choga mkuu
JF-Expert Member
- Apr 11, 2016
- 283
- 110
By Sambaja ( Katbu CHASO IAE)
Serikali ya ccm inatia aibu kitika anga za kimataifa juu ya mambo yafuatayo
1) KUNYANG'ANYA WANANCHI HAKI KISA HAWAITUMII KAMA SERIKALI INAVYOTAKA.
Serikali ya awamu hii ya tano imeamua kuwanyan'anya wananchi haki ya kuangalia na kusikiliza mkutano wa bunge unaorushwa moja kwa moja kwa hoja dhaifu kama WANANCHI wengi huwa hawatazami na kusikiliza bunge wakati Wa mchana , na gharama za urushaji Wa matangazo hayo kuwa kubwa, japo kuna wadau waliojitokeza kugharamia urushaji Wa moja kwa moja Wa mikutano Wa bunge kwa kituo chochote kitakachohitaji msaada .
Lakin serikali kwa kutumia waziri Nape ikaja na kihoja kingine cha kuanzisha kituo cha habari za bunge kinachomilikiwa na bunge kwa dhana ya kurusha vipindi vya maswali na majibu pekee na vipind vingine kurekodiwa . Tujue kuwa kitu kilichorekodiwa huwa kinapoteza uhalisia wake,na hata umuhimu kwa watazamaji maana huchukuliwa ni kama suala la kawaida mno.
Hii ni hatari sana maana kama Leo wameweza kuondoa HAKI ya kuangalia bunge live kisa hatuitumii kama serikali inavyotaka tutegemee HAKI zetu zingine kupokwa na na watawala kisa serikali hairidhiki na jinsi tunavyozitumia, hali ambayo itatufanya siku za ALHAMIS na jumamosi kuambiwa ni siku ambazo kila Mwananchi anatakiwa kuvaa nguo zenye michoro ya NYERERE na pengine za rangi KIJANI,hatutakuwa na nguvu ya kukataa maana tulizoea kukubali makosa yanayofanywa na watawala.
2) SERIKALI KUBADILI MATUMIZI YA FEDHA BILA IDHINI YA BUNGE
serikali yetu imekuwa ikibadili matumizi ya fedha na kuzielekeza ktk matumizi mengine(japo n mazuri pengine) bila idhini ya chombo kilicho na mamraka ya kufanya hivyo. Ikumbukwe katiba imeweka utaratbu wa fedha yoyote kuidhinishwa na bunge matumizi yake(sio rais ) .
Kama hata wakati TAIFA linapoingia kwenye vita fedha bunge lazima likae lijadili budget ya fedha itakayotumika wakati Wa vita hiyo ,KWANINI Leo mh Rais anabadili matumiz ya fedha bila idhini ya chombo kilichopewa mamlaka hayo? Tujue siku moja tukiendelea kuchekelea hali hii viongoz watakula pesa alafu watwambie zilibadilishwa matumizi.
TUKUMBUKE RAIS ZUMA AFRICA KUSINI alishitakiwa kwa makosa kama haya na mahakama ilimwamru arudishe fedha aliyozidisha ktk matumiz yake .