Barakaeli174
Senior Member
- Aug 2, 2015
- 171
- 142
Niseme tu kwamba gorofa za Wizara mbali mbali zilizopo dar es salaam hazijajengwa ndani ya miaka 5 zote zikakamilika, wizara ya Mali asili ilijengwa na jengo bado jipya huku wakijua serikali lazima ihamie Dodoma. Je katika bajeti ya mwaka wa fedha 2016-2017 kuna bajeti ya ujenzi wa ofisi ya waziri mkuu Dodoma? anahamia mwezi 9 maana yake yeye na watumishi wake lazima wapate jengo dodoma kwa gharama yoyote, kama ni kukodi jengo la mtu binafsi ni vema pesa za kukodi zianze ujenzi ili ofisi itakapo kamilika wahamie maramoja ( tuangalie double spending) unaacha jengo lako dar unaenda kupanga, serikali ya mtaa na serikali kuu haina majengo ambayo yalikuwa hayatumiki ili yawapokee watumishi wote waanze kazi mara moja. naomba mnisaidie kujibu maswali haya ili tukubaliane wote:
1. watumishi wenye familia zao dar na wameisha jenga wataenda kuanza maisha mapya dodoma kwa nyumba za kupanga je kodi za kulipa advance ya miezi 6 wataipata wapi, na sh ngapi itaachwa nyumbani kwa ajili ya matumizi. tayari tumechukua mikopo tumebaki na 1/3 hatuishi tena kama malaika hatuna safari na posho itakuwaje? mishahara haijaongezwa itakuwaje? tutapewa advance kwa ajili ya kulipia nyumba dodoma na kuanza kununua vyombo vya ndani au tutakuwa tunafanya kazi dodoma jioni tunarudi dar?
2. Maghorofa kwa ajili ya wizara huwa hayajengwi kwa mwaka 1 tu huchukua miaka itakuwaje hapa.
USHAURI: Swala hili lingetekelezwa taratibu majengo ya watumishi yakiandaliwa mwaka hadi mwaka, kila jengo la wizara linapokamilika wanahamia na huku mishahara ikiongezwa mwaka hadi mwaka ili kuwawezesha watumishi wasipate shida.
WATUMISHI WOTE WA WIZARA KUANZIA JUMA MOSI YA TAREHE 23/07/2016 USIKU HAKUNA ALIYEPATA USINGIZI KITANDANI HATA HAMU YA KULA TUNDA HAMNA SASA HIVI, WANAFIKIRIA MAKAZI MAPYA AMBAYO HELA YA PANGO ITAKUWA KAZI KUBWA SANA NA MAISHA WATAYAENDESHAJE UGENINI.