Kkimondoa
JF-Expert Member
- May 31, 2014
- 4,453
- 4,933
Niipongeze serikali kwanza kwa taarifa nlizo pata kuwa imetoa waraka wa likizo ambao utafuatwa huo na shule zote tanzania kama tetesi hizo ni kweli basi nayo ni hatua moja kubwa
Lakin niombe hili ambalo pia linaleta usumbufu mkubwa sana swala la masaa ya masomo hasa siku ya ijumaa ,hili linachanganya sana maana shule zingine wanatoka saa 6 wanafunzi wote na shule zingine wanatoka saa nane na nusu, zingine saa kumi yaani mambo haya eleweki kila mkoa una taratibu zake ,kila wilaya ina taratibu zake
Kibaya ni kwamba baada ya waislam kwenda masjid wengine huku wana endelea na taratibu zingine za masomo hasa kwa mikoa ambayo idadi ya waislam sio kubwa kitu ambacho kina wakosesha haki waislam wachache walio enda swala, maana na wao wana haki sawa na walio baki , kwenda kwao msikitini sio sababu ya kuwaadhibu kwa kuto shiriki katika shughuli au masomo au michezo inayo endelea wakati wapo ibadani
Niiombe wizara husika ilitazame na hili pia maana linaleta usumbufu mkubwa sana hasa kwa waumini wa dini ya kiislam kukosa haki ambazo wengine wanazipata pindi wao wanapo kuwa kuswali
Bora serikali itoe waraka mmoja wa wa masaa ya masomo nchi nzima kama ilivyo fanya kwenye likizo ,hasa siku ya ijumaa ijulikane je wanao baki wanaendelea na masomo au michezo wakati wengine wapo msikitini ilihali nao wana haki ya kushiriki michezo!? Au mda wa kuswali wanafunzi wote warudi makwao . utoke tu waraka , maana sasa kila mkoa /wilaya au kata ina utaratibu wake unao leta mkanganyiko