Kama Mwananchi na Mtanzania riba inayotozwa na Mabenki hapa nchini kwa wananchi ni KUBWA SANA. Mfano hai mtu anapokopa anatakiwa kulipa riba ya 19% mpaka 22% wakati mwananchi huyo huyo akiweka fedha zake Benki anapewa riba ya 3%. Hapa hakuna usawa kabisa na kuonekana kuwa wananchi wananyonywa katika nchi yao. Tunaiomba Serikali yetu sikivu isimamie Mabenki nchini ili riba inayotolewa iwe rafiki kwa wananchi.