya itawaona walio wanaovalia suruali chini ya makalio? Wewe tangu uzaliwe ulishaona serikali inafunga vyuo vya elimu ya juu kwa miezi kadhaa eti kwa kuwa pesa za kuviendeshea vyuo hivyo zimeenda kununua tishert, kanga, kofia, na takataka nyingine za kampeni? Uneshaona serikali ambayo watu wanajitangazia ujambazi kiasi cha kuchoma raia sindano za sumu, kuwachomea nyumba, wake na watoto? Ulishaona serikali ambayo waislam wanaamka kwenda kuwachomea wakristo nyumba, magari, mabanda ya nguruwe, na nyumba zao na wasichukuliwe hatua yeyote? Ulishaona wapi serikali ambayo polisi wake wanatoka kwenda kuwalipua raia na mabomu kama wanyama? Ni wapi ilipatikana serikali ambayo inaokota rushwa, kuwaachia wahalifu na kuwafunga watu wasio na hatia?
  Je hii ni serikali au ni usanii?
   
Loading...